Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Wakuuu hii alama hapa inamaanisha nin na ikiwepo hapo tatizo ni nin maana leo siku nzima ijazima inawaka tu
 
Wakuuu hii alama hapa inamaanisha nin na ikiwepo hapo tatizo ni nin maana leo siku nzima ijazima inawaka tu
View attachment 404388

Peleka kwa fundi anayeweza kutumia mashine ya kufanya diognosis ili acheki ktk injini kuna ttzo gani. Unajua magari mengi ya sasa yana sensor nyingi sana, naamini itakuwa suala la sensor tu hilo. Ukipata ufumbuzi wa hilo tatzo njoo utoe mrejesho ilikuwa ni nini.
 
Wadau napenda kujua nini kazi ya thermostat kwenye gari na je ikitolewa ina madhara gn?

Hiyo najua ina control maji au coolant kutoka kwenye engine na kurudi kwenye rejeta. Maji yakichemka saana kwenye engine thermostat inafungua valve, yanatoka yanaenda kupozwa kwenye rejeta
 
Kuna kifaa kinaitwa Digital Music Changer, unakiunganisha kwenye radio ya gari, then kinakupa uwezo wa kutumia flash disc na aux port kwa kuwa operated na radio yako kama vile umeweka cd.
 
kwanini gari nyingi zenye piston tatu zina ugonjwa wa kutetemeka ukiwasha hasa kwenye steling&[HASHTAG]#65311[/HASHTAG];.mfano passo.piston tatu na nyingine&[HASHTAG]#65311[/HASHTAG];

Engine za piston/cylinder chache huwa zinatetemeka kwa sababu kunapokua na idadi chache ya cylinder, crank shaft inacheza cheza saana. Na kunakua hakuana kitu wanaita counter weight ili kupunguza vibration. Hata ukilinganisha four cylinder na six cylinder utaona tofauti. Hasa ukipata ile six cylinder wanaita inline 6, ambayo cylinder zimejipanga kwenye mstari mnyoofu. Huwa inatulia saana, unaweza weka glass ya maji iliyojaa na yasimwagike hata kidogo. Ila ukiweka kwenye v6, au engine ya cylinder chache utaona mtetemeko.

Subaru walianzisha engine zinaiter boxer. Hizo cylinder zake zimekaa kwenye 180 degrees, so zinapunguza saana mtetemeko
 
Engine za piston/cylinder chache huwa zinatetemeka kwa sababu kunapokua na idadi chache ya cylinder, crank shaft inacheza cheza saana. Na kunakua hakuana kitu wanaita counter weight ili kupunguza vibration.

Solution ni nini mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…