Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Hahahahaaaaaaa nafikiri ni kazi na dawa
 
Mkuu vipi kuhusu gari za NISSAN body type- sedan ? Mfano primera, skyline etc zina uzuri au ubovu gani? Kwanini hazipendelewi hapa kwetu?

Nissan ni nzuri sana body zake lakini zile za nyuma hizi za siku hizi body zake ni nyanya na hii si kwa Nissan tu bali gari nyingi za kisasa
Nissan zinaogopewa hapa kwetu kwa kuwa wengi wana ile notion ya ughali wa spare
 
Hahahaaa, Sorry mkuu, tatizo ni muonekano peke yake au kuna lingine? then wewe ni jinsia gani?
Ushauri wa fasta:
Uza hiyo Killi time, nunua hiyo ya 2006
 
Tafadhari wadau,

Ni wiki ya pili sasa nateseka na spea ya gari bila mafanikio. Nahitaji puli yenye sensor ya Rav4, 3s, VVti, Yamaha engine. Upande mmoja ina meno 32 upande mwingine meno 23.

Tafadhari hata taarifa za masuper dealer wa spares nitashukuru sana.

Nawasilisha
 
Hahahaaa, Sorry mkuu, tatizo ni muonekano peke yake au kuna lingine? then wewe ni jinsia gani?
Ushauri wa fasta:
Uza hiyo Killi time, nunua hiyo ya 2006

Kama watu wanaweza kubadili engine, mataili, viti nk, mfano wanatoa engine ya Benz kwenye Body yake wanaweka ya Corolla! Au wanatoa taili size 14 wanaweka 15 na gari inakuwa sawa tu, iweje Steering (Usukani) wa aina ya gari hiyo hiyo ishindikane kwa ajili ya toleo tu?

Ngoja wanaojua ufundi wa magari waje siyo wewe dereva usiyejua ufundi wa kutengeneza.
mshana jr njoo uokoe jahazi mtalaamu wetu
 
Last edited by a moderator:
Natanguliza shukrani wakuu. Ivi kati ya suzuki swift ya kuanzia mwaka 2006 na Toyota vitz ya kuanzia mwaka 2006, ipi ina market value wakati wa kuuza?
 
wadau naombeni kujuzwa kati ya injini ya rav4 3s na 4s ipi yenye nguvu zaidi?
 
Steering hasa za same make zinaingiliana vizuri tu bila shida yoyote, kuna watu hutoa original steering na kuweka sports steering au zile zenye madoido
 
Last edited by a moderator:
Wadau naomba kujua matatizo ya engine za ZD30 hasa iliyofungwa kwenye Nissan Patrol
 
Vip unaweza kuniambia ubora na mapungufu ya Toyota-wish,bei zake zinaendaje show room na kuagiza
Natanguliza shukulani zangu kwako mshana jr
 
Last edited by a moderator:
Vip unaweza kuniambia ubora na mapungufu ya Toyota-wish,bei zake zinaendaje show room na kuagiza
Natanguliza shukulani zangu kwako mshana jr
mdocho niwie radhi kwa hili lakini Toyota wish ni gari nyanya kwa body hata na vinginevyo hasa huko chini kwenye bushes ball joints na gearbox
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ni gali ipi inweza kumfaa mtu wa hali ya chidi kuanzia bei,uimara pamoja na matumizi ya mafuta!!!
 
Nissan ni nzuri sana body zake lakini zile za nyuma hizi za siku hizi body zake ni nyanya na hii si kwa Nissan tu bali gari nyingi za kisasa
Nissan zinaogopewa hapa kwetu kwa kuwa wengi wana ile notion ya ughali wa spare

Pamoja na ughari wa vipuri Nissan ni gari ambazo ni stable barabarani hasa ukiwa high speed.
 
Mkuu ni gali ipi inweza kumfaa mtu wa hali ya chidi kuanzia bei,uimara pamoja na matumizi ya mafuta!!!

Chukua hizi corolla carina Ti na akina Duet na cami hizi nyingine za kisasa kina Porte na Siensta ni majanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…