Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Sikushauri ununue Vista kwa bei hiyo.

Asante sana mkuu, na mshana jr na kwa kunifungua macho....kati ya vista na Carina ti nichukue ipi? Intention yangu ilikuwa ni ti sasa nimekutana na vista anapiga bei hiyo....
 
Pls to my personal advice achana nayo tafuta group ya madalali wa magari kuna magari mengi Mazuri kwa bei poa sana

Napataje group ya madalali mkuu, nisaidie plz. Mawazo yangu nimvue mtu carina ti, sprinter au sasa ndo nimeanza kutamani pia vista baada ya kuiona kwa mtu.
 
Napenda kuuliza, natumia gari aina ya corona injini 5A, injini imeshachoka je! ni bora kufanya kipi, ovaholi au kununua injini nyingine? Na gharama inakuwaje kununu injini coz overall fundi ameniambia nitafute kama laki 7

Nunua used block engine nyingine (kifupi namaanisha half engine kutoka Japan)mjomba wala haizidi laki 8 then makandokando kama self..stering power na distributor unatumia zile zile..ukifunga au unavyosema 'overhauling' maisha kwa hizo engine ndogo ni mafupi hazichelewi kukurejesha kwenye gharama utakazozikwepa.Overhaul iko poa kwa engine kubwa. Achana na ushauri wa fundi wako huyo na kanunue 'used block engine' utakuwa uko katika 'safe side'
 
Asante sana mkuu, na mshana jr na kwa kunifungua macho....kati ya vista na Carina ti nichukue ipi? Intention yangu ilikuwa ni ti sasa nimekutana na vista anapiga bei hiyo....

Carina ni gari ya kisasa na ipo sokoni kwa biashara na kwa private.Vista mpaka upate mstaafu aliyelipwa mi noti kibao utakapoamua kuiuza ,na vista nyingi engine zake ni D4 ambazo mafundi wengi hawazijui.Kwa uoga wa watu wengi na engine za D4 unaweza kukumbana na changamoto nyingi usoni kwa kwenye suala la kuiuza na pia service. Chukua Carina TI.
 
Asante mkuu,
 
wakuu nina Toyota Surf ilikuwa ina injini ya 2LT imekufa sasa ninataka kufunga injini ya 1KZ na gearbox automatic, naomba ushauri wakuu, pia vipi kuhusu upatikanaji wa used engine ya 1KZ.....?!
 
Kama gari yako unatumia mjini tu na kwa nadra safari ndefu huna haja ya kuitoa. Ila kama unasafiri safari ndefu mara kwa mara nakushauri uitoe kwani madhara yake ni makubwa, unaweza hata kupasua rejeta, n.k

sio kweli mkuu hiyo kitu haitakiwi kutolewa kabisa mkuu hutakiwi kuitoa.hilo suala la sijui kupasua rejeta ukiona Gari inafanya hivyo ujue inamatatizo mengine .

na wengi thermostert zikiwa zinakaribia kufa au zikianza kufa au kufa kabisa huwa hawaelewi.lakini wakikutana na mwenye ujuzi kidogo akimwambia aitoe na akiitoa Gari ikiwa fresh basi kila Gari ikija kwake au ushauri atakao utoa ni kuitoa tuu.

yaani ni sawa sawa na kuwa engine za D4 mbovu.watu wanaongea ukimuuliza ubovu wake hajui atakwambia ooo hazitengenezeki
 
Sikushauri ununue Vista kwa bei hiyo.

hahaha bila shaka ushauri huo umeutoa kwa kuwa vista ni D4 lakini angeniuliza mm au ukiniuliza juu ya engine ya D4 huwa zimung'unyi hata neno moja nitakwambia tu ichukue inafaa sana na ni engine yenye technologia ya kisasa zaidi low consumption of fuel more power low emmision n.k

kama huto jali naomba unambie why asichukue vista utoe sababu na suala la D4 liweke pembeni
 
Carina ni gari ya kisasa na ipo sokoni kwa biashara na kwa private.Vista mpaka upate mstaafu aliyelipwa mi noti kibao utakapoamua kuiuza ,na vista nyingi engine zake ni D4 ambazo mafundi wengi hawazijui.Kwa uoga wa watu wengi na engine za D4 unaweza kukumbana na changamoto nyingi usoni kwa kwenye suala la kuiuza na pia service. Chukua Carina TI.

hahahaha mkuu umenichekesha sana aisee Carina ni Gari ya kisasa ina usasa gani mkuu?? yaani uifananishe Carina TI na vista???

in short vista ndio Gari ya kisasa zaidi mkuu ndio maana hata wewe unasema mafundi wake sio wengi na wengi bado hawajajua kuzitengeneza.
acheni kuwapotosha watu wewe yaonekana ni m1 wapo na kama ni fundi au ungekuwa fundi basi ungedondokea group hilo LA mafundi waogopa d4.

ila sijajua usasa wa Gari nyie mwaupima vipi.

Hembu angalia hiyo Carina ti na vista halafu jiulize IPI ni ya kisasa zaidi.maana technologia ya mwisho ya mzungu ni d4 sasa hapo sijui utasemaje
 
wakuu nina Toyota Surf ilikuwa ina injini ya 2LT imekufa sasa ninataka kufunga injini ya 1KZ na gearbox automatic, naomba ushauri wakuu, