Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Asante sana mkuu kwa majibu mahususi, sasa kidogo mwanga umeanza kuonekana mbele....
Clearing agent wangu ananidai ati USD 200 kwa gharama za Delivery order??? wakati ka gari kenyewe ni kadogo kwa engine 0.66litres.
Halafu ati handling charges kachanganya na storage charges....hivi kwa ka gari kadogo handling charges zinaweza kuwa kiasi gani?
Ingawa gari ilishakuwa inspected japan na kupitishwa ati hapa tena kuna gharama za TBS (tsh 25,000) yaani !!
ndio maana mkuu nakuja na maswali mengi namna hii
Shukran!

Futota,ni shughuli hasa espcly issue ya kodi nyingi gari yako ikifika...japo kwa ufupi...D/O ni paper itakayoruhusu mzigo wako kuwa released kutoka kwa shipper/dealer na kuhakiki kwamba mali imefika salama,...handling charges na d/o ni tofauti kama vinavyojieleza,hata hivyo visikupe tabu agent wako atadeal navyo muhimu ujue exact price ya kila service asije akakupiga! Kuhusu handling charges TPA ndo wanahusika nayo huwa wanatoa cargo service invoice ambayo humo utaona muda wako wa neema I.e grace period 7 days kwa gari yako kukaa kwenye yard za bandari kama gari yako ni suv inarange kati ya usd 150 /250 may be itategemea ni gari gani though! ......handling charges baada ya grace period kuisha muulize agent atakuambia ni ngumu kupata exact figure ya bei hapa but it's probably more than 5,000/_ / day...Gharama za ukaguzi wa tbs zipo ilipaswa uzilipe kwa dealer huko ulikonunulia kama ni Japan tbs wanafanya certification hukohuko na kukagua various issues ikiwemo mileage na road worthiness,likifika huku halijakaguliwa possibility ya gharama kuwa juu ni kubwa ukizingatia madafu cash yetu na penalties za tbs kwa kuimport gari isiyokaguliwa! .....sina uhakika na normal charge za inspection bila shaka haivuki $80 ...japo kwa ufupi ila bei halisi muulize agent,au laah! Tinga tra,tpa upate hakikisho la exact price agents wengine njaa kali hawachelewi kukupiga za uso...nikutakie mafanikio
 
Ndugu futota je nikupe agent wangu wangu, kama yawezekana. But kama nilivosema port charges na clearing estimation budget ni $800 na ni lazima akuletee risiti zote tena tra na hapo Kuna chenji nyingi sana inabaki.. Call me ukiwa wataka msaada zaidi au njoo quality Center
 
Asante sana mkuu kwa majibu mahususi, sasa kidogo mwanga umeanza kuonekana mbele....
Clearing agent wangu ananidai ati USD 200 kwa gharama za Delivery order??? wakati ka gari kenyewe ni kadogo kwa engine 0.66litres.
Halafu ati handling charges kachanganya na storage charges....hivi kwa ka gari kadogo handling charges zinaweza kuwa kiasi gani?
Ingawa gari ilishakuwa inspected japan na kupitishwa ati hapa tena kuna gharama za TBS (tsh 25,000) yaani !!
ndio maana mkuu nakuja na maswali mengi namna hii
Shukran!

Hizo Gharama kuanzia namba mbili ndio nilizitumia wakati natoa Gari yangu Bandarini ilikuwa ni trh 04.09.14 ndio lilitoka,sikulipa zaidi ya hapo.Labda Sijui kama mambo yamebadilika sasa hv.
 
Attachments

  • 1433921381065.jpg
    1433921381065.jpg
    49.7 KB · Views: 342
Shukrani mkuu, maana clearing agent anakuja na mabei naona anataka niliache gari bandarini.

Hizo Gharama kuanzia namba mbili ndio nilizitumia wakati natoa Gari yangu Bandarini ilikuwa ni trh 04.09.14 ndio lilitoka,sikulipa zaidi ya hapo.Labda Sijui kama mambo yamebadilika sasa hv.
 
Mkuu Barbados kwa heshima na taadhima hiyo sio lugha yetu hapa kwen huu uzi. Please usimdharau usiyemjua. Kuwa na uwezo na kujua ABC za gari ni vitu viwili tofauti. Huenda huyu ni daktari bingwa...

