Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Asante sana Mkuu, nimekupata.
Hapa basi itabidi nijitayarishe na kama milioni sita hivi Duuh! Hii gari naona sasa imeniwia gharama kubwa sio jinsi nilivyotegemea...nilidhani ni kagari kadogo engine 0.66 basi itakuwa nafuu. Sasa naelewa kwanini watu huwa wanaacha magari yao Bandarini



Hilo gari, kama ungelinunua kwa $3217 (custom value CIF) au chini ya hapo, basi ushuru ungelipa 4.33mil. Lakini kwakuwa CIF yake ni zaidi ya $3217, TRA watatumia hiyo CIF yako ya $4100, tegemea ongezeko kubwa tu la ushuru, huenda likazidi 1mil kwenye huo ushuru wa 4.33mil. TRA watafanya kadirio la ushuru upya kwa kutumia CIF yako na wao ndio watajua ni kiasi gani, huwezi pata hiyo details kwenye web yao. Pia ongeza kama 1mil nyingine kwa ajili ya kufanya clearance na kulipia bima ("chenji" huenda ikabaki).
 
HONDA HR-V

Naomba kuulizia uwezo wa hii gari katika kusafiri masafa ya mbali maana nimevutiwa na ulaji wa mafuta(1.6L ingine size) pia bei yake si mbaya (mfano gari ya mwaka 2000 inauzwa kwa FOB -2000 USD.) Zaidi ina umbo/size kubwa ukilinganisha na magari mengine yenye ingine size hiyo(1.6L).

Zaidi naomba nijuzwe upatikanaji wa spare za hii gari na bei ya hizo spare zake.....


Nashukuru na Karibuni.
 
Wakuu hivi ni muda gani gari inatakiwa kukaa bandari kabla haijalipiwa ushuru? je ni wakati gani mugaziaji atapigwa penalt?
 
Wakuu hivi ni muda gani gari inatakiwa kukaa bandari kabla haijalipiwa ushuru? je ni wakati gani mugaziaji atapigwa penalt?

Haitakiwi kuzidi siku 7. Ndani ya siku 7 inabidi iwe imelipiwa ushuru na tozo nyingine zote ili itoke.
 
Habari wataalam, Naomba mwenye uelewa wa haya magari TOYOTA CELICA (Hasa ya kuanzia mwaka 2000) anipe uzoefu, inaonekana ni mazuri ila sijui spea zinapatikana au la, bei za spea juu au kawaida, tatizo la ujumla, na mengine mengi.
Nimeuliza hivi kwa vile nimeanza kuona yanaongezeka hapa Dar si kama miaka ya nyuma.

Natanguliza shukrani.
 
wadau natafuta cresta gx 100 ,iwe katika hali nzuri vitu kama AC ifanye kazi.iwe na uwezo wa kutoka dar hadi mombasa. bajeti yangu m 6. please please please mi mwenyewe mtoto wa mjini gari famba staki tusipotezeane muda na magari mabovu

Mkuu hiyo gari ipo hapa Dar es salaam,so kama bado haujapata na uko interested naomba tuwasiliane
 
Wakuu salaam!

Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumiliki kausafiri nina funcargo, ila siku za hivi karibuni kuna tatizo ambalo limeanza kusumbua gari langu.Iko hivi gari linapokuwa limepaki na liko ON nikiwasha tu AC huzima, ila nikiliwasha tena na nikawasha AC kuna mawili, AC inaweza ikafanya kazi kama kawaida lakini wakati mwingine bado litazima tena.Ila likiwa kwenye mwendo na nikawasha AC tatizi hili hutokea kwa nadra sana, yaani AC hufanya kazi kama kawaida.Kwa kuongezea nikiswitch tu AC on ghafla kuna mlio wa engine ambao si wa kawaida huibuka (yaani inakuwa kama vile engine inasitasita kufanya kazi au ni kama vile inachezacheza like umeme wa majumbani unavyochezacheza na time hiyo hata dash board huwakawaka na kuzimazima) ni kama vile engine inajaribu kupambana na mzigo mzito ambao inakuwa imetwishwa ghafla kwa AC kuwa on ! vile vile taa ya cheki engine huwaka ingawa baadae huzima.

