Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Wakuu taa ya ABS ikiwaka au ikiwa inawaka na kuzima nini maana yake.
Kwa lugha nyepesi iliyonyooka tafadhali msaada
 
Wakuu msaada kidogo,
Wapi nitapata wataalam wa kubana mafuta kwenye rav4 old model!?
Kwani now ulaji wake wa mafuta ukoje mkuu?? Lita moja inakwenda kilomita ngapi??

ukijibu swali hilo basi nitakwambia kama unachokitaka kinawezekana au laaa.
 
Wakuu ivi gar kama inakausha maji kila iktembea umbali flan tatzo linakuwa ni nn?!!
 
Wakuu taa ya ABS ikiwaka au ikiwa inawaka na kuzima nini maana yake.
Kwa lugha nyepesi iliyonyooka tafadhali msaada[/ kama ulichange pads shida kuanzia huko, yangu nilichailiweka hz za elf 25 taa ya abs vsc nac zote iwakamaa alinawezaecnilichangeinaonyesabsuu wa kushoto shida, nimvscescziliwakaalicegoognimegoonikapata ushaur niweke pads za zaman nikatoa terminal zikazima moja kwa moja. SULUHISHO NIKAWEKA ZA BEI KUBWA
 
Wakuu taa ya ABS ikiwaka au ikiwa inawaka na kuzima nini maana yake.
Kwa lugha nyepesi iliyonyooka tafadhali msaada
Nijuavyo mimi ni kuwa either sensor ni mbovu au ulibadilisha kitu kwenye miguu ambapo ring uliyoweka haigusi na hivyo kufua usumaku ambao sensor itaihisi. Kwa lugha nyingine kagua switch za ABS kama zimekufa na au kagua miguu kama sensor inagusa vizuri, na hii hutokea kwa baadhi ya magari spare zake za dukani zinapungua vipimo kidogo, so mafundi hung'oa hizo ring zenye meno na kuziweka kwenye mpya ya dukani ili sensor iweze kugusa kwa mbali na kufua usumaku, na hivyo kufanya kazi
 
Kwani now ulaji wake wa mafuta ukoje mkuu?? Lita moja inakwenda kilomita ngapi??

ukijibu swali hilo basi nitakwambia kama unachokitaka kinawezekana au laaa.
Sasa hivi inaenda km 8 mpaka 9 mkuu.
 
Gari langu ni Suzuki Swift. Kwa sasa sipati gia namba 1 na gia namba 5. Hii gari ni automatic naomba ushauri tafadhali
 
Kama ni model chini ya 2010, usiwe na shida na gia namba 5 kwa sababu automatic zote ni 4 speed ie zina gia 4. Kuhusu hiyo gia namba 1, mafundi watakuja soon.
 
Asante Mr. Rugambwa. Labda nilikosea katika maelezo. Gia ambayo sipati ni top gear au overdrive. Naomba isomeke hivyo
 
Okay, kutokana na experience yangu na research kidogo, inawezekana Transmission fluid haijabadilishwa muda mrefu, au ulibadilisha hiyo fluid lakini haukurudishia ambayo imekua recommended kwa hiyo gari. Afrika tunapata shida saana kwenye hayo mambo maana sometimes ni vigumu kupata transmission fluid iliyokuwa recommended na manufacturer wa gari. Wakati mwingine inakua very expensive. Mfano transmission fluid inayokua recommended na toyota unawezakuta lita moja ni zaidi ya sh 45,000.

Pia kama sio shida ya transmission fluid, basi transmission control module ina shida. Hii ni kama ECU ya gear box. Ndio inaiambia auto gear box ni muda gani wa kubadilisha gia. Huwa haziharibiki kirahisi, lakini ikiharibika au ikiwa na shida inaweza sababisha matatizo kama yako.
 
Gari langu ni Suzuki Swift. Kwa sasa sipati gia namba 1 na gia namba 5. Hii gari ni automatic naomba ushauri tafadhali
Kama gia namba 1 hupati basi hata namba 5 huwezi kuipata pia.inawezekana kuna valve moja inaweza ikawa majanga mbovu
 
Nashukuru kwa maelezo yenu. Nimemleta fundi toka Ilala na akabadilisha clutch set moja na sasa gari linafanya kazi vzuri na gia zote zinapatikana
 
Nina gari aina ya toyota Belta ikifika speed kuanzia 90 km/hr mlio unabadilika unakuwa kama wa subaru au hizi sports car. Nimeangalia line ya exhaust kama imeachia lakini sioni tatizo. Sijui shida inaweza kuwa nini nisije nikapeleka kwa mafundi wakasababisha tatizo lingine. Msaada jamani ni nini fundi au mimi natakiwa niangalia au nifanya
 
Ninafikiri inawezekana sio tatizo. Ni Toyota's vvti inakua kwenye kazi yake. Maana ukizidi 90, kwa engine ya Belta, unakua kwenye rpm 3,500 na zaidi so ECU inatumiwa msg kuwa unahitaji performance zaidi kuliko economy. So, with vvti, valves zinaanza kuingiza hewa kwa wingi zaidi, na hewa nyingi inatolewa kwenye exhaust system pia. Hivyo mlio lazima ubadilike.
 
Kiongozi mwaka jana hilo tatizo halikuwepo. Nilikuwa naenda mpaka 140 km/hr.
 
Back
Top Bottom