Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Wakuu nawashkuru sana sana kwa michango yenu wandugu.

Nilitingwa sana leo sikupata nafasi ya kuingia hapa nilipata msiba na nashkuru kuwa tumezika salama.

Pole kiongozi...Mungu awatie nguvu...
 
Hapo ndipo TRA wanawachanganya waagizaji na huenda ikapelekea kutoeleawana katika pande husika.
Mfano angalia hapo kwenye calculator ya TRA inasema US $3,114 wakati invoice ya muagizaji inasema uS $3,600.
Hapa ni wazi ushuru wa hii gari hauwezi kuwa 5.5m.
Labda vinginevyo aje mtu hapa anayeelewa hili eneo atupe ufafanuzi kiundani zaidi.
cc: KIOO, [URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=20033"]mayoscissors, [URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=20103"]Preta[/URL][/URL]


Mkuu ni kweli CIF ikiwa juu kuliko CUSTOM VALUE hata kodi pia huwa inaongezeka pia lakini si sana kama unavyoona hapo kuwa kuna tofauti kidogo mkuu kwa hivyo hata tax yake sidhani kama itaongezeka sana kupita ukilinganisha na CV na CIF kiongozi.

Labada atusaidie hapo mkuu ilonga au lucky sabasaba kwenye hilo suala.
 
Last edited by a moderator:
mkuu hiyo hapo;

Reference Number1415412147
Make:NISSAN
Model:X-TRAIL
Body Type:SUV
Year of Manufacture:2002
Fuel Type:PETROL
Engine Capacity:1001 - 2000 CC
Customs Value CIF (USD):3114.00
Import Duty (USD):778.50
Excise Duty (USD):194.63
Excise Duty due to Age (USD):1167.75
VAT (USD):945.88
Total Taxes (USD):3087
Total Taxes (TSHS):5541165

Barikiwa sana kiongozi nashkuru mno kwa mchango wako mkuu.
 
Pole kiongozi...Mungu awatie nguvu...

Amin......Amin......Amin mkuu nashkuru sana kiongozi na pia nashkuru sana kwa mchango wako wa hali ya juu MUNGU akubariki sana mkuu, THANKS AGAIN & AGAIN.
 
Amani iwe nanyi!Naomba kuuliza.
Gari ikishatoka bandarini unaweza ukaanza kutembea nayo au ni lazima uifanyie service kwanza.
 
Mkuu umemwelewa Samora10?

Kumuelewa kwangu ni kama ananitahadharisha kuhusu running costs na hasa spare kwa ujumla juu ya gari husika and thats why akanitakia kila la heri mkuu.

Au labda si hivyo mkuu ...?.
 
Last edited by a moderator:
Habari zenu wakuu.

Natumai mu-wazima kabisa wadau kama MADA inavyojieleza wakuu naomba msaada wa kujua ushuru wa hii gari kuitoa bandarini..................ipo njiani, tarehe 22 Apr inataraji kufika bandarini ningependa kujua mapema gharama ili nijue kipi cha kufanya wakuu,natanguliza shukran.


SPECS :

Make : Nissan X-trail

Engine Size :1,990cc

Registration
Year/month :
2002/3

Manufacture
Year/month :
2002/3

Price : U.S $ 3600

BF369773_1aea8d.jpg


BF369773_13e0d2.jpg


BF369773_a6e0ca.jpg


For more details visit here :

Nissan X-trail.Beforward


THANK YOU.

Total si chini ya Tshs. 18 Milioni mkuu
 
Amani iwe nanyi!Naomba kuuliza.
Gari ikishatoka bandarini unaweza ukaanza kutembea nayo au ni lazima uifanyie service kwanza.

Inakuwa na karatasi ya service, soma next service ni km ngapi, angalia kwenye dashboard kuna kilometa ngapi, Fanya uamuzi
 
Back
Top Bottom