Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Wadau ni kweli brevis ni gari la gharama kulimudu kuliko mark X haswa kwenye case kubwa ya saiv VIPULI na MAFUTA.....juzi nimepeleka mark X dodoma, niliweka full tank pale filling station ya TOTAL mlimani city lakini nimefika dodoma gari ilikua imetumia mafuta nusu tank kwa chini kidogoooo, na nilikua natembea speed na kiyoyozi juu.

Lakini nimekuja kusafiri na brevis tena kutoka dar to dom nikajaza full pale pale city lakini niliingia dodoma gari imebaki robo tank.....

Na gari zote hizi hakuna iliyovuka CC 2500, zote 6 cylinder..
 
Hapana hili la airbag kuhitaji service nilipo pata Nagasaki Japan kwa mtaalam wa airbags! Ni sawa na gari unatakiwa kufanya service baada ya kilometres fulani usipofanya hakuna tatizo lakini performance na lifespan ya gari inapungua ndio hivyo hivyo kwa airbags!
Binafsi nimeshakutana na kesi zaidi ya sita za head collition na airbags hazikufunguka na kwenye kesi zote hizo ilikuwa ni gari za 1995-1999s
BTW kubadilisha airbag pekee kwenye steering na dashboard bila kubadili sensors/ control box ni kazi bure kwakuwa kinachosense mshindo/impact ni sensors zilizopo kwenye control box na steering

Hapana mkuu.Alivyosema Richard ndio sahihi, Airbag ikishapachikwa kwenye sterling haiguswi wala sensor haiguswi, Airbag sio kama tunavyobadilisha Oil au spark Plug. Airbag sio hivyo, ikishafungwa pale inasubiri tu ajali itokee ikulinde si zaidi ya hilo.
 
Msaada wana jamvi gari yangu raum old model nikiendesha sehemu ya muinuko speed inapungua

Nadhani piston rings za pressure zitakua zimekwisha au block engine imetanuka. Cheki pia kama kiasi cha moshi kimeongezeka ina maana oil rings kwenye piston zimekwisha. Ni mtazamo wangu tu
 
Check pia kama ina leakage ya exos na silenter,kwe mlima check overdrive


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
waungwana niko njiani naenda mwanza natoka Moro nina GX 100,imebadili mlio na sasa nasikua kama mruzi hivi,itakuwa nn hiki?chonde usiku ndo huu niendelee na safaru?
 
waungwana niko njiani naenda mwanza natoka Moro nina GX 100,imebadili mlio na sasa nasikua kama mruzi hivi,itakuwa nn hiki?chonde usiku ndo huu niendelee na safaru?

Sio exhaust kweli hiyo? Vp taa za dashboard ziko sawa? Cheki na tairi pia angalia na mabadiliko ya gear
 
Kwa nini wabongo tunanunua migari ya kufanana wote? Rav 4 namba1, ist mmmh kero kila gari 5 basi 2ist. Tatizo ni nini?
 
Back
Top Bottom