Nimekuelewa mkuu ushauri wako naukubali hasa hapo ulipogusia mafundi majanga !!!
Ila kwa manufaa ya jukwaa mafundi hawa kanjanja ndio huwa wanawafikisha watu kwenye dead end na gharama lukuki.
Nikupe Mfano ,karibu turbocharged 2 series zote za miaka ya tisini, kutoka Toyota (2c T, 2l T, 2h T) hazikupata jina zuri kwetu kutokana na mafundi wetu kutozijua undani wake,
Ni hivi katika kila engine , ie 2l T kulikuwa na version mbili, moja turbocharged , ya pili turbocharged and intercooled , trend hii Toyota wameitumia mpaka miaka ya hivi karibuni ilipokuwa mandated kuwa kila turbocharged engine must be intercooled. Kitaalam kazi ya intercooler ni kupooza hewa ya moto kutoka kwenye turbo , engine yenye turbo pekee bila kuwa na intercooler huwa na desturi ya kuwa na nguvu pamoja na kasi sana , lakini kwa wakati huo huo , zina kawaida ya kupata joto kwa haraka sana , na hivo uwezekano wa kuchemsha ni mkubwa sana ,
Njia pekee ya kuishi na engine zenye turbo bila intercooler ni kuhakikisha kuwa hutumii nguvu yote za engine ,(don't push to the limit) hata Kama gari itaonesha kuwa bado ina uwezo , mfano badala ya kupanda mlima gia namba tano full trottle, tumia via namba nne , half throttle... Hii huifanya cooling system kutobeba mzigo mkubwa wa joto na ndio utakuwa unaokoa maisha ya engine yako,
Bahati mbaya Toyota surf nyingi zilikuja na 2L T bila intercooler , ndo maana zikaonekana mbovu .