Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

kama upo dar nicheki PM Cd zipo za kutosha sio za kuuza lkn ila ukija itakayo kubali kufungua redio yako tunaweza kukufanyia mpango wa copy yake
 
Msaada jaman
Nataka kuagiza Mazda atenza sport naomba ushauri
 
ISUZU BIG HORN gari ya kuleta umaskini mwaka wa 3 sijapata mteja maana nishachoka nalo linakunywa mafuta ka limetumwa
 
ISUZU BIG HORN gari ya kuleta umaskini mwaka wa 3 sijapata mteja maana nishachoka nalo linakunywa mafuta ka limetumwa
Hilo kalitafutie mteja mikoani ...hapa dar itafika mahali utapiga nalo picha
 
ISUZU BIG HORN gari ya kuleta umaskini mwaka wa 3 sijapata mteja maana nishachoka nalo linakunywa mafuta ka limetumwa
Gawia ndugu, sio kila gari lazima uuze ondoa dhana hiyo. Ukimpa mdg wako au mama kule bush watakuona wa maana mnoo
 
Gawia ndugu, sio kila gari lazima uuze ondoa dhana hiyo. Ukimpa mdg wako au mama kule bush watakuona wa maana mnoo
Ni kweli, asipokuwa makini mwisho "litamfia" mikononi mwake!
 
Wadau hebu nipen maoni yenu...kati ya passo cc1000 na duet cc1000 ipi ni kibaby walker bora zaidi?!
 
ISUZU BIG HORN gari ya kuleta umaskini mwaka wa 3 sijapata mteja maana nishachoka nalo linakunywa mafuta ka limetumwa
mkuu.hiyo big horn yako inatumia engine gani??
maana isije ikawa ni 4jx1 hiyo engine wengi hulaum kama ambavyo huwa wanazilaum engine za d4 kuwa ni mbovu.

hapo cha msingi tujaribu kuweka details zake juu ya engine yake na ulaji wake wa mafuta ndio tutoe hukumu isije ikawa tokea umeinunua mpaka now hujawahi fanyia service nozel zake harafu unalalamika na kulaum tuu.
harafu utwambie inakula mafuta lita 1 kwa kilomita ngapi??
sio unalalamika yawezekana hufanyi servirce unailalamikia gari tuu.
 
Naomben kujua kuhusu hawa Sijui n Mafundi utasikia John Car Sound Wana fanya kuunganisha miziki mikubwa kwenye Magari Hii hupelekea vip Gari Kupata Short ya umeme???? Naomba kujuzwa
 
Naomba Ushauri Nataka kununua Ki device cha kupimia Engine faults za magari. Diagnosis Tools.

Kwa ajili yangu na Kusaidia watu wa karibu. Je ipi ni Bora na naweza pata wapi kwa gharama gani?
 
Wadau..naomba maoni yenu ya kiusalama....nataka kusafiri usiku kuanzia saa tisa kuelekea moshi kupitia njia ya msata....! Naomba maoni yenu je ni salama kupita njia hyo kwa usiku wa saa tisa??!
 
Habari wadau,kwanza niwashukru kwa ushauri mzuri niliopata kutoka humu,nimeweza kubadirisha engine na gearbox ya freelander na kuweka 3S,sasa kunatatizo la kukatika cable ya gear selector wamenishauri nitafuta ndefu zaidi,mwenye nayo au uelewa wa tatizo hilo anisaidie,nawasilisha!
 
Usithubutu
Asante kiongozi....! Safar yangu nimeifanya jana....ingawa nilikuwa nahofia kuwa naweza kupimwa tezi dume maeneo yale...lakin nimekatiza mida ya saa nane kuelekea saa tisa usiku bila shida yyte. Hata hvo sishauri sana watu kuiga...bse...kwakweli unaweza kupimwa tezi dume bila hiari yako!
 
Na wewe pia usizoee kabisa hiyo maneno
 
Wadau kuna hii gari inaitwa Mitsubishi Airtrek naona iko kama Subaru Forester, vipi haisumbui kama Pajero iO? Nimeondokea kuvutiwa nayo. Kama kuna mtu ana ujuzi na uzoefu na hii gari atupe maujanja, je spea zipo Shaurimoyo?! Engine haisumbui? Vipi ulaji wa mafuta ni jini kama Subaru? Naipenda sana kama kuna mwenye data atusaidie kuzimwaga humu jamvini au ni PM!
 
Wadau..naomba maoni yenu ya kiusalama....nataka kusafiri usiku kuanzia saa tisa kuelekea moshi kupitia njia ya msata....! Naomba maoni yenu je ni salama kupita njia hyo kwa usiku wa saa tisa??!
Usijaribu hata siku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…