CLES B
JF-Expert Member
- Jul 7, 2013
- 733
- 458
Mkuu Mshana jn niko na Toyota premio d4. Nimetumia Gari hii kwa muda mrefu bila tatizo lakini sasa ghafla imeanza kupoteza nguvu kwenye mlima inajikongoja na kuchanganya inachelewa na nikikimbia Gari inastukastuka hata speed 90 haifiki inamis na sometime inazima ukiiwasha haitaki ila ikikaa muda kiasi inakubali kuwaka.nimebadiki hydraulic kwenye gearbox kwa kudhani labda imechoka lakini tatizo bado. Tatizo laweza kuwa nini mkuu?
Kwa uzoefu wangu mdogo wa magari nimeishakutana na watu 2 walio na magari yenye engine za D4 mafundi wengi wengi wamekuwa wakisema D4 ni kimeo ingawa bado sipata strong point ubovu wake ni upi.Kifupi mafundi wengi D4 zinawatoa kamasi...Next time check for 7A engine kama bado una prefer Premio.