Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

mwenye ujuzi wa kuzitofautisha atujuze jamani hata mimi rav4 L na rav4 J zinanichanganya sana
 
Mi nmezitumia na sijagundua tofauti...japo moja ilikua manual nyingine auto ila sikumbuki ipi ilikua L na ipi J, na moja ni 4wheel nyingine sio
 
Wadau naomba kujua kuhusu Passo. Je inaweza kunyanyuliwa kiasi gani na pia inaweza kuingia tairi ya ukubwa gani maximum ?
 
Wadau naomba kujua kuhusu Passo. Je inaweza kunyanyuliwa kiasi gani na pia inaweza kuingia tairi ya ukubwa gani maximum ?

Usiinyanyue asilani na ikibidi kubadili tairi onana na wauzaji was tairi watakushauri vema zaidi
 
Tatzo ni nini ???

Hili nimeshalijibu sana tu huko nyuma, ni hivi
-Gari hupoteza mwonekano wake wa asili
-Gari hupoteza udhibiti wa barabara hasa unapoenda 80+ speed
-Gari hupoteza mneso kwakuwa spring na. Shockups zinakuwa zimebanwa na Spencer
-Central gravity ya gari kuwa mislocated
 
Ninaomba nisaidiwe . Hivi kuna uwezekano security system(alarm) system kwenye gari ika cut power kwenye fuel pump hivyo kusababisha gari kutowaka na ikaonaekana kama fuel pump imekufa?
 
Ninaomba nisaidiwe . Hivi kuna uwezekano security system(alarm) system kwenye gari ika cut power kwenye fuel pump hivyo kusababisha gari kutowaka na ikaonaekana kama fuel pump imekufa?

Upo huo mfumo wa kukata mafuta baada ya gari kutembea kidogo, lakini ishu ya kujua ninini kimetokea ni mpaka mtaalam aje acheki huwezi kufikia tu conclusion kuwa fuel pump imekufa
 
Kwa ushauri tu chukua Toyota Kluger 4WD yenye CC 2400 VVTi ,nzuri sana kwa safari ndefu, stability barabarani ,consumption ya highway ni nzuri, mwisho kwenye rough terrain, tope nk hutajutia kwa kweli , ni muhimu uchukue ya kuanzia mwaka 2004 , zina engine tuning nzuri kuliko za mwaka 2001,2002

Usichukue ya cc 3000, na pia zipo nyingi zisizo na 4WD(kama lengo ni kwenda kwenye vijiji vya Dongobesh,Hydom huko Manyara)hivyo kuwa mwangalifu wakati wa manunuzi
Mwenye wazo tofauti karibu,
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naomba kujua kuna wanatoa thermostat kwenye magari yao wakusema inatumika kwa nchi za ulaya zenye baridi huku kwetu hazihitajiki kwakuwa kuna joto he in sahihi kufanya hivyo?
 
Kaka mshana jr naomba kukuuliza 20m naeza pata toyota vanguard new model? Please i need 2 kno its strenghts & weakness...
 
Kaka mshana jr naomba kukuuliza 20m naeza pata toyota vanguard new model? Please i need 2 kno its strenghts & weakness...

Nafikiri unapata kuna model ya nyuma kidogo ililkuwa 18m ngoja takuchekia
 
Mkuu naomba kujua kuna wanatoa thermostat kwenye magari yao wakusema inatumika kwa nchi za ulaya zenye baridi huku kwetu hazihitajiki kwakuwa kuna joto he in sahihi kufanya hivyo?

Sometimes ni kuleta tu uharibifu kwenye gari, kwakuwa sehemu kama hakuna baridi haiwezi fanya kazi kwahiyo hata ukiiacha haina madhara
 
Kaka nikihitaji kununua gari kwa mtu mkononi vitu muhimu vya kucheki ni nin na nin ndugu?
 
Hbr,nimependa sana jinsi unavotuelimisha humu kuhusu magari,naming nataka kununua Gari ila napenda unisaidie ni Gari gani inauzwa bei ya chini ni ya kisasa na inatumia mafuta kidogo.ni kwa ajili ya safari za mjini tu,ukiweza nitajie bei kaka na wapi zinapatikana.ahsante.
 
Kaka nikihitaji kununua gari kwa mtu mkononi vitu muhimu vya kucheki ni nin na nin ndugu?

Kwanza lazima ukubali kuwa halitakosa kasoro ndogondogo ambazo si tatizo sana

Pili pata fundi mkweli mjuzi na mwaminifu aicheki kisha mfanye wote road test

Tatu angalia kama haidaiwi RL TRA ikiwa ni pamoja na ushuru na usajili, hapa huna jinsi inabidi uende TRA makao makuu kitengo cha investigation ghorofa ya NNE chumba cha kwanza ukitoka kwenye lift, hapo utapewa ukweli kuhusu hizo kodi na uhalali wa gari
 
Pata gari yeyote ambayo cc zake hazizidi 1500, kuhusu uzuri pitia nyuzi za nyuma utapata mengi lakini kwa haraka kuna Cami, IST, DUET, KEI corolla, nk bajeti ni kati ya 6-9m
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…