Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Hapana tumia recommend oil kama ingekuwa ni kuhusu hilo wangetoa na alternative
 
Habari wadau.
Naombeni ushauri wa haya kwa wenye uelewa natumia rav 4 1997 model

1. power steering fluid inavuja nikijaza safari moja tuu yameisha

2. mlango wa nyuma kwenye boot uligongwa nikanyoosha lakini naona una kelele ninapotembea rough road. mpya nitapata kwa bei gani?

3. kubadili stuts/ shockups zote mbele na nyuma inaweza kula sh ngapi?

4. tairi bora kwa hii gari ni ipi na inaweza kiwa sh ngapi? kwa zote nne.

5.bima imeisha nilikiwa natumia NIC kama kuna kampuni ingine bora naombeni mniambie.

Naombeni ushauri kwa wanaofahamu
Ahsante.
 
Hapa naomba niwaalike hawa wadau
CC : RRONDO, LEGE etc
 
1.inawezekana kuna seal zimechoka kwenye power steering pump yenyewe au kwenye steering rack
2.jitahidi kuepuka kunyoosha gari, huwa hairudi 100%, nunua mlango used, take your time nenda ilala utapata.
3.haizidi 500 genuine, za kichina haizidi 350,000. again take your time tembelea maduka ya spare kariakoo.
4.inategemea mfuko wako ila pirelli,hankook,yokohama,bridgestone ndio tairi bora.
5.zipo nyingi jaribu jubilee,britam,insurance group etc
 
ahsante mkuu kwa ushauri
 
Mwanzo kabla sijavuta hii kitunilikua nasikiliza sana story za kijiweni tokea nivute hiko chombo cjutii pesa niliyotumia. Kuna siku nilikua naenda Moro yani uko njiani zile V8 zilikua zinanisoma tu plate number aiseee, nilipofika msavu nikawa nimepaki sehemu wale jamaa ilibidi wachungulie dirishani kuona ni nani dereva na mtu wa status ipi maana yule waliyekua wanampeleka alikua na plate namba ya waziri
 
Ushauri je wa kuhusu hizo seal kwenye power steering? Maana na mie gari langu linaugonjwa huo huo, umeanza kama wiki 2 zilizopita
 
Ushauri je wa kuhusu hizo seal kwenye power steering? Maana na mie gari langu linaugonjwa huo huo, umeanza kama wiki 2 zilizopita
Solution ni kubadili seals kama zinapatikana. Zisipopatikana huna budi kununua power steering pump au steering rack.
 
Msaada jamani...,gari langu ni automatic nimezima baada ya kupaki lakin nikwasha kwa sasa haliwaki ila taa za kwenye dashboard zinawaka na betri ni jipya kabisa. Tatizo huenda likawa ni lipi
 
Msaada..gari langu ni automatic limezima ghafla Ila taa za dashboard zinawaka ingawaje engine can't start na betri ni jipya kabisa
 
Msaada jamani...,gari langu ni automatic nimezima baada ya kupaki lakin nikwasha kwa sasa haliwaki ila taa za kwenye dashboard zinawaka na betri ni jipya kabisa. Tatizo huenda likawa ni lipi
Embu cheki huenda ulizima ikiwa kwenye D badala ya P arking P....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…