Kwa wale watumishi wa umma wanaohitaji msamaha wa kodi pindi waagizapo magari, nimeipata hii toka kwenye tovuti ya TRA. Fahamisha na wengine. (Tafadhali usii-qoute hii post nzima, nimecopy baadhi tu ya maelekezo)
Kwa mujibu wa sheria, vyombo vya usafiri vinavyohusika na msamaha huu bila kujali kama chombo kimenunuliwa hapa nchini au nje ni hivi vifuatavyo:-
(a) Magari
i. Magari madogo aina ya saloon.
ii. Magari aina ya pick ? up yenye uwezo wa kubeba mzigo usiozidi uzito wa tani mbili.
iii. Magari mengine ambayo hayabebi zaidi ya abiria tisa.
iv. Gari lenye ujazo wa injini usiozidi 3,000.
v. Gari lenye umri chini ya miaka kumi tangu lilipotengenezwa bila kujali miezi.
(b) Pikipiki za aina zote.
5.0 Ushuru unaosamehewa
Mtumishi wa umma ambaye ametimiza masharti yote yanayotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa
anasamehewa kulipa ushuru wa forodha (import duty) tu. Kodi na ada zingine kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ushuru wa bidhaa (Excise duty) na ada za usajili atatakiwa kulipa.
Zingatia: Mtumishi wa umma akinunua gari lenye umri wa miaka kumi au zaidi toka kutengenezwa hatapata msamaha kabisa.
6.0 Masharti ya kuzingatia kwa mtumishi wa umma. Ikumbukwe kuwa Serikali ina nia njema kwa watumishi wake kutoa upendeleo kwao kwa njia ya msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vyombo vya usafiri. Hivyo ni vema masharti yafuatayo yakazingatiwa: -
(a) Kibali cha msamaha kinachotolewa ni kwa ajili ya mtumishi wa umma anayehusika na sio mtu mwingine yoyote. Ni kosa kisheria kwa mtu yeyote asiye husika kufaidika na msamaha huu, na wala chombo cha usafiri chenye msamaha wa ushuru
hakiruhusiwi kutumika kwa shughuli za biashara.
(b) Msamaha utasitishwa na ushuru uliosamehewa utatakiwa kulipwa mara moja iwapo mtumishi wa umma ataacha kuwa mtumishi wa umma kabla ya miaka minne kupita tangu tarehe ya kupewa msamaha, au iwapo atahamisha umiliki au kuuza chombo hicho cha usafiri kwa mtu mwingine.
(c) Msamaha utatatolewa kwa chombo kimoja tu cha usafiri katika kipindi cha miaka minne. Baada ya muda huo kupita, mtumishi wa umma anaruhusiwa kuomba msamaha mwingine, lakini ni lazima ushuru ulipwe kwa chombo cha usafiri cha zamani kwa kiwango cha uthaminishaji kama ilivyoainishwa na Idara ya Forodha. Thamani itakayotumika
kukokotoa kodi husika ni thamani ya chombo hicho wakati kilipoingia nchini; mmiliki anapaswa kutunza nyaraka zote za chombo hicho cha usafiri vizuri.
Hivyo basi, ili mtumishi wa umma astahili kupewa msamaha mwingine baada ya miaka minne kupita ni lazima aambatanishe maombi yake na stakabadhi ya malipo ya ushuru kwa ajili ya chombo cha usafiri cha zamani toka TRA
7.0 Taratibu muhimu za kufuata Kujaza fomu ya maombi (Nakala nne) ambayo ni lazima iwe na viambatanisho vifuatavyo:-
(a) Magari yanayoagizwa toka nje ya Nchi
i. Barua ya utambulisho toka kwa mwajiri,
ii. Salary Slip ya mwezi wa karibu,
iii. Barua ya kuajiriwa kazini/Barua ya kupandishwa Cheo,
iv. Nakala ya kitambulisho cha kazi,
v. Anatakiwa pia kuambatanisha picha nne (4) za passport size ?kwenye fomu ya maombi,
vi. Kuambatanisha namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN),
vii. Kumbukumbu za ununuzi au uingizaji wa chombo husika cha usafiri hapa nchini.
http://tra.go.tz/publications/Msamaha wa ushuru kwa vyombo vya usafiri kwa watumishi wa umma.pdf