Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Jamani nina gari aina ya brevis.inanisumbua sterring inatetemeka mfano nikiendesha ikiwa speed 120.chini ya hapo inakuwa iko poa tu.nimefanya wheel balance na alignment lakin bado .je hili tatizo litaakuwa inasababishwa na nini?
 
Jamani nina gari aina ya brevis.inanisumbua sterring inatetemeka mfano nikiendesha ikiwa speed 120.chini ya hapo inakuwa iko poa tu.nimefanya wheel balance na alignment lakin bado .je hili tatizo litaakuwa inasababishwa na nini?

mkuu Ngoja waje mafundi machenics mm lingekuwa la UMEME ndio saize yangu
 
Mimi nataka kujua hasaa kuhusu Pajero mini, uimara wake na matatizo yake.
 
Jamani nina gari aina ya brevis.inanisumbua sterring inatetemeka mfano nikiendesha ikiwa speed 120.chini ya hapo inakuwa iko poa tu.nimefanya wheel balance na alignment lakin bado .je hili tatizo litaakuwa inasababishwa na nini?

Uaangalie size ya upepo wa magurudumu ya gari lako kama uko kwa size mojana pia rotter disc zako kama zipo poa na kama zimelika hiyo shida huwa inatokea.Angalia pia brake pads kama zinaliwa upande ujue rotter disc zina kasoro.usifanye refacing endapo disc zitakuwa na shida nunua disc zingine kabisa.
 
Wakuu kama kuna mtu yoyoyte ambaye ana uzoefu na freelander iliyofungwa injini 3s ya Rav 4, anijuze kama hiyo modification haisumbui perfomance ya gari
 
Hivi hii mada bado hakujakuwa na group whatsapp, make tunatuma namber za simu lakini hakuna jitihada za ku-add kama kweli group exist
 
Wadau nataka kujua gari ikitoka japan service gani ni za mhimu kufanya.
Halafu naomba kujua kwa dar au mbeya nitapata wapi duka la spare za nissan
 
Heshima kwenu Banaa..!
Plz,nawaombeni ushauri, nataka kununua gari kati ya Suzuki Escudo new model kwa Arusha wanaziita TANAPA au Toyota Harrier. Plz naomba mwongozo wa ubora, uimara na gharama za matunzo kwa gari hizo au nyingine ni kwa matumizi ya kawaida tu. Thanks in advance..!
 
Kwa wale watumishi wa umma wanaohitaji msamaha wa kodi pindi waagizapo magari, nimeipata hii toka kwenye tovuti ya TRA. Fahamisha na wengine. (Tafadhali usii-qoute hii post nzima, nimecopy baadhi tu ya maelekezo)

Kwa mujibu wa sheria, vyombo vya usafiri vinavyohusika na msamaha huu bila kujali kama chombo kimenunuliwa hapa nchini au nje ni hivi vifuatavyo:-
(a) Magari
i. Magari madogo aina ya saloon.
ii. Magari aina ya pick ? up yenye uwezo wa kubeba mzigo usiozidi uzito wa tani mbili.
iii. Magari mengine ambayo hayabebi zaidi ya abiria tisa.
iv. Gari lenye ujazo wa injini usiozidi 3,000.
v. Gari lenye umri chini ya miaka kumi tangu lilipotengenezwa bila kujali miezi.
(b) Pikipiki za aina zote.


5.0 Ushuru unaosamehewa
Mtumishi wa umma ambaye ametimiza masharti yote yanayotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa anasamehewa kulipa ushuru wa forodha (import duty) tu. Kodi na ada zingine kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ushuru wa bidhaa (Excise duty) na ada za usajili atatakiwa kulipa.

Zingatia: Mtumishi wa umma akinunua gari lenye umri wa miaka kumi au zaidi toka kutengenezwa hatapata msamaha kabisa.


6.0 Masharti ya kuzingatia kwa mtumishi wa umma. Ikumbukwe kuwa Serikali ina nia njema kwa watumishi wake kutoa upendeleo kwao kwa njia ya msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vyombo vya usafiri. Hivyo ni vema masharti yafuatayo yakazingatiwa: -
(a) Kibali cha msamaha kinachotolewa ni kwa ajili ya mtumishi wa umma anayehusika na sio mtu mwingine yoyote. Ni kosa kisheria kwa mtu yeyote asiye husika kufaidika na msamaha huu, na wala chombo cha usafiri chenye msamaha wa ushuru
hakiruhusiwi kutumika kwa shughuli za biashara.


