Wakubwa heshima kwenu
Napenda kutoa mrejesho wa changamoto ya gari RAV4 Kama nilivyowasilisha hapa, napenda kushukuru kuwa tatizo limetatuliwa, namshukuru Sana ndg yetu
LEGE ambaye alijitolea na kufix Tatizo hilo, kilichoonekana Kama Tatizo ni mfumo wa mafuta, fuel pump na chujio lake, na nozel vilikuwa vimejaa uchavu, vumbi na takataka kibao, hivyo Mafundi walifungua tank, fuel pump, chujio na nozel na kusafishwa ipasavyo, Kwa sasa napenda kusema kuwa gari ipo vzr kabisa inapiga na kuongeza Mwendo bila kusita na bila wasiwasi wowote.
Nachukua fursa Hii kutoa shukrani za dhati Kwa ndg
LEGE na wadau wote wa hii thread , mchango wenu umefanikisha kutatua changamoto iliyokuwa inasumbua.
Asanteni