Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

habari wadau?
mimi nauliza kuhusu toyota platz na honda Hr-v ziko vipi ? uimara , spares matumizi ya mjini na barabara ya vumbi mara moja moja.. kati ya hizo mbili ipi ni bora zaidi kama unamshauri mtu anayetaka kununua?

Mmh platz ni majanga kuanzia body mpaka injini zinahitaji handle with care kama hujachukua achana nayo
 
habari zenu wadau,naomba mnijuze maana ya wheel balance na wheel alignment,zinanichanganya sana.Pia gari yangu ikitembea spidi kubwa tairi inavuta kidogo na kutaka kunitoa barabarani,nifanye nini?
 
Kuna jambo fani limenipa wasiwasi hapa naomba kuuliza ili nijue kama linaweza kuleta madhara gani. Mwaka jana nilipata ajali na gari yangu ikawa imeharibika sana na nilikuwa na bima ndogo so nikaamua kuikata kata nikauza spea, kuna jamaa alikuja akataka nimuuzie kadi na plate number pamoja na kibati flani chenye engine number. Nataka kujua kama inaweza kuleta madhara yeyote kwangu maana huyo jamaa alinishawishi kwa laki nane nikampa sa kwa maelezo ya watu hapa napata wasiwasi.

Mghosi
 
Huyo alikuwa na gari ambalo aidha alilingiza bila kulipia ushuru, au lilikuwa linadaiwa RL ndefu lakini hasahasa alikuwa na gari ya wizi hivyo alienda kubadili kila kitu kupoteza ushahidi

Hicho kibati ndio kina engine no, model, make, color trim vitu ambavyo ndio vinasoma kwenye kadi
 
Tumpiche nashindwa kukuquote sijui kuna nini lakini hicho cha gari kuhama ni wheel balancing yaani tairi haziko sawa, kuna moja inamzidi mwenzake
Wakati alignment ni - adjustment of the wheels' angles so that they would be parrel to each other and perpendicular to the road, na hii mara nyingi ni kwa ajili ya afya na maisha ya tairi 1429463468725.jpg
 
Last edited by a moderator:
Tumpiche nashindwa kukuquote sijui kuna nini lakini hicho cha gari kuhama ni wheel balancing yaani tairi haziko sawa, kuna moja inamzidi mwenzake
Wakati alignment ni - adjustment of the wheels' angles so that they would be parrel to each other and perpendicular to the road, na hii mara nyingi ni kwa ajili ya afya na maisha ya tairiView attachment 244928

sante mkuu
 
Last edited by a moderator:
Mara zote magari yanayouzwa online huoneshwa gari husika limekwisha tembea km kiasi gani.
Je! Gari likifikisha km ngapi linakuwa mkweche au skrepa kabisa?
 
Ingawa km sio kipimo pekee cha uzee au uchakavu wa gari, as kama linapata matunzo mazuri na services muda muafaka gari, linaweza fikisha km mpaka mililion moja na liko vizuri. Ila kama unataka kununua used car from Japan, inashauliwa kuangalia mwaka wa gari na km zilizopo. On average gari hutembea angalau km 10,000 kwa mwaka, so kama lina miaka 10, basi km 100,000 plus. ila ukipata lililo chini ni vizuri zaidi, ila lisiwe chini saana kama km 30,000 kama lina umri mkubwa. Pia lisizidi km 150,000.

Kwa European cars, tafuta lenye km chache, maana magari yao yana systems nyingi za umeme. Likitembea km nyingi systems nyingi zinaanza ku fails. So angalau lisizidi km 100,000
 
Mkuu inategemea na aina ya gar plus engeen quality...km zinachakachuliwa hiz.unaweza kuta km chache kumbe gar hamna kitu
 
Mara zote magari yanayouzwa online huoneshwa gari husika limekwisha tembea km kiasi gani.
Je! Gari likifikisha km ngapi linakuwa mkweche au skrepa kabisa?

Kuna vigezo vingi zinapaswa kuangaliwa kabla ya kusema gari ni mkweche ama la kwa kutumia kigezo cha km.
Mathalani ukubwa wa injini.Landcruiser yenye km 150k ni tofauti na Vitz yenye km 150k ama pikipiki.

