Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Nzuri sana hasa ukipata RD5, inakamata road vizuri ngumu fuel consuption ni nzuri ndani kuna nafasi ya kutosha pia

Mkuu hizi gari ni super, ndio maana soko lake kubwa liko UK, ni gari nzuri nimeitumia kwa mda mrefu sana
 
Mr mshana naomb na wadau wengine wajuz mnisaidie kati y spacio old model n terious IPI nzuri mana Kazin napandisha mlim
 
Mr mshana na wadau wajuz naomben msaad kati ya spacio old model n terious IPI inafaa n haisumbui mana kazin napandisha mlima
 
Inaweza kuwa kweli, sijawahi kubadilisha nilishasoma kwenye kichwa cha dipstick ya gearbox hydraulic pameandikwa "Do not change under normal operation"

Mkuu Columbus umefanikiwa kutatua tatizo lako?

Naomba tuwe tunapeana mrejesho wa utatuzi wa matatizo kwa manufaa ya wanajukwaa.
 
Naomba kuuliza, kwann toyota passio znauzwa bei nafuu kdogo ukilinganisha na gar znazoendana nazo kama toyota ist. Nini siri ya hz kuuzwa bei nafuu au zna matatzo mengi ukilinganisha na ist? Wajuzi wa magar naomba msaada, nmevutiwa na mwonekano wa passio ila bei yake inanipa walakain kidogo
 

spacio gari nzuri sema haitaki shida... sio gari ya kuendesha rough.kwa barabara zetu za kibongo.. wengi hawakai nazo muda kabla hazijaanza kugonga na kutoa milio.. kama ni mtumiaji mzuri wa gari uta enjoy spacio
 
Nisaidieni wadau jinsi ya kuwa naweka mafuta kwenye gari pale sheli kwa kutumia kadi nataka niachane na hii tabia ya kutoa pesa mfukoni

Mkuu, Tz hii au hiyo shell ni kampuni ya wapi? Nijuavyo hizo system kwa Tz ni km bado kabisa. Unazungumzia EFPOS si ndio? Kama zipo basi kunakua na mashine ambayo lazima awepo operator ukimaliza kuweka mafuta basi unaenda counter na kutaja pump ulojaza anakuomba kadi unalipa kwa kadi baada ya kumpa mhudumu. Sijajua km tumeelewana?!
 

Una maanisha spacio au passo? Sijakusoma vzr
 
wakuu za jumapili...nina gari aina ya PASSO piston 3 inatatizo ambalo nimepeleka kwa mafundi wengi lakini wameshindwa kulikwamua.....

tatizo lenyewe ni kuwa wakati wa asubuhi nikiiwasha huwa haina nguvu nahapo hapo huzima so huwa narazimika kuiwasha kwa zaidi ya mara moja na ili nianze safari inanibid niiache iungurume kwanza kwa zaid ya dakika 5... pia tatizo hili hujitokeza kipindi ambacho gari haijawashwa kwa muda mrefu..jr tatizo lipoi hasa ...je ni sencors tu na je ni ipi?

n.b. gari imefanyiwa service yote pamoja na kuwekwa plag mpya
 

Pole sana mkuu, unaposema nguvu una maanisha 'compression' ya engine au ni kuwa ukiweka gear na kuongeza fuel haiondoki? I pity u brother hope utapata solution tu
 
wakuu naomba kuuliza ubora wa toyota probox van, engine code 1NZ, 1490cc ya mwaka 2009.. nataka kuitumia kwa ajili ya kubeba mizogo midogo midogo ya dukani. maana nimeona ina space kubwa na pia ukikunja kiti cha nyuma ina nafasi ya kutosha kuweka mzigo.. mnanishaurije wakuu kuhusu engine na maintenance yake???
 
Na corolla yangu nayo ina tatizo kama hilo ndugu yangu msaada tafadhali
 
Mhana kwa kuongeza more knowldge kuhusu magari,, usisahau namba hii pia to connect to whatsap group 0713535363,
 

Noted!
 
wadau mwenye uzoefu na gari aina ya mitsubish GDI au io please maana natamani kununua kwa mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…