Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

mkuu 0717228064 tutafutane yote yanawezekana kufunga control box nyingine au kukuchongea funguo nyingine yenye sensor wapatikana wapi hata kama upo mkoani utafuatwa tuu.tutafanyiana bei za ki JF zaidi
Asante niko mikoani ntakupigia
 
na mi naomba kuuliza kuhusu engine oil nna gari yangu toyota raum 2005 model ndo imefika toka japan ina engine ya 1NZ-Fe 1498cc nataka kubadili engine oil kwenye manual book wamerecommend 5W-30 ambayo nimetafuta dar nzima hakuna, mafundi wengi wameniambia niweke total au castrol 20W-50. Je hii oil inafaa kwenye hii engine?

Mkuu gari yangu pia inatumia hii oil 5W-30,na sio sahihi kwamba dsm nzima hakuna,na usijaribu hata kidogo kuweka oil tofauti na hii,hiyo gari imetengenezwa kwaajili ya kutumia oil nyepesi hivyo ukiweka oil nzito it ll be just a matter of time before your engine is dead.nenda kkoo tafuta duka moja linaitwa PACIFIC you will find what you need.
 
Jamani Kuna ishu hii ya kumwaga oil kila baada ya km 3000 sielewi kabisa. Nimepita kwenye website ya Toyota inaonyesha models zao nyingi unatakiwa kumwaga oil after 15000 km hii inakuwaje wadau.
 
Jamani Kuna ishu hii ya kumwaga oil kila baada ya km 3000 sielewi kabisa. Nimepita kwenye website ya Toyota inaonyesha models zao nyingi unatakiwa kumwaga oil after 15000 km hii inakuwaje wadau.

Mkuu angalia manual ya gari yako inasemaje?,sio kwamba Toyota zote zinabadilishwa oil baada ya muda sawa,hii ya kubadilisha oil kila baada ya km 3000 ilikuwa muhimu kwenye miaka ya 70 ambapo magari mengi yalitumia 10W-40 oil,ambayo ilikuwa inaisha kabisa inapofikia km 3000,.

Lakini sasa hivi chemistry ya oil imeimprove sana ubora wake umekuwa mkubwa na vilevile tighter tolerances katika assembling ya engines inaifanya hiyo km 3,000 isiendelee kutumika.

Sasa hivi kuna magari unashauriwa kubadilisha oil at 5000,7000,10,000 hadi 15,000 miles kwa model mpya za magari kwa mfano gari kama Toyota tacoma-pickup ya 2005 unashauriwa kubadili oil naada ya 5000miles,Honda wanashauri 7,500 miles for its 2002 Odyssey, General Motors wanashauri 7,500 miles for its 2007 Chevrolet Malibu,and Ford wanashauri 10,000 miles for its 2011 Fiesta.

Angalizo ni kuwa makini na aina ya oil unayoweka kama inaendana na hiyo engine na vile vile kufuata maelekezo ya manual ya gari inatakaje.kwa mfano ni lazma utumie oil inayomeet viscosity index ya 5W30 kama manual inakutaka hivyo,maana hii inamaanisha kuwa kuwa oil pressure regulator na sensor ambavyo viko sensitive sana kwa aina ya oil tofauti na hiyo will shut it down when you use the wrong oil.
 
Lege,mshana naomba kukumbushwa sensor ambayo ikianza kufa gari huzima ukiwa umesimama huku gari ikiwa kwenye gia. Ila ukiweka parking au neutral haizimi.
 
Wakuu lege,mshana jr na wengine,heshima kwenu,naomba kujua kidogo kuhusu hii gari inaitwa mazda demio,uimara,mafuta,upatkanaji wa spare,plz nataka kuchukua,Thanks in advance.
 
Wakuu lege,mshana jr na wengine,heshima kwenu,naomba kujua kidogo kuhusu hii gari inaitwa mazda demio,uimara,mafuta,upatkanaji wa spare,plz nataka kuchukua,Thanks in advance.
Mmh ni vgari vipya vinafaa kwa matumizi mepesi spare bado hazijawa nyingi ila zipo fuel consumption vinanusa, uimara ni tofauti na GX 100 yani havimfikii huyo mnyama
 
Hii ni nzuri kwa msaada. Ndugu zangu natumia kagari kangu PASSO ila naona kameanza mchezo wa kustuka yaani mfano nimepaki nakawasha naingiza gia yoyote iwe R au D inaganda kwanza alafu inastuka ndio ianze kwenda, msaada wenu tatizo laweza kuwa ni nini?
 
Kuna shida kwenye gearbox hydraulic haipandi haraka na kuingia kwenye system ya gear
Nasubiri jibu
 
Naombeni ushauri wakuu. Nataka kununua moja wapo kati ya gari hizi: NISSAN X-TRAIL, FORD ESCAPE, MAZDA TRIBUTE, SUBARU FORESTER au HONDA CRV. Ni kwa ajili ya shughuli zangu nyingi za nje ya mji ambapo barabara siyo lami hivyo nahitaji gari iliyonyanyuka juu. Mwenye uzoefu na gari hizo tafadhali naomba ushauri
 
Kwa ushauri wangu binafsi chukua Honda CRV Rd 4 au 5
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Mshana Jr binafsi sijawahi kumiliki gari ila imefika wakati nahitaji kununua kwa ajili ya matumizi ya familia hapa mjini na Mara moja moja kwenda likizo kutoka mbeya kwenda kahama naomba ushauri kati ya gari hizi IPI itanifaaa Ist cc 1299,Toyota belta cc 1290,Toyota premio cc 1490,corolla axio cc 1490 na Toyota raum,ipi itanifaa zaidi ?
 
Back
Top Bottom