Lakini vile vile suala la service ni muhimu.Gari inayofanyiwa service zinazohitajika haiwezi kuwa mkweche.

Mimi kwa mfano nina Landrover imetembeaa km 954k mpaka nnavyoandika na bado sio mkweche
 
Ingawa km sio kipimo pekee cha uzee au uchakavu wa gari, as kama linapata matunzo mazuri na services muda muafaka gari, linaweza fikisha km mpaka mililion moja na liko vizuri. Ila kama unataka kununua used car from Japan, inashauliwa kuangalia mwaka wa gari na km zilizopo. On average gari hutembea angalau km 10,000 kwa mwaka, so kama lina miaka 10, basi km 100,000 plus. ila ukipata lililo chini ni vizuri zaidi, ila lisiwe chini saana kama km 30,000 kama lina umri mkubwa. Pia lisizidi km 150,000.

Kwa European cars, tafuta lenye km chache, maana magari yao yana systems nyingi za umeme. Likitembea km nyingi systems nyingi zinaanza ku fails. So angalau lisizidi km 100,000

Ahsante sana.Elimu safi.
 
Ugharama wa vipuli ndio unanitisha. ....
kabanga ila ukifunga ni uhakika sio kitu cha kuharibika leo au mwakani, after all kama una uwezo wa kumiliki BMW halafu ukashindwa kuikatia comprehensive insurance ni kichekesho
 
Last edited by a moderator:
kabanga ila ukifunga ni uhakika sio kitu cha kuharibika leo au mwakani, after all kama una uwezo wa kumiliki BMW halafu ukashindwa kuikatia comprehensive insurance ni kichekesho
Kabisa, ndio ndoto yangu kumiliki gari, maana kama usafiri upo....
 
Mmh platz ni majanga kuanzia body mpaka injini zinahitaji handle with care kama hujachukua achana nayo

Mkuu jamaa wanasema hizi honda zinasumbua spea halafu zikichoka "zinachoka vibaya sana".. vipi fuel consumption?
Kuna ndugu yangu ana platz anaisifia sana.. anapiga nayo masafa nairobi - dar , anasema iko poa... hapo mnanichanganya kiasi..
 
Unajua kila mtu ana uzoefu wake inategemea yeye ana Platz model gani,lakini kwa ninazozifahamu mimi sikushauri

Honda nazo zipo ambazo ni vimeo hasa lakini kwa mfano ukipata RD5 ni gari nzuri mno, hata RD 1 pia kuna mdau kavuta moja hapahapa jukwaani baada ya kushauriana anaweza kuwa shuhuda mzuri

BTW gari yeyote ni matunzo, hata upate gari ngumu vp kama itakosa matunzo tarajia kifo cha mapema tu
 
Kuna vigezo vingi zinapaswa kuangaliwa kabla ya kusema gari ni mkweche ama la kwa kutumia kigezo cha km.
Mathalani ukubwa wa injini.Landcruiser yenye km 150k ni tofauti na Vitz yenye km 150k ama pikipiki.

Lakini vile vile suala la service ni muhimu.Gari inayofanyiwa service zinazohitajika haiwezi kuwa mkweche.

Mimi kwa mfano nina Landrover imetembeaa km 954k mpaka nnavyoandika na bado sio mkweche

Sure, hizi gari zenye cc 650, 900, 1200 au hat 1500 ikiwa na km 70000 huenda ni sawa na gari yenye cc2700 yenye km 150,000! Hii ni sawa umtembeze mtoto wa miaka 10 kwa umbali wa km 50, na useme ni sawa na mtu wa miaka 20 atembee the same distance. Mtoto wa miaka 10 lazima achoke mapema, hivyo huenda km zake 30 tu ni sawa na kuchoka kwa km50 kwa mtu wa miaka20
 
kabanga ila ukifunga ni uhakika sio kitu cha kuharibika leo au mwakani, after all kama una uwezo wa kumiliki BMW halafu ukashindwa kuikatia comprehensive insurance ni kichekesho

Kwani sedan bmw model ya 2005 au 2006 ni bei gani
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom