Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Peleleka hiyo kwenye kituo cha mafuta wakuonyeshe eneo maalum la kufanyia service.kuna bolt ya kufungua ili oil imwagikie chini ndipo waweke mpya
 
Sawa mkuu,ila nilikuwa garage kwa mafundi.
Wengine wamesema hizi hazibadilishwi..
Du hata sijui inakuaje ila kwasababu gari inatembea ngoja niongeze milage.
 
Hakuna ambacho hakibadilishwi labda hao mafundi waseme hawajui au peleka kwenye garege maarufu
 
Waungwana naombeni ushauri wa haraka,
Nimekuja fanya service sasa nataka nibadili hydroulic ya gear box,
Stick haiyonekeni na koki yenyewe haipo.
Wala kibox cha sterling hydraulic hakipo.
Hii inakuaje?? Ya mwaka 2006
hiyo ni cvt transimission je gari yako ina km ngapi?
 
hiyo ni cvt transimission je gari yako ina km ngapi?

Hapana inasoma km 43260,ila si unajua hizi huwez jua kama walirudisha nyuma.
Ila nisaidie mkuu kama unayajua haya mambo.
 
Hapana inasoma km 43260,ila si unajua hizi huwez jua kama walirudisha nyuma.
Ila nisaidie mkuu kama unayajua haya mambo.
yap kama haina deep stick hiyo ni cvt transmission na inatumia oil maalum ya cvt usiweke transimission oil ya kawaida itaua hiyo gearbox ukipeleka garage utafahamishwa
 
yap kama haina deep stick hiyo ni cvt transmission na inatumia oil maalum ya cvt usiweke transimission oil ya kawaida itaua hiyo gearbox ukipeleka garage utafahamishwa

Ndugu yangu JohnQ, nimeenda garage leo.
Jamaa mmoja kaniambia nisiweke hydraulic za kawaida. Ipo hydroulic nyeupe ndio special kwa hizi gari.
Mwingine kasema haina haja kubadili kwasababu zinatakiwa ziende hadi km 100,000.
Lakini hapo kuna koki walishafungua na hakijamwagika kimimika chochote.
Lakini JohnQ,upande wa sterling nako vipi mana hakuna kibox cha kuweka pia.
Inatumia nini labda?
 
nahisi gari yako itakuwa inatumia electric power stering na sio hydraulic power stearing ukienda garage wakuchekie hata mwenyewe unaweza kuchunguza kwenye dashboard kama ukiweka on inawaka taa ya EPS ujue una Electric Power Stearing (inatumia umeme)
 
Ubarikiwe mkuu..
Asante kwa msaada wako.
 
Nina rav 4 yangu...nimefunga Sony dvd yenye screen ktk dashboard....nimeona ni GPS inbuild ila nikijaribu kucheki GPS navigation haifunguki...nawezaje kuifanya GPS navigation
 
Nina rav 4 yangu...nimefunga Sony dvd yenye screen ktk dashboard....nimeona ni GPS inbuild ila nikijaribu kucheki GPS navigation haifunguki...nawezaje kuifanya GPS navigation
Bado hatujawa na hii kitu hapa kwetu nafikiri kitu kinachoitwa Local GPS, ambayo unaconnect na radio , iliyopo kwasasa ni hii ya satellite tunayoipata kupitia mawimbi ya mawasiliano kwenye simu
 
Msaada Run X ya 2004 inatumia electric power steering, kuna wakati steering inakuwa ngumu kidogo, na wakati mwingine kawaida, je shida inaweza kuwa ni nin?
 
Haya ndugu zangu! Kwa wale wamiliki wa Nissan Tiida! Ninayo engine Mbichi Kabisa, imetumika bongo Miezi mi'4 gari ikaanguka! Pamoja Na vikololo vingine mpaka milango! Hiyo engine Ni Laki 6 tu.
 
Kaka mshana Jr. Lege na wengineo
Msaada hapa tatizo ni nini

Nina rav 4 old model ukiwa kwenye mwendo inatoa sauti ya kuvuma kutokea miguu ya nyuma

Ni kama berling zimeisha. Ila nilivyomwita fundi akazicheki hizo berling ziko poa wala hazivumi na mimi mwenyewe nilishuhudia.
Lakini ukiendesha hasa kwenye lami inatoa sauti ya kuvuma.
 
Umwshawahi kucheki diff oil au kuongeza hata maramoja? Hebu kacheki hilo kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…