hard like rock
Member
- Mar 20, 2015
- 16
- 4
Kwanza lazima ukubali kuwa halitakosa kasoro ndogondogo ambazo si tatizo sana
Pili pata fundi mkweli mjuzi na mwaminifu aicheki kisha mfanye wote road test
Tatu angalia kama haidaiwi RL TRA ikiwa ni pamoja na ushuru na usajili, hapa huna jinsi inabidi uende TRA makao makuu kitengo cha investigation ghorofa ya NNE chumba cha kwanza ukitoka kwenye lift, hapo utapewa ukweli kuhusu hizo kodi na uhalali wa gari
Asante mkuu nina swali mim nina gar yangu pia kuna jamaa anataka kuniuzia body tupu nifunge kwenye gari yangu hais sasa kadi itasoma tofauti na body inakuaje hapo ili nioanishe engine namba na cheses namba kwenye kadi yangu?
poa ndugu! Nimekupatakinachozingatiwa hasa tra ni engine no. Chassis no. Body type. Model. Make na rangi, hivyo nenda polisi kapate barua nenda tra wafanye ukaguzi watakubadilishia, ili jiridhishe kwanza hiyo body nyingine gari yake haina matatizo na tra
poa ndugu! Nimekupata
tra kama hyo body itakua inadaiwa itabidi ilipiwe rl. Na je watahtaji kadi yake?
Kwa maoni yangu IST na CARINA
Poa kaka asante kwa ushauri wako ndugu nimepata elimu tosha kwa hloSio hivyo tu pamoja na wizi isije ikawa gari yake ilipigwa mahali na pengine ilihusisha vivo ndio maana huwa inabidi kuanzia polisi
Halafu kuna mtu akishaona gari yake ina shida TRA huamua kuikata na kuiuza spare sasa ukichukua kitu kama engine au chassis na pengine body kuna shida mbeleni
jamani naombeni ushauri hivi ni vitu gani hupelekea gari kuchemsha na ikitokea hivyo nini cha kufanya?
Hiyo spring ya mfuniko ikiwa weak basi pressure ndogo tu ya maji ndani radiator itaruhusu maji yahamie kwenye reserve tank,ingawa pia maji yaliyo kwenye reserve tank hutakiwa kurudi ndani ya radiator ikiwa radiator imepungukiwa na maji.
Shukrani sana wakuu. Gari yangu toyota hilux inatumia engine ya 3y. Tatizo lake nikipita kwenye madimbwi ya maji tu inapoteza nguvu, inaingiza miss na inazima hapo mpaka niiwashe kwa kuikanyagia sana ndo inakubali nikiiendesha kidogo ile mis inapotea tatizo laweza kuwa nini manake fundi akikagua anasema kila kitu kiko sawa?
Kuna muda pia nikitembea umbali mrefu kama km 50 tu inaweza ikatokea hiyo kupoteza nguvu kabisa na kuzima ila ikipoa inaenda vizuri tu na mis inapotea.
Tatizo jingine engine inachemka sana sana hebu nishaurini kwa kuanzia. Transmision ni auto