Naomba kwa anayeelewa anieleweshe hasa tatizo laweza kuwa nini, maana mafundi kadhaa nilioongea nao kila mtu anakuja na la kwake!

Napenda angalau kuwa na clue/idea maana kibongobongo mafundi wengine si waaminifu wanaweza kula pesa zangu ilihali tatizo laendelea kama kawa.

Nashukuru sana kwa mawazo mbalimbali yatakayojitokeza
 
Lazma utakua mwanamama,, duh maana kwa maelezo yako nazan hakuna mwanaume anaweza kuja jf kuomba ushauri wa jambo kama lako.any way lazima pump ya ac itakua mbovu bearing zake na hvyo kusababisha kuwa ngumu,nenda kwa fundi mwambie aitolee beriti na ajaribu kuizungusha kwa mkono lazma atagundua tatizo....duh!

Umemfanyia unfair profiling....hilo tatizo halielezei jinsia yake
 
Lazma utakua mwanamama,, duh maana kwa maelezo yako nazan hakuna mwanaume anaweza kuja jf kuomba ushauri wa jambo kama lako.any way lazima pump ya ac itakua mbovu bearing zake na hvyo kusababisha kuwa ngumu,nenda kwa fundi mwambie aitolee beriti na ajaribu kuizungusha kwa mkono lazma atagundua tatizo....duh!

Si haki kwa ushauri wenye attack ndani yake,
Humkumtendea uungwana,ushauri huu inatuhusu wote, jukwaa ni kubwa tuvumiliane kwa yote
 
Lazma utakua mwanamama,, duh maana kwa maelezo yako nazan hakuna mwanaume anaweza kuja jf kuomba ushauri wa jambo kama lako.any way lazima pump ya ac itakua mbovu bearing zake na hvyo kusababisha kuwa ngumu,nenda kwa fundi mwambie aitolee beriti na ajaribu kuizungusha kwa mkono lazma atagundua tatizo....duh!

Nadhani hujajibu swali kistaarabu nimefuatilia uzi huu tangu mwanzo watu wengi wamesaidiwa sana na tumejifunza mengi sijawahi kuona majibu ya shombo kama uliyotoa. Lazima ujue hakuna mtu aliyezaliwa anajua watu tunajifunza taratibu.

Mghosi
 
jamani naizimia sana corola sprinter hebu wajuzi wa hii gari semeni kitu kabla sijajiingiza
 
Habar zenu wakuu, napenda kutoa shukran zangu za dhati kwa kuanzisha hii thread ya magari, Pia ningependa kuuliza swali na pia kupata ushauri. Nina kagari changu toyota duet ina tatizo la kupandisha temperature kila baada ya umbali fulan, ilianza kunitokea mara ya kwanza gari ikachemsha nikaiwahi nikaipaki kwa muda then nikaweka maji ikawa fresh ila ikaja tatizo fan ya pale kweny rejeta haizunguk bahat nzuri kuna jamaa mmoja anaujuz kidogo akachomoa wire ya fan ikaanza kuzunguka nikafika nilipokua naenda nikarudi nikapeleka kwa fund wakasema wanaiunga direct kama mwezi umeshapita juzi kati tatizo limeanza tena temperature kupanda nikampelekea akaangalia tukatest akasema haina shida kwamba fan ilishindwa tu kuwaka but haitachamsha kuenda baada kama uya 25 km ikaanza kuandisha temper nikampata fundi akarekeibisha akasema kuna kitu huwa kinalock kinafanya maji yasiingie kwenye engine so akarekebisha then akadisconnect wire unaofanya gauge inasoma. Swali langu je tatizo la gari ni nini hasa coz kila fundi anakuja na idea yake? Na linatatuliwaje wanajf wenzangu? Natanguliza shukrani
 
Mkuu Mshana jn niko na Toyota premio d4. Nimetumia Gari hii kwa muda mrefu bila tatizo lakini sasa ghafla imeanza kupoteza nguvu kwenye mlima inajikongoja na kuchanganya inachelewa na nikikimbia Gari inastukastuka hata speed 90 haifiki inamis na sometime inazima ukiiwasha haitaki ila ikikaa muda kiasi inakubali kuwaka.nimebadiki hydraulic kwenye gearbox kwa kudhani labda imechoka lakini tatizo bado. Tatizo laweza kuwa nini mkuu?
 
Back
Top Bottom