Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali


mkuu kwa sababu kubwa ni short kwenye otoneta kwenye diode/rectifire kama utaunga huku Gari ikiwa IPO off na hujatoa terminal ya betri inamaana utaruhusu ule umeme wa mashine ya welding uflow mpaka kwenye diode na kuziharibu.

lakini kama utakuwa umeiwasha Gari uhalibifu hauwezi tokea kwa kuwa otoneta inakuwa inafanya kazi na suala LA UMEME Ku flow mpaka kwenye diode hauwezi tokea.

sijui kama utakuwa umenielewa kama utakuwa hujanielewa au utataka maelezo ya kiufundi zaidi nitakushushia tuu.maana hapo upele umemkuta mkunaji.
 
Last edited by a moderator:

Umejifunza lini kupiga ramli? Kwenye post yangu nimeongelea "bei"; sijaongelea engine technology (D4). Mie sio mtaalam wa injini hivyo nisingeweza kushauri kitu nisichokijua. Bila shaka wewe unazimanya sana D4.

Asilimia kubwa ya wanaonunua magari ni vijana, na magari tunayoyanunua si ya kukaa nayo milele. Pia kuna swala la mazingira ya barabara tunazotumia, asilimia kubwa si rafiki kwa magari ya kisasa sana (ambayo bodi zake ni nyanya).

Shida inakuja unapotaka kuliuza ili ununue lingine. Tunafanya kazi ya pannel beating na jamaa yangu, nimeona ni jinsi gani wanaotaka kuuza Vista wanasumbuka. Hivyo ni bora ainunue kwa bei rahisi ili akitaka kuiuza baadae asiumie.
 

Nashukuru mkuu, gearbox ni ya automatic.

Naomba mwenye taarifa ya wapi nitapata hiyo engine ya 1KZ anijuze.
 
Jamani wadau nina RAV4 old model ya 1999
Ina tatizo moja nisipotumia AC baada ya mda kidogo inachemsha
Ila kwa kuwa mda wote natumia AC basi joto linakuwa chini mpaka utaisifia hiyo rejeta yake
Nimejaribu kuichunguza feni ya rejeta labda imekufa lakin inafanya kazi.
Naombeni msaada tatizo itakuwa nini??
 
Wadau kama kuna mtu anauzoefu na hizi Toyota Tactis, naona imenivutia, je nichukue au pasua kichwa #mshana jr,
#LEGE

Kama unamaanisha ractis iko poa,tofauti ni body tu, ractis inatumia engine ya 1nz ambayo ni sawa na funcargo,vitz,raum,corolla,allex,porte,allion ist,sienta ,na platz
 
Nimeuliza swali jamani.............!

Naomba mwenye taarifa ya wapi nitapata hiyo engine ya 1KZ anijuze.
 
Kama unamaanisha ractis iko poa,tofauti ni body tu, ractis inatumia engine ya 1nz ambayo ni sawa na funcargo,vitz,raum,corolla,allex,porte,allion ist,sienta ,na platz

Kweli ni RACTIS mkuu, nimeipenda naona ndani ina nafasi kubwa ila engine ndogo na nasikia hata ukitaka kusafiri haina shida
 
Nimeuliza swali jamani.............!

Naomba mwenye taarifa ya wapi nitapata hiyo engine ya 1KZ anijuze.

mkuu upo wapi wewe kwani ?? hata kama upo mkoani unaagiziwa tuu.zipo nyingi sana mkuu .mm nipo dar zinapatikana sana tuu.sijui unataka 1kz ipi we we.ya kwenye body gani
 
Nataka kubadilisha engine na fuel system yote from petrol to diesel nina nissan xtrail vipi inawezekana?
 

kwa haraka haraka hiyo fen ya rejeta itakuwa na matatizo mkuu.hata kama wewe waiona inazunguka lakini itakuwa haizunguki kwa speed inayotakiwa na je ushawahi badilisha mota ya feni?? na je ushawahi badilisha panga lake?? hapo kama ushawahi Fanya hayo kuna mistake itakuwa ilifanyika.mbali ya kuangalia rejeta kwa ndani Hembu jaribu kuangalia mbele ya rejeta hakuna uchafu /takataka zilizo nasa??. au mbele ya Gari hewa inapita vizuri mpaka kufika kwenye rejeta??.

unapatikana wapi mkuu
 
Nataka kubadilisha engine na fuel system yote from petrol to diesel nina nissan xtrail vipi inawezekana?

ndio mkuu inawezekana vizuri kabisa.labda wataka kufunga engine gani??

ili usitumie sana garama hapo mkuu nunua engine ya Nissan extrail ya diesel unanunua na control yake hapo uta enjoy sana hakuna modification yoyote utakayo ifanya hapo aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…