Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Ninaomba ushauri kuhusianana gari aina ya toyota WISH mwenye uzoefu aje anipe experiences
 

Mkuu niuzie hii gari kama bado unayo. Nahitaji sana
 
Ni kawaida Vitz Clavia Full fuel tank 42ltrs ila napenda kuchanganua Reserve Tank 7litrs kwa hyo ukiona bar ina blink ujue unaanza kula Reserve Tank km unataka uamini ikianza kublink kaweke Full tank fuel utaona mafuta utakayopimiwa yatakuwa 37Ltrs kwa hapo utakuwa umenielewa
 
Wakuu poleni na majukumu nina mark x yangu yenye engine ya 4GR kuna wakati inakuwa na mis na wakati mwingine ukiendesha ina shitua kama vile inachanganya then inapunguza kasi lakini pia wakati huo ikiwa inaishiwa nguvu ukikanyaga accelerator mshale wa RPM unafika sehemu hauendelei na unashuka wenyewe huku ukiwa bado umekanyaga.
Naomba msaada nini shida.
 
Mimi kwa uzoefu wangu altezza nyingi 4 cylinder zinasumbua sana engine lakini ukipata 6 cylinders iko poa na kuhusu mafuta sio kweli kama inakula sana
 
Most likely coil zimeshachoka za kubadili
 
Hello wakuu...nina mambo mawili naomba niulize.
1. Hivi unaponunua shockups za gari...unatakiwa upewe na coil springs au zile zinanunuliwa tofauti?
2. Engine oil best kwa Carina Si ni ipi...huwa natumia SAE 40...je ni sawa???
 
Hello wakuu...nina mambo mawili naomba niulize.
1. Hivi unaponunua shockups za gari...unatakiwa upewe na coil springs au zile zinanunuliwa tofauti?
2. Engine oil best kwa Carina Si ni ipi...huwa natumia SAE 40...je ni sawa???
Kubadili springs ni optional... Mara nyingi tunachobadili ni shock ups... Engine oil hiyo ni sahihi Ila pata genuine
 
Nimekupata, aksante sana kaka Mshana Jr...changamoto ipo hapo kwenye kuipata ambayo ni genuine...naijuaje???
Hivi kaka Mshana...bima ya gari ikishaexpire...ukirenew nilazima utumia kampuni hilo la awali au naweza lipa kwa kampuni lingine ninalopenda???
 
Oil kwa Carina yako sio sahihi oil sahihi ni 5w30 au 10w30 hasa kwa hapa nchini unashauriwa utumie mojawapo kati ha hizo
 
Aisee hizo oil huku nilipo hazipatikani kabisa...ipo ile 20w50...wapi naweza pata hapa nchini???
Kwa Tanzania hii nadhani hakuna sehemu ambapo hakuna magari yanayofika kutokea hapa dar es salaam nadhani ukiitaji utapata hata kwa kutumiwa
Kwa ushauri kuhusu oil na vilainishi +255719263074
 
Bei ndio inatofautisha.. Bima unaweza kubadili kampuni bila shaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…