Jamani Kuna ishu hii ya kumwaga oil kila baada ya km 3000 sielewi kabisa. Nimepita kwenye website ya Toyota inaonyesha models zao nyingi unatakiwa kumwaga oil after 15000 km hii inakuwaje wadau.
Mkuu angalia manual ya gari yako inasemaje?,sio kwamba Toyota zote zinabadilishwa oil baada ya muda sawa,hii ya kubadilisha oil kila baada ya km 3000 ilikuwa muhimu kwenye miaka ya 70 ambapo magari mengi yalitumia 10W-40 oil,ambayo ilikuwa inaisha kabisa inapofikia km 3000,.
Lakini sasa hivi chemistry ya oil imeimprove sana ubora wake umekuwa mkubwa na vilevile tighter tolerances katika assembling ya engines inaifanya hiyo km 3,000 isiendelee kutumika.
Sasa hivi kuna magari unashauriwa kubadilisha oil at 5000,7000,10,000 hadi 15,000 miles kwa model mpya za magari kwa mfano gari kama Toyota tacoma-pickup ya 2005 unashauriwa kubadili oil naada ya 5000miles,Honda wanashauri 7,500 miles for its 2002 Odyssey, General Motors wanashauri 7,500 miles for its 2007 Chevrolet Malibu,and Ford wanashauri 10,000 miles for its 2011 Fiesta.
Angalizo ni kuwa makini na aina ya oil unayoweka kama inaendana na hiyo engine na vile vile kufuata maelekezo ya manual ya gari inatakaje.kwa mfano ni lazma utumie oil inayomeet viscosity index ya 5W30 kama manual inakutaka hivyo,maana hii inamaanisha kuwa kuwa oil pressure regulator na sensor ambavyo viko sensitive sana kwa aina ya oil tofauti na hiyo will shut it down when you use the wrong oil.