Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Wakuu napenda kufaham hiv ac kwenye magari nikweli zinaongeza fuel cunsuption?

Ac inaongeza ulaji wa mafuta sana sana kwa magari yote madogo pamoja na magari makubwa ya abiria.na kwa upande wa magari madogo tofauti unaweza kuigundua unapokua kwenye foleni au kwenye mwendo mdogo,lakin mwendo wa 80kph kuendelea huwezi kuona tofauti yoyote.kwa upande wa magari makubwa ya mizigo naweza kusema uwezi kuona tofauti yoyote na hili linasababishwa na ukubwa wa engine wakati cabin yake ikiwa inalingana na ya vits kwahiyo na pump ya ac watengenezaji uweka ndogo kitu ambacho injin haiwez kustrugle hata kdg
 
Kwanza nianze na hiyo ECT kirefu chake ni Electronically Controlled Transmission, kwa urahisi ni batani inayokuwezesha kulipa gari udhibiti binafsi wakati linapopita maeneo yenye changamoto kwake Mf.mlima,mteremko,barafu,tope zito nk ECT kile inafanya ni kupunguza mabadiliko ya Mara kwa Mara ya gia kwa mfano ukiibonyeza hiyo batani ktk PWR mode wakati unapanda mlima automatically gia za kupanda mlima aghlabu 1,2au3 zitakuwa zikijiseti kulingana na ukubwa wa mlima ukiweka batani ktk PWR mafuta zaidi yanatumika Ila injini nguvu yake inaongezeka,haishauriwi uiweke on kwenye normal town cruises,wenzetu kwenye barafu Kama huko Ulaya wanatumia hiyo batani Kama special effect kuwezesha gari kuhimili uterezi kwa sababu ECT huwezesha ongezeko la nguvu ya injini kwa kushabihisha na mzunguko wa injini kwa dkk-rpm, hapa Tanzania hiyo special effect inapatikana zaidi ktk Lexus,Escudos,baadhi ya corolla na mengineyo,
Kwa mukhtasari ECT batani husaidia gari kutumia low gear kwa muda mrefu.

Mkuu umenipa mwanga hapa, hebu nipe ushauri wa hizi cruiser v8 petrol engine ulaji wake wa mafuta naziona sana sakoni miaka hii
 
Vipi kuhusu hizi probox jamani, naziona tu barabarani na watu wanazisifia kuwa ni nzuri. Vipi zinahimili barabara zetu hizi rough na fuel consumption ikoje?

Nice car, engine yake ni imara hata bodi yake ni bati imara mikoani kv Njombe wanaitumia Kama tax,japo sijaona wengi wakiipendelea hapa Dar labda sa'bu iko chini
 
Wakuu napenda kufaham hiv ac kwenye magari nikweli zinaongeza fuel cunsuption?
Ndio,mzunguko wake unatumia kiwango fulani cha kadiri cha horsepower ya jumla ktk gari yako, so inaconsume fuel ingawa ulaji wa mafuta sio kiwango kikubwa Kama watu wanavyoexaggerate labda mifumo ya AC iwe below standards/mibovu kv tatizo la pipes kuvuja nk,ingawa huko sie hatushughulikii sana sie engine zaidi Kama una shida ya repairs npm
 
Wengi wetu tunanunua used kutoka Japan na Europe. Unaweza kukuta manual au usiikute, na inaweza kuwa imeandikwa kijapan!

Download op. manual books zipo online bei chee kuanzia $ 5 -300 kutegemeana na aina ya gari
 
Mimi naombeni kujua ubora na matumizi ya mafuta kwa gari aina ya Toyota Ipusm model 240S zinazotumia engine za 2AZ-FE.
 
Mi nataka kujua kuhusu Nissan X-Trail,uzuri wake na matatizo yake kwenye matumizi ya kawaida
sasa hivi naona bongo zimekuwa nyingi tofauti na zamani watu walikuwa wanaziogopa
 
Mi nataka kujua kuhusu Nissan X-Trail,uzuri wake na matatizo yake kwenye matumizi ya kawaida
sasa hivi naona bongo zimekuwa nyingi tofauti na zamani watu walikuwa wanaziogopa
Kama huna kipato cha kueleweka hiyo gari usinunue itakutesa hasa gharama ya vipuri
 
Nina Nissan x-trail nliinunua from Japan 2009, taa ya kuonyesha kuna tatizo kwenye engine inawaka na baada ya kuifanyia diagnosis wananiambia tatizo ni VVTI senser, duka la master card hawana, kuna watu wananiambia Ilala naweza kuuziwa mbovu pia, je naweza kuipata wapi?
 
Hilo la gharama ya spare ni kweli nimelisikia siku nyingi kwa upande wa X-TRAIL
 
Ni kweli vipuri vyake ni gharama lakini uzuri wake ukinunua vinadumu kwa muda mrefu sana na unasahau.

mwenye ushuhuda wa kumiliki aina hii ya gari kwa muda mrefu atupe uzoefu na sisi.....naipenda ile option yake ya 2wd na 4wd na cc zake si nyingi
 
Nataka kununua gari aina ya SUZUKI Kei cc650 kuna mtu mwenye ufahamu mzuri wa hizi gari upande wa spare parts na kama kuna tatizo!!! Naona inafaa kwa ulaji mdogo wa mafuta na 4wd inasaidia ukipita sehemu zenye mchanga!!
 
Back
Top Bottom