Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

mshana jr haunitendei haki kwenye ili swali langu, sijapata jibu.
Mokoyo samahani kwakweli nilitaka kufanya hivyo jana nikasahau unajua kwasasa sipo mjini na huku nilipo ni mpaka nipate wireless ndio nakuwa hewani
Ti ni nzuri sana kwenye mafuta na ni gari imara pia ila kwa safari sio kivile hasa kwenye ishu ya mwendo!kwa misele ya mjini in alipanga sana
 
Last edited by a moderator:
Invisible tunaomba hii thread muiweke sticky jamani, hebu tusaidieni japo kwa hili wakuu maana kutuanzishia kajukwaa ketu imeshindikana, Tuwekeeni badi hii sticy, au kuna masharti yoyote wakuu tusaidiane kutekeleza?
 
Last edited by a moderator:
Kuna hii gari inaitwa NISSAN MURANO.Hebu mwenye uzoefu anisaidie.Kujibu maswali haya mafupi.
1.Strenghs zake ni zipi hasa?
2.Weaknesses zake ni zipi?
 
Kuna hii gari inaitwa NISSAN MURANO.Hebu mwenye uzoefu anisaidie.Kujibu maswali haya mafupi.
1.Strenghs zake ni zipi hasa?
2.Weaknesses zake ni zipi?

Gari nzuri ina speed ni ngumu ulaji wa mafuta ni mzuri kwa maana ya kwamba ukizingatia kanunuliwa za kuendesha automatic ina nafasi kubwa ndani (sio kwa ajili ya kufanyia matusi lakini)

Weaknesses zake ni kwamba inahitaji utunzaji na bei iko juu si chini ya m30
 
Ahsante Mshana Jr kwa Ushauri mzuri.Nahitaji ufafanuzi zaidi uliposema "Inahitaji utunzaji".

Na vipi kuhusu upatikanaji wa SPEA zake?
 
Kha! Umenichekesha hapo kwenye mabano
 
Ahsante Mshana Jr kwa Ushauri mzuri.Nahitaji ufafanuzi zaidi uliposema "Inahitaji utunzaji".

Na vipi kuhusu upatikanaji wa SPEA zake?

Gari ni kama kitu kingine chochote inahitaji utunzaji na uangalizi wa karibu kwa maana ya uendeshaji na kufanya service kila muda unapofika na kutumia lubricants genuine na spare genuine pia

Spare parts sio kwamba nafagilia sana Kenya ila ndipo karibu ambapo mtu anaweza kupata chochote kwa bei nzuri/nafuu na genuine
 
Gari ni kama kitu kingine chochote inahitaji utunzaji na uangalizi wa karibu kwa maana ya uendeshaji na kufanya service kila muda unapofika na kutumia lubricants genuine na spare genuine pia

Spare parts sio kwamba afagilia sana Kenya ila ndipo karibu ambapo mtu anaweza kupata chochote kwa bei nzuri/nafuu na genuine

Ahsante Mkuu Mshana Jr kwa Ushauri murua.
 
Naombeni mnieleweshe hichi kitu, hivi ni kwanini mtu anaposafiri na gari muda mrefu kisha akasimama sehemu fulani huwa hashauriwi kuzima gari? Je huwa inahitajika muda gani upite ili yeye aweze kuzima gari pale aliposimama. Asanteni.
 
Kuna majibu hapo juu kwenye post zilizotangulia jaribu kupitia kuna majibu ya kutosha
 
Wakuu kuna hii kitu, gari kuwa "silence" juu kila ukiwasha asubuhi na baada ya about 2mins silence inarudi kawaida. Je ni tatizo au kawaida?
 
Wakuu kuna hii kitu, gari kuwa "silence" juu kila ukiwasha asubuhi na baada ya about 2mins silence inarudi kawaida. Je ni tatizo au kawaida?

Mfano wake unapoamka asubuhi unajisikia mwili kuchoka lakini kadiri dkk zinavyojongea unapata nguvu,samewise kwa gari so worry out
 
ABS inapokuwa katika ubora wake hufanya kazi popote! Lakini hilo la barabara ya vumbi kutofanya Nazi vizuri linahitaji utafiti zaidi kuliko majibu ya kubahatisha

Mimi ni mhanga. Nilikuwa kasi kwenye mashimo, kufunga brake pad zinaachia kama vile inavyokuwa ngumu kufunga mkanda kwenye mashimo. Lakini hii hali hutofautiana kati ya gar na gari.

ABS inafanyaje kazi?
Kuna sensor moja ina usumaku ambayo ina connection kati ya brake pad/ liner na mfumo wa Hydraulic. Sasa, ukiendesha gari, unapofunga brake tairi ikislide sensor zinazuia mafuta ya hydraulic yasije na hivyo brake haishiki na tairi likianza kuzunguka tena sensor zinaruhusu mafuta kuja na pad zinafunga na breki kupatikana. Process hiyo ya kuruhusu au kutoruhusu hufanyika ndani ya muda mfupi( fraction of seconds). Hali hiyo ya ABS kukataa breki inasaidia kutosikia zile kelele za tairi kruuuu pale ufungapo breki,kwamba tairi likiteleza tu automatically pad zinaacha likijaribu kuzunguka tu breki inajirudia, sensor haziruhusu kabisa tairi kulia ule mlio wa kizamani ambao ukifunga breki kali gari linateleza na kama ni kwenye ukingo unaweza kupinduka maana litaslide. Kule ndani ya gari lako unaweza kudisconnect boya( switch za mfumo) halafu jaribu kufunga breki gari utaona inashika lakini linateleza vibaya. Ukirudishia breki zinakuwa na taadhima
 
Nataka kujua nini tofauti kati ya gari inayotumia timing chain na timing belt?
 
Nakubaliana na wewe mkuu ila horse power zinatofautiana kati ya 6 na 4. Pia 4 cylinder YAHAMA waliongezea ujuzi pale na kuifanya 3S engine zilizofungwa kwenye altezza zote za RS200 kuwa more powerful and sport handling

Mkuu ebu niongezee somo apo kwenye rs200 kwenye altezza
 
Gari nzuri ina speed ni ngumu ulaji wa mafuta ni mzuri kwa maana ya kwamba ukizingatia kanunuliwa za kuendesha automatic ina nafasi kubwa ndani (sio kwa ajili ya kufanyia matusi lakini)

Weaknesses zake ni kwamba inahitaji utunzaji na bei iko juu si chini ya m30

Kanuni za kuendesha automatic ni zipi?
 
Kwakweli sidhani kama hapa kwetu tuna wataalam wa hiyo kitu ila najua Nairobi ipo, kinachoangaliwa ni pressure, sensor na wiring kama hakuna malfunctions, ndo maana huwa unakuta kuna baadhi ya magari ikitokea mizinga airbags hazifunguki

Makampuni makubwa kama Toyota Nissan nk nafikiri wanaweza kuwa na hiyo mitambo

Mkuu heshima mbele.

Hizi Airbags zinapoundwa na kufungwa toka kiwandani kwenye gari husika zinakuwa zinaishi kwa muda wote wa maisha ya gari hiyo mpaka pale inapotokea ajali kubwa ambayo itasababisha airbag itoke.

Airbag inapotoka kutokana na ajali ya gari basi huwa inabadilishwa na mafundi wenye ujuzi na magari yaliyopata ajali.

Naona tuendelee na darsa.
 
Back
Top Bottom