(b) Msamaha utasitishwa na ushuru uliosamehewa utatakiwa kulipwa mara moja iwapo mtumishi wa umma ataacha kuwa mtumishi wa umma kabla ya miaka minne kupita tangu tarehe ya kupewa msamaha, au iwapo atahamisha umiliki au kuuza chombo hicho cha usafiri kwa mtu mwingine.


(c) Msamaha utatatolewa kwa chombo kimoja tu cha usafiri katika kipindi cha miaka minne. Baada ya muda huo kupita, mtumishi wa umma anaruhusiwa kuomba msamaha mwingine, lakini ni lazima ushuru ulipwe kwa chombo cha usafiri cha zamani kwa kiwango cha uthaminishaji kama ilivyoainishwa na Idara ya Forodha. Thamani itakayotumika
kukokotoa kodi husika ni thamani ya chombo hicho wakati kilipoingia nchini; mmiliki anapaswa kutunza nyaraka zote za chombo hicho cha usafiri vizuri.

Hivyo basi, ili mtumishi wa umma astahili kupewa msamaha mwingine baada ya miaka minne kupita ni lazima aambatanishe maombi yake na stakabadhi ya malipo ya ushuru kwa ajili ya chombo cha usafiri cha zamani toka TRA



7.0 Taratibu muhimu za kufuata Kujaza fomu ya maombi (Nakala nne) ambayo ni lazima iwe na viambatanisho vifuatavyo:-
(a) Magari yanayoagizwa toka nje ya Nchi
i. Barua ya utambulisho toka kwa mwajiri,
ii. Salary Slip ya mwezi wa karibu,
iii. Barua ya kuajiriwa kazini/Barua ya kupandishwa Cheo,
iv. Nakala ya kitambulisho cha kazi,
v. Anatakiwa pia kuambatanisha picha nne (4) za passport size ?kwenye fomu ya maombi,
vi. Kuambatanisha namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN),
vii. Kumbukumbu za ununuzi au uingizaji wa chombo husika cha usafiri hapa nchini.

http://tra.go.tz/publications/Msamaha wa ushuru kwa vyombo vya usafiri kwa watumishi wa umma.pdf
 
Wakuu kama kuna mtu yoyoyte ambaye ana uzoefu na freelander iliyofungwa injini 3s ya Rav 4, anijuze kama hiyo modification haisumbui perfomance ya gari

mm nakushauri usifanye hiyo kitu mkuu.ingawa wengi wanaifanya na wanashauriwa kuifanya ila hapo radha ya Gari na uhalisia WA Gari huwa unapotea kabisa .ukishafanya hivyo uimara wa Gari unapotea kabisa mkuu.

kama unauwezo lekebisha hiyo engine au nunua nyingine tuu.mambo ya kutembea na Gari iliyochomewa drive shaft.hakuna uhakika wa safari au imekatwa vikombe ni hatari tupu
 
Check engine mounting na ball joints, zikichoka hua pia zinaleta shida hiyo.

Engine mounting zikiwa na shida silencer huonekana iko juu maana engine ya gari inakuwa inauunguruma ikitetemesha bodi la gari.Boll joint kunakuwa na ka mlio fulani ka kuudhi gari inapotembea & stability ya miguu ya gari inapotea.
 
Wakuu kama kuna mtu yoyoyte ambaye ana uzoefu na freelander iliyofungwa injini 3s ya Rav 4, anijuze kama hiyo modification haisumbui perfomance ya gari

Modifications huwa sio nzuri maana hata mkao wa engine pia ni tabu.Hata kama fundi awe mtundu vipi modification haifikii u genuine wa gari ilivyokuwa.
 
Wakuu habar naomb mnisaidie Nina raum new model zile herufi ABS zinawaka je tatizo ni nini au ni kawaida
 
Okk nashkuru ni tatizo kubwa sana man naogopa isijekua hatarii

Hapana ni ngumu kusema ni kubwa au dogo mpaka umpate fundi mzuri wa kucheki lakini hata hivyo ni warning sign tu ya kukwambia kuna defect kwenye mfumo wa break
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…