Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mkuu nimenunua body la Toyota Hilux SURF ilikuwa automatic, nataka nivalishe gearbox manual, nipe ushauri mkuu.
mkuu hapo hakuna tatizo.kama utaweza na utataka uenjoy usifanye mambo yakaonekana niyakunjunga na kuunga unga.

kama upo dar nitatoa mfano huu kwa kuwa mm nipo dar na ukitaka machimbo ya spea dar nayafaham mengi kidogo.ukinunua gearbox yako inakaa bila kufanya modification yoyote ile mkuu sababu gearbox ya automatic na manually sehem za kufungia zinaendana kwa magari mengi sana.

unaenda kwa watu wanao katakata masurf au kwa mtu mwenye body ya surf noze cut au kwenye mahilux unanunua spea na kuzifunga kwenye gari yako kama zilivyo hiongezi wala kupunguza.

ingekuwa ni gari tofauti hapo sawa kama toyota na nissan hapo ingekuwa shida kidogo.

ila kwa toyota kunjua roho mkuu maana toyota ni mnyonge wetu sana bango fundi ukishindwa kutengeneza gari ya toyota sijui utaweza kitengeneza gari gani bongo hiii
 
LEGE hapa tunapeana maarifa si kwamba nimesema haiwezekani bali nimesema kutokana na utaalam wetu hafifu ila kupitia reply yako nimegundua kuwa kuna mahali mtu anaweza kusaidika with guarantee
haina shida mshana jr kwa hayo magari ya toyota bongo mbona ndio vibonde wetu na ubaya au uzuri hiyo gari anayo isema ishakatwa sana screper so spea zipo za kutoshaa atashindwa yeye tuu
 
Shukran mkuu kwa ushauri
 
Msaada hiyo button iliyoandikwa SNOW ina kazi gani kwenye gari
 

Attachments

  • 1456034310784.jpg
    44.5 KB · Views: 60
Msaada hiyo button iliyoandikwa SNOW ina kazi gani kwenye gari
Kwa nchi zenye ukanda wa hali ya hewa ya joto kwa kipindi chote cha mwaka haina faida yoyote...hiyo ni kwa ajili ya zile nchi zenye vipindi vya baridi kali na barafu
 
Nashukuru mkuu, panapo majaaliwa nitakufuta huko dar.
 
Tairi ya gar ya mbele inaweza sababisha sterling kukutetemeka gar ikifika kuanzia 60km/hr? Aina ya gari ist
 
Naomba ushauri mwenye uzoefu we hii gari nataka kununua milion 8
Ni Mazda MPV. Namba DBS ...

 
Salaam wanajukwaa,, shida yangu kubwa ni kutaka Kujua ni kwa namna gani naweza kupandisha gari langu kwenda juu? Ni vitu gani naweza kununua? Kwa mfano gari kama Land rover discovery. Ili iwe na tyre pana na kubwa. Msaada
 
Salaam wanajukwaa,, shida yangu kubwa ni kutaka Kujua ni kwa namna gani naweza kupandisha gari langu kwenda juu? Ni vitu gani naweza kununua? Kwa mfano gari kama Land rover discovery. Ili iwe na tyre pana na kubwa. Msaada
Ushauri: iache kama ilivyo tayari discovery iko juu huhitaji kuipandisha zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…