Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Naomba mnijuze hivi kuna utofauti hasa fuel consumption kati ya engine ambayo ni D4 VVTi na VVTi isiyo D4 ikiwa zote ni 2362cc kwenye similar platform? Shukrani.


Mkuu apo kwenye ya vvti always kwenye fuel consumption iko vizuri ukilinganisha na iyo d4 isiyo vvti sababu kubwa moja wapo ni vvti engine inatumia umeme mwingi wakati huo huo ikishilikiana na hewa kwaio kwa pamoja vinapunguza ulaji wa mafuta uki-compare na zile engine ambazo si vvti eg 1G,1kz, etc
 
Uhusiano wa breaks na ac ni nini?
Gari hii inakuwa shida breaks kama ac ziko on. Nikizima zinakaa vizuri
 
Hii gari leo imenipa mtihani sana

Jamani hizi gari za kisikuizi tuwe makini. Nimetoa terminals za battery tu imeleta kizaa zaa balaa baada ya kurudisha. Ni kama computer flan kwa sababu imefuta memory zote kuanzia ac, radio, doors, side mirrors, silence na ukiwasha tu inawaka but ukiweka gear inazima.

Pls kama una gari hizi za kuanzia 2006 na kuja juu muwe makini jamani hasa kwenye terminals za battery hapa ndio fundi anafanya data recovery at least some parts are now active
 

Mmh ni gari gani hiyo kaka!?
 
mshana jr nna Toyota GDI pajero ina misi mpk nataman kuichoma moto hivi hizi gari shida ni nino
 
Last edited by a moderator:

Pole kaka, hata mimi lilinijuta hilo tatizo kwenye forester, ni kweli kuwa computer ya gari imepoteza memory, unachotakiwa kufanya ni kupeleka kwa mafundi wanaofomart gari kwa computer itakuwa poa
 
Hilo mkuu

Hii ni Mitsubishi pajero GDI, Sio Toyota kaka! Hiyo miss yawezekana ni plugs, sensors za breezer, aircleaner au gari ilipitishwa kwenye maji aidha wakati wa kuoshwa au kwenye dimbwi. Hapa inabidi apatikane fundi mjuzi acheki kwa hakika tatizo ninini kabla ya kukimbilia kununua vipuri
 
Pole kaka, hata mimi lilinijuta hilo tatizo kwenye forester, ni kweli kuwa computer ya gari imepoteza memory, unachotakiwa kufanya ni kupeleka kwa mafundi wanaofomart gari kwa computer itakuwa poa

Nimeshaflash ingawa bado sio 100/100 kama ilivyokua awali but at least nimedrive back home
 
Habari wanajamvi, nina toyota vitz vvti inakula mafuta vizuri sana, yaani average ni 17 to 20km per litre. Nimemwagizia wife same capacity na milleage ulaji unaenda hadi max 16 km per litre, yenyewe haina vvti.
Mwenye kufahamu hili vvti ni mdudu gani? Very interesting
 

Ni kirefu cha Variable Valve Timing with intelligence ni mfumo wa kusukuma injini ambapo umeme na upepo hutumika zaidi kuliko mafuta

Kwamba 'kiitelejensia mfumo huamua ni muda gani upepo utumike au umeme utumike vikisindikizwa na kiasi kidogo cha mafuta

Mara nyingi gari za VVT-i kwenye dashboard huwa na taa ya ECO/economy yaani spidi 0- 80.ukivuka hiyo spidi taa ya ECO huzima kwa maana hiyo mafuta zaidi huanza kutumika

Vilevile kuna VVT-iE, angalia picha
Wakati mfumo wa VVT-i huwekwa kwenye plugs, mfumo wa VVT-iE huwekwa kwenye shaft ya injini, VVT-iE ni HY-BRID ya VVT-i

Zaidi ya hizo siku hizi kuna mfumo mpya wa engine-baterry-mortar hii ndio mwisho wa matatizo kwakuwa Lita moja ni km 30+, mfumo wake uko hivi Engine-mafuta, engine-umeme/battery na engine mortar, na huo mfumo ni auto, huamua wenyewe ni wakati gani na kwa spidi gani utumie nini
 
Wandugu Habari zenu nahitaji kununua next month, nahitaji ushauri kwa gari hizo nne, gari ipi safi kwa mazingira Ya Tanzania.comfortable barabarani, less fuel consumption,Upatikanaji wa vifaa.jf najua kuna wataalamu wa kila kitu.
Asanteni sana.
 
Mkuu mshana jr bado cjapata suluhisho la ile changamoto yangu ya RAUM new model kutumia kiwango kikubwa cha mafuta kupitiliza.

Hii gari ina VVTi engine, na sijawahi kuifanyia modification yoyote ile.

Kwako sasa fuel consumption yake ni 8km kwa lita, kuna kila dalili za kunifilisi hii gari.
 
Last edited by a moderator:

Duuu aisee kama ni hivyo kweli shida ni kubwa ngoja nirudi Dar wikiendi hii au ukiweza ipeleke pale Toyota kwa diagnosis au popote pale wanapotoa hiyo huduma
 
Last edited by a moderator:
vipi wakuu nina driving license ila for the rest of the year nitakua uganda masomoni je naweza kuitumia driving license yangu hiyo ya tanzania kudrive nikiwa kule? na kama ni impossible what should i do?
 
vipi wakuu nina driving license ila for the rest of the year nitakua uganda masomoni je naweza kuitumia driving license yangu hiyo ya tanzania kudrive nikiwa kule? na kama ni impossible what should i do?

Haitawekana kuitumia huko kwakuwa hatujawa na sera ya pomoja kuhusu hilo sana sana utaenda nayo huko ukawaonyeshe kisha wakupatie ya kwao AU omba leseni ya kimataifa hapahapa nchini
 
Duuu aisee kama ni hivyo kweli shida ni kubwa ngoja nirudi Dar wikiendi hii au ukiweza ipeleke pale Toyota kwa diagnosis au popote pale wanapotoa hiyo huduma

Shukrani sana, labda nitafute sehemu nyingine lkn wale jamaa TOYOTA wanacharge hizi gari za serikali hapa ofisini, nawaogopa kwa bei zao!

Ngoja nijaribu VETA CHANG'OMBE, najua wana diagnosis nzuri

Shukrani sana mkuu mshana jr
 
Last edited by a moderator:

Asante mkuu, hii itakuwa kigezo cha kuagizia gari.
By the way ni mfano wa gari ipi used yaweza kwenda hadi 30km/litre? Aisee hii ndo ya kununua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…