Cc mshana jr RRONDO Preta

asante sana mkuu kwa utetzi. hata kama ningekua nauza mkaa sio sababu ya kunidharau.
 
Last edited by a moderator:
Toyota harrier inaonyesha engine check light na kuishiwa nguvu wakati wa kuanza safari. Tatizo ni nini na gharama za vifaa na ufundi.
 
Asante mkuu mshana jr kwa mafunzo na kuelewesha jamii kwa upana juu ya mambo ya magari. Samahani kama wsali hili litakua limeshaulizwa hapo awali.
Uimara na ulaji wa mafuta wa RAV J engine ya 3s- Fe upoje?
 
Jamani kwa wenye uzoefu wa Nissan xtrail na Serena natamani sana kununua mojawapo
 
Mavado natamani kununua xtrail au serena, nipe uzoefu wako kwa ubora na weaknesses zake
 
Asante mkuu mshana jr kwa mafunzo na kuelewesha jamii kwa upana juu ya mambo ya magari. Samahani kama wsali hili litakua limeshaulizwa hapo awali.
Uimara na ulaji wa mafuta wa RAV J engine ya 3s- Fe upoje?

Aisee hizi gari zilipendwa sana hapo nyuma ni imara kiasi chake shida ni fuel consumption iko juu kiasi
 
Toyota harrier inaonyesha engine check light na kuishiwa nguvu wakati wa kuanza safari. Tatizo ni nini na gharama za vifaa na ufundi.

Angalia kama timing belt imeshafikisha km laki 1, basi jua Unatakiwa kubadili haraka zipo za elfu 30-laki1 nafikiri
 
Nenda kaangalie miguu (matairi), huenda ndo kuna tatizo, kuna kidude fulan hivi kimefungwa hapo mafundi wanakijua. Chukua fundi makenika afungue tairi then fundi umeme akikague hicho kidude. Ikishindikana ndio upige diagnosis.
-

Thanks kaka. Tumeangalia miguu, brake pad moja iliisha na kuharibu disc. Kuna cylinder pale pia ikawa inavujisha mafuta. Nime change pads zote. Wamefunga iko safi.
 
Mshana jr naomba kujua ubora na udhaifu wa serena na extrail plz
 
Mshana jr naomba kujua ubora na udhaifu wa serena na extrail plz

X-trail niliwahi kuzisifia kwa uzoefu wangu lakini nikaja kugundua kuwa hapo Nissan alichemka hata Serena pia but all in all gari ni utunzaji
 
Toyota harrier inaonyesha engine check light na kuishiwa nguvu wakati wa kuanza safari. Tatizo ni nini na gharama za vifaa na ufundi.

Ya mwaka gani kiongozi? Basically unatakiwa upeleke kwa wanaofanya diagnosis wajue tatizo hasa liko wapi usipeleke kwa mafundi wa mtaani. Gharama za vifaa na ufundi itategemea na tatizo watakalogundua. All the best
 
Asante kwa majibu but natamani kujua udhaifu wake nipime kama naweza kuumudu
 
Aisee hizi gari zilipendwa sana hapo nyuma ni imara kiasi chake shida ni fuel consumption iko juu kiasi
Ok asante sana mkuu kwa jawabu hili. Lakini naziona nyingi sana mtaani, kwa haraka haraka lita moja inaweza kwenda kwa km ngapi? Na je ni tofauti na Rav 4 L katika ulaji wa mafuta?
 
mshana jr au mwingine mwenye uzoefu nataka kuagiza raum, ila watu wanasema old model ni imara kuliko new model, please mwenye kujua haya magari vizuri, na matatizo yake,
 
Ok asante sana mkuu kwa jawabu hili. Lakini naziona nyingi sana mtaani, kwa haraka haraka lita moja inaweza kwenda kwa km ngapi? Na je ni tofauti na Rav 4 L katika ulaji wa mafuta?

Utofauti siujui sana niwe tu mkweli katika hili ila fuel consumption inarange km 8-10 kwa litre moja
 
Back
Top Bottom