Mgagaa na Upwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 13,481
- 28,116
Chukua halafu nawe iweke sokoni usiitumie zaidi ya mwaka kwa ushauri wangu ni heri upate Daihatsu kid Duet corolla au Ti yani hizi za misele ya kawaida
Ahsante sana na ubarikiwe mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chukua halafu nawe iweke sokoni usiitumie zaidi ya mwaka kwa ushauri wangu ni heri upate Daihatsu kid Duet corolla au Ti yani hizi za misele ya kawaida
UMEWAHI KUKAMATWA NA POLISI BARABARANI?
Je, umewahi kukamatwa na polisi wakati ukiendesha gari, pikipiki au baiskeli?
zijue haki na wajibu wako !
Bila kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani kutakuwa na vurugu katika barabara zetu.
Soma na ujifunze kanuni, Sheria Mpya za Barabara iwapo kila mmoja atazifuata sote tutafika tunapokwenda kwa urahisi na usalama zaidi. Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana ya kutekeleza sheria. Lazima kushirikiana nao, isipokuwa kama wanatenda kinyume na sheria.
Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati gani anakusimamisha uwapo barabarani.
Mamlaka ya kusimamisha gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako kama atakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani pia anaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).
Leseni ya kuendesha gari:
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari anaweza kukataa fotokopi hata hivyo, unaweza kuamua kupeleka leseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa. Ili kuepuka matatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).
Hati ya usajili:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili gari lazima liendane na maelezo ya kwenye kibandiko, lakini vitu vidogo kama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).
Leseni ya barabarani, na bima ya gari:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani na kibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).
Kunyanganywa:
Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.
Mikanda ya kiti ya usalama:
Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe inatembea au imesimama) unatenda kosa kama unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote wafunge mikanda.
Kuendesha baada ya kunywa pombe:
Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi cha pombe kwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatia ya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).
Kutumia simu ya mkononi wakati unaendesha:
Ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la kuendesha kwa uzembe (RTA, s.42, s. 50).
Mwendo kasi:
Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa Ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) ofisa wa polisi anaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unaweza kupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73 (2)).
Kustahili kuwepo barabarani:
Ofisa WA polisi ana haki ya kukagua Kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri unawezakutakiwa kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.
KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA: Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 20,000 kwa ofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezo kwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na nyote wawili mtatia saini kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu iliyotiwa saini. Unaweza kwenda Na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIA YOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisi anakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishi kwa Ofisa Msimamizi Mkuu ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu usitoe rushwa na usipokee rushwa.
Unaweza ukapenda kukata maelezo haya na kuyaweka kwenye gari lako lakini kumbuka kwamba ni mwongozo tu.
Ukitaka hii Gari, tembelea Autocom Japan used car exporter QUALITY Center, Nyerere Road Dar es salaam almaarufu kama uchumi supermarket or  0767328063 for more information.
Imara sana ila fuel consumption iko juu kiasi si sawa na passo
Wadau naomba kufahamishwa kuhusu ubora na uimara au matatizo ya Toyota Cami kwa wanaojua tafadhali nijuzeni. Nataka kuagiza soon but nimeona niulize kwanza.
Habari za muda huu wadau, natalajia kupata usafiri wakutembele hv punde (gali) aina ya gxmia cresta VP kwa uhimara wa aina hyo?
Mkuu dunia ya leo huwezi fanya biashara bila kuwa na website.....ni ngumu sana. Unless you have a specific focus group of clients you are targeting.
Habari za muda huu wadau, natalajia kupata usafiri wakutembele hv punde (gali) aina ya gxmia cresta VP kwa uhimara wa aina hyo?
Kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na Uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.
Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.
Kwa Uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake
Karibuni sana
Mtoa mada umefanya vema, ngoja niwe around nipate kujua zaidi kuhusu hii model ya Honda CRV hapa Tz hasa kuhusu kuitunza kwake inakuaje. Kikubwa ningependa kujua garage zake za uhakika tukichilia zile kubwa kubwa.
Pia sio mbaya waliowahi kumiliki wakatueleza kuhusu matatizo yanayowakumba mara kwa mara.
Mimi napenda gari lenye possibility ya seat 7. Wataalamu wa magari mnisaidie gari zuri in terms of fuel consumption, availability of spears and maintenance na comfort ability. Nimepekua nikakutana na haya:
Toyota Avanza,
Toyota Passo Sette,
Toyota Spacio Corolla,
Toyota Wish,
Toyota Noah, Voxy
Naombeni msaada.