Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali


Kama una contact na mtu Nairobi au South Africa agizia huko
 
Nakubaliana nawe kabisa nilichosema mimi ni engine za 2lt, na kuhusu turbo nimemshauri asiweke engine ya hivyo kwakuwa mafundi wengi ni majanga

Nimekuelewa mkuu ushauri wako naukubali hasa hapo ulipogusia mafundi majanga !!!
Ila kwa manufaa ya jukwaa mafundi hawa kanjanja ndio huwa wanawafikisha watu kwenye dead end na gharama lukuki.
Nikupe Mfano ,karibu turbocharged 2 series zote za miaka ya tisini, kutoka Toyota (2c T, 2l T, 2h T) hazikupata jina zuri kwetu kutokana na mafundi wetu kutozijua undani wake,

Ni hivi katika kila engine , ie 2l T kulikuwa na version mbili, moja turbocharged , ya pili turbocharged and intercooled , trend hii Toyota wameitumia mpaka miaka ya hivi karibuni ilipokuwa mandated kuwa kila turbocharged engine must be intercooled. Kitaalam kazi ya intercooler ni kupooza hewa ya moto kutoka kwenye turbo , engine yenye turbo pekee bila kuwa na intercooler huwa na desturi ya kuwa na nguvu pamoja na kasi sana , lakini kwa wakati huo huo , zina kawaida ya kupata joto kwa haraka sana , na hivo uwezekano wa kuchemsha ni mkubwa sana ,
Njia pekee ya kuishi na engine zenye turbo bila intercooler ni kuhakikisha kuwa hutumii nguvu yote za engine ,(don't push to the limit) hata Kama gari itaonesha kuwa bado ina uwezo , mfano badala ya kupanda mlima gia namba tano full trottle, tumia via namba nne , half throttle... Hii huifanya cooling system kutobeba mzigo mkubwa wa joto na ndio utakuwa unaokoa maisha ya engine yako,

Bahati mbaya Toyota surf nyingi zilikuja na 2L T bila intercooler , ndo maana zikaonekana mbovu .
 

Duu aisee asante sana binafsi nimejifunza kitu hapa kuhusu turbocharged na intercooler, natamani wenye haya magari yenye hizi specifications wapitie hapa! Binafsi na kusema kweli nilikuwa nadharau sana engine za 2LT, na kwakweli wengi wameingizwa mikenge na mafundi kanjanja na kuharibu engine zao
Nakumbuka mwaka 2006 pale Temeke Davis corner kulikuwa na gereji nyingi sana, tukakuta Surf bomba kabisa 2LT turbo, tuliiacha kwasababu ya kigezo kimoja tu ENGINE ni 2LT
 

Ndio hivo mkuu, tuna tatizo Kubwa la mafundi kuliko tunavyodhani
 
Ni nzuri ila sio imara hasa huko chini kwenye wish-bones , tyrodends ball joints na stabilizer links huyo ndio ugonjwa wake mkubwa

hizi tyrodends ball joints , wish-bones na stabilizer links ni vitu ghali sana na huwa vinadum vikibadilishwa?
 
hizi tyrodends ball joints , wish-bones na stabilizer links ni vitu ghali sana na huwa vinadum vikibadilishwa?

Original genuine ni ghali ila vinadumu! Vya maduka mengi Dar ni feki, Lakini vyovyote iwavyo hivi vitu vina aleji ya maji na matope
 
Duu nafikiri ni tierod ends,mimi nilizungumzia kwa ujumla wake tu, swali lako liko sahihi BTW links na tierod ends ni vitu viwili tofauti kwa ufahamu wangu (I may be corrected)

Wayiiii........vitajibeba.......bora gari iende.......
 
Au aseme........wakati anabadili shockups........coil zipoje........?......tuanzie hapo.......

Aisee Preta shida hapo ni hizo shockups, hizi spare nyingi hapa dar ni majanga, unabadili leo baada ya miezi mitatu ni kwichi kwichi kwichi
 
Last edited by a moderator:
Ok. Nakushukuru sana kaka @ mshana jr kwa maelezo yako.. Nikianza mchakato ntakushtua coz am not expert. God bless u
 
Wanajamvi naomba kujua jinsi ya kunigotiate bei wakati wa kununua gari mtandaoni..eg beforward...yaan unafanyanyaje hadi wakupunguzie bei...iliyoko kwenye tangazo....tafadhalini...
 
Wanajamvi naomba kujua jinsi ya kunigotiate bei wakati wa kununua gari mtandaoni..eg beforward...yaan unafanyanyaje hadi wakupunguzie bei...iliyoko kwenye tangazo....tafadhalini...

Hakuna ufundi zaidi ya kuwapa ofa yako wakiikubali mnafanya biashara
 
Kaka Mshana nahitaji kununua Suzuki escudo naambiwa ni imara na ngumu ila bei ndio kubwa. Mfano nimeuliza yard ya mhindi mmoja kasema m37 ya 2006. Nawezaje pata ya bei chee, je uimara wake upoje?

Dah kaka nikipata hii gari ntafurahi sana. Ushauri tafadhali jmn hasa kwenye naeza pata kwa bei ndogo kdg. Asante
 

Naomba jaribu showrooms tofauti tofauti na kwenye mtandao pia, nafikiri unaweza pata chini ya hiyo bei tukumbushane Jumamosi naweza kuwa na jibu

Ni gari ya kisasa kwahiyo inahitaji utunzaji ukizingatia taratibu za kulitunza gari utaipenda na kuifurahia
 

Asante sana kaka, nitafuatilia
 
All in all, engine ya 2L-TE haina nguvu kwa kweli. Nilinunua prado yenye engine hiyo, nikipakia watu saba na kuwasha AC, hata Scania lorry inanipita. Nikavua kule na kuweka 1KZ. Si engine ya kwenda 120 km/h ukiwa na abiria.
 


Unawezapata kwa bei chini kidogo kama upo serious nicheck pm naweza kuunganisha na mtu atakayeweza kukupatia kwa gharama nafuu kidogo
 

Mshana hutu tugari vipi kwenye ubora, naviona old model vingi vya zamani viko njiani tu vikina Samurai, vitara & escudo naona kamekaa vzr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…