Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Kwanza lazima ukubali kuwa halitakosa kasoro ndogondogo ambazo si tatizo sana

Pili pata fundi mkweli mjuzi na mwaminifu aicheki kisha mfanye wote road test

Tatu angalia kama haidaiwi RL TRA ikiwa ni pamoja na ushuru na usajili, hapa huna jinsi inabidi uende TRA makao makuu kitengo cha investigation ghorofa ya NNE chumba cha kwanza ukitoka kwenye lift, hapo utapewa ukweli kuhusu hizo kodi na uhalali wa gari

Asante mkuu nina swali mim nina gar yangu pia kuna jamaa anataka kuniuzia body tupu nifunge kwenye gari yangu hais sasa kadi itasoma tofauti na body inakuaje hapo ili nioanishe engine namba na cheses namba kwenye kadi yangu?
 
Kinachozingatiwa hasa TRA ni engine no. Chassis no. Body type. Model. Make na rangi, hivyo nenda polisi kapate barua nenda TRA wafanye ukaguzi watakubadilishia, ili jiridhishe kwanza hiyo body nyingine gari yake haina matatizo na TRA
 
kinachozingatiwa hasa tra ni engine no. Chassis no. Body type. Model. Make na rangi, hivyo nenda polisi kapate barua nenda tra wafanye ukaguzi watakubadilishia, ili jiridhishe kwanza hiyo body nyingine gari yake haina matatizo na tra
poa ndugu! Nimekupata
 
wakuu naomba ushauri wenu nataka kuagiza gari moja wapo kati ya hizi katikati ya mwezi may IST,CARINA,CORONA PREMIO., nahitaji ushauri wenu wakuu
 
tra kama hyo body itakua inadaiwa itabidi ilipiwe rl. Na je watahtaji kadi yake?

Sio hivyo tu pamoja na wizi isije ikawa gari yake ilipigwa mahali na pengine ilihusisha vivo ndio maana huwa inabidi kuanzia polisi

Halafu kuna mtu akishaona gari yake ina shida TRA huamua kuikata na kuiuza spare sasa ukichukua kitu kama engine au chassis na pengine body kuna shida mbeleni
 
jamani naombeni ushauri hivi ni vitu gani hupelekea gari kuchemsha na ikitokea hivyo nini cha kufanya?
 
Poa kaka asante kwa ushauri wako ndugu nimepata elimu tosha kwa hlo
 
jamani naombeni ushauri hivi ni vitu gani hupelekea gari kuchemsha na ikitokea hivyo nini cha kufanya?

Cooling system inakuwa na faults hasa kwenye radiator ikiwa chafu, fan ya radiator kutozunguka au kukosa nguvu, pipe za maji kuvuja au kutopitisha maji vizuri, compressor ya AC kuwa na nguvu kuliko engine(kama haifanyi kazi vizuri)
MFUNIKO wa radiator nao ni sababu kubwa sana! Mifuniko original ina spring ambayo hutanuka kuruhusu hewa/ mgandamizo toka kwenye radiator upenye na hivyo radiator kupumua, sasa ile spring ikifa au ukipoteza ule mfuniko ukapata feki gari itachemsha mpaka utaikimbia
 
How radiator cap works 1429424887873.jpg1429424904497.jpg1429424919208.jpg1429424935522.jpghaka kadude ni kadogo sana kwenye gari lakini kana kazi kubwa sana kwenye gari
 
Hiyo spring ya mfuniko ikiwa weak basi pressure ndogo tu ya maji ndani radiator itaruhusu maji yahamie kwenye reserve tank,ingawa pia maji yaliyo kwenye reserve tank hutakiwa kurudi ndani ya radiator ikiwa radiator imepungukiwa na maji.
 
Thanx leipzig nilisahau kuhusu hilo
 
Last edited by a moderator:
Shukrani sana wakuu. Gari yangu toyota hilux inatumia engine ya 3y. Tatizo lake nikipita kwenye madimbwi ya maji tu inapoteza nguvu, inaingiza miss na inazima hapo mpaka niiwashe kwa kuikanyagia sana ndo inakubali nikiiendesha kidogo ile mis inapotea tatizo laweza kuwa nini manake fundi akikagua anasema kila kitu kiko sawa?
Kuna muda pia nikitembea umbali mrefu kama km 50 tu inaweza ikatokea hiyo kupoteza nguvu kabisa na kuzima ila ikipoa inaenda vizuri tu na mis inapotea.
Tatizo jingine engine inachemka sana sana hebu nishaurini kwa kuanzia. Transmision ni auto
 
habari wadau?
mimi nauliza kuhusu toyota platz na honda Hr-v ziko vipi ? uimara , spares matumizi ya mjini na barabara ya vumbi mara moja moja.. kati ya hizo mbili ipi ni bora zaidi kama unamshauri mtu anayetaka kununua?
 
naombeni kwa mwenye ufaham kuhusu bmw x 3 atujuze

BMW karibia zote ni gari bomba na imara sana kuanzia body mpaka mashine kimoja na cha muhimu hazitaki shida nyingi na vipuri viko juu
 
Shukrani sana wakuu. Gari yangu toyota hilux inatumia engine ya 3y. Tatizo lake nikipita kwenye madimbwi ya maji tu inapoteza nguvu, inaingiza miss na inazima hapo mpaka niiwashe kwa kuikanyagia sana ndo inakubali nikiiendesha kidogo ile mis inapotea tatizo laweza kuwa nini manake fundi akikagua anasema kila kitu kiko sawa?
Kuna muda pia nikitembea umbali mrefu kama km 50 tu inaweza ikatokea hiyo kupoteza nguvu kabisa na kuzima ila ikipoa inaenda vizuri tu na mis inapotea.
Tatizo jingine engine inachemka sana sana hebu nishaurini kwa kuanzia. Transmision ni auto

Kuna shida kwenye gearbox na mfumo wa umeme fanya diagnosis haraka, lakini hakikisha unampata funding mahiri, mzoefu na mwaminifu ni muhimu sana ili kuepuka guess works, pia acheki pump na fuel system
 
Back
Top Bottom