Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Huwa nawashauri wateja wangu wanaonunua magari, pamoja na mambo mengine ni salama kwa iwapo watajiridhisha kwamba wanaowazia magari ni wamiliki halali. "Buyer beware" kanuni hii inahusu sana.
 
Mkuu mapigo yangu ya moyo yanaenda sawasawa kiongozi mbona unataka kuyaongeza kiongozi...?.

Hiyo ni jumla kuu from your CIF mpaka unaitoa hapo bandarini...! Total pamoja na CIF na Kodi zote si chini ya TSHS. 18 Milioni
 
Hiyo ni jumla kuu from your CIF mpaka unaitoa hapo bandarini...! Total pamoja na CIF na Kodi zote si chini ya TSHS. 18 Milioni

Mkuu mbona watu wote waliotoa michango hapa hawajafika hiyo amount kiongozi it means wamekosea ku-calculate au...?.
 
nashukuru sana mkuu,umenitoa tongotongo vya kutosha!
 
Mkuu mbona watu wote waliotoa michango hapa hawajafika hiyo amount kiongozi it means wamekosea ku-calculate au...?.

Mkuu kuwa makini na kukatishwa tamaa...kuna watu wengine uzoefu wao ni wa mwaka 47...kwa calculator ya tra hiyo gari haifiki huko...kwa uzoefu kuagiza gari ya 2004 kwa mfano ni cheap kuliko ya 2010...kuagiza gari siyo issue nzito kama wanavyotishia...niliagiza pajero io nikatishiwa sana...ooooh huliwezi sijui nn...leo mwaka 5 ninalo...
 
Reference Number 1415412147
Make: NISSAN
Model: X-TRAIL
Body Type: SUV
Year of Manufacture: 2002
Fuel Type: PETROL
Engine Capacity: 1001 - 2000 CC
Customs Value CIF (USD): 3114.00
Import Duty (USD): 778.50
Excise Duty (USD): 194.63
Excise Duty due to Age (USD): 1167.75
VAT (USD): 945.88
Total Taxes (USD): 3087
Total Taxes (TSHS): 5541165
 
Hivi utajuaje kiasi cha mafuta yanayotunzwa/reserve ktk tanki kwa gari husika. Na ni nini athari/madhara ktk engine na gari kwa ujumla ya kuendesha gari wakati taa ktk dashboard ya kuku-alert mafuta ktk tank kupungua kiwango cha kawaida inawaka.?!
 
Inategemea gari na gari na ukubwa wa tank! Kwa mfano reserve ya Duet haiwezi kuwa reserve ya Mark X au Brevis! Magari yenye engine kubwa huwa na tank kubwa na automatically reserve pia huwa kubwa
Vyovyote viwavyo taa ikishawaka moja kwa moja bila kuzima una uwezo wa kwenda km 30 ndio izime kabisa, kwahiyo hapo unaweza kufanya mahesabu kulingana na ulaji wa mafuta wa gari lako

MADHARA YA KUTEMBELEA EMPTY TANK/MAFUTA KIDOGO

kwenye tank la gari kuna pump inayochuja na kusukukuma mafuta yaende kwenye mfumo wa engine, ile pump hulala kwenye sakafu ya tank na huinuka kadiri mafuta yanavyokuwa mengi (ina boya)

Mafuta ambayo hayajadhibitiwa vema huingia na chembechembe za michanga, ambazo hutuwama chini ya tank, hivyo ukitembea mafuta kidogo kila wakati pump badala ya kuvuta mafuta inavuta uchafu na hatimaye kuziba na kushindwa kupeleka kiwango cha kutosha kwenye mfumo wa engine

Haya madhara si kitu cha maramoja bali huja taratibu mno, kwahiyo kwa USHAURI
-Epuka mafuta ya videbe/drip
-Epuka kuendesha gari mara kwa mara likiwa halina mafuta ya kutosha
-Epuka kuweka mafuta kwenye vituo vya kienyeji
 
Hivi utajuaje kiasi cha mafuta yanayotunzwa/reserve ktk tanki kwa gari husika. Na ni nini athari/madhara ktk engine na gari kwa ujumla ya kuendesha gari wakati taa ktk dashboard ya kuku-alert mafuta ktk tank kupungua kiwango cha kawaida inawaka.?!

Jaribu hii technique! Taa ikiwaka tu nenda station jaza full tank (hata km ni town trips). Tumia mpk iwake tena weka full tank, hiyo mm inanisaidia sana kuepuka kuua pump
 
Jaribu hii technique! Taa ikiwaka tu nenda station jaza full tank (hata km ni town trips). Tumia mpk iwake tena weka full tank, hiyo mm inanisaidia sana kuepuka kuua pump

Cha muhimu zaidi ni kwenda filling stations nzuri kwa ubora na kuhakikisha muda mwingi mafuta hayapungui mpaka taa kuwaka moja kwa moja
 
Mshana jr mimi nataka kununua gx 100 cresta wiki tatu zijazo,hilo nalo vp?
 
Mshana jr mimi nataka kununua gx 100 cresta wiki tatu zijazo,hilo nalo vp?

Mnyama huyo usimwache tatizo lake ambalo laweza kuwa sio tatizo iko chini sana kwahiyo rough road inabidi kuwa mpole otherwise ni gari ya kijamaaa sehemu kubwa na ubepari kidogo yaani 75/25%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…