Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Jamani taratibu na baadhi ya ushauri mtauwa watu bure na presha,wengine ndo kwanza gari zipo baharini zinakuja mnataka wafe sasa
 
Heshima kwenu wana jf
Naomba ushauri, mwezi may nataka kuagiza gari aina ya Toyota cami ama Daihatsu Terios,hivyo kabla ya kuagiza naomba wadau wenye kujua ubora au.udhaifu wa gari hiz. Na ipi ni bora kati ya aina hizo za magari kwan zinafanana sana kwa muonekano.
Msaada plz
 
Spare utapata mtaa wa jangwani kuna duka la subaru au karibu na dtb kwa nyange sema ana bei
 
Fundi mzuri wa subaru yupo ubungo external karibu na njia panda ya bakwata uuliza fundi wa subaru yupo poa anazijua gari na bei yake nzuri
 

Fuatilia nyuzi za nyuma naona Daihatsu ndio imesifiwa zaidi
 
Kuna hasara gani gari ukiipandisha kuondoa kama kiko chini sana
 
Jamani taratibu na baadhi ya ushauri mtauwa watu bure na presha,wengine ndo kwanza gari zipo baharini zinakuja mnataka wafe sasa

Umeagiza gari gani? Usitishike sana labda iwe ishu ya wese tu lakini hapa utakuwa umepata mengi kiasi kwamba hata gari yako itakapofika utakuwa na knowhow kwenye mengi
Kikubwa ni utunzaji
 
ABS inatakiwa iwe on muda wote au inakuaje, si pale kwa juu ya dash huwa kuna sign ya ABS
 
Kuna hasara gani gari ukiipandisha kuondoa kama kiko chini sana

Utapoteza centre of gravity kwa hiyo gari itakuwa haitulii barabarani kwenye mwendo mkali. Jaribu kunyanyua kwa kutumia tairi saizi kubwa imgawaje haitanyanyuka sana.
 


Soma page tatu au nne nyuma ila kwa kifupi hazina tofauti
 
Habari zenu wakuu.

Natumai mu-wazima kabisa wadau kama MADA inavyojieleza wakuu naomba msaada wa kujua ushuru wa hii gari kuitoa bandarini..................ipo njiani, tarehe 22 Apr inataraji kufika bandarini ningependa kujua mapema gharama ili nijue kipi cha kufanya wakuu,natanguliza shukran.


SPECS :

Make : Nissan X-trail

Engine Size :1,990cc

Registration
Year/month :
2002/3

Manufacture
Year/month :
2002/3

Price : U.S $ 3600







For more details visit here :

Nissan X-trail.Beforward


THANK YOU.
 
Ushuru andaa ml 6.5-7 bandarini laki 3 shipping line $ 85 wakala maelewano lakini si chini ya laki 2.
Mkuu labda ungeweka gharama zote ikiwa ni pamoja na road licence, insurance, registration ili ajue kbs total cost na ajiandae. Nimesema hvy coz unaonekana so exprienced kwenye hili itatusaidia na wengine hasa ukizingatia JF ni jungu kuu.

Asante.
 
Mkuu labda ungeweka gharama zote ikiwa ni pamoja na road licence, insurance, registration ili ajue kbs total cost na ajiandae. Nimesema hvy coz unaonekana so exprienced kwenye hili itatusaidia na wengine hasa ukizingatia JF ni jungu kuu.

Asante.

Yes ni kweli kabisa kiongozi RAI yako imekaa vyema sana mkuu ingekuwa vyema kama mdau angeweza kudadavua ili kujua tunajipanga vipi mkuu.

Wakala amesema yatupasa kumpa laki 3 sasa sijajua port charges na tax ya gari husika na pia italazimu kuilipia excise fees (kodi ya uchakavu).

Sasa si vibaya kama ukatupa mwanga ili kuweza kuweza kujua inatugharimu kiasi gani mpaka inaingia barabarani mkuu.

MANI
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana mkuu cha msingi andaa pesa kama uliyonunulia hiyo gari, usipokuwa makini unaweza kuiuzia bandarini maana ushuru utadhani maji ya bahari ya hindi serikali yako sikivu huwa inayalipia ushuru!!
 

Attachments

  • 1428608470435.jpg
    31 KB · Views: 1,131
Ingia tovuti ta tra.go.tz kuna calculator itakayo kusaidia kupata hesabu sahihi ya kodi itakayo kuhusu.Gharama zingine hazita fikia milioni moja baada ya kodi.
Calculator yenyewe ni rahisi kuitumia
 
.....calculator inahusika hapa qasikuogopeshe....ni kama 5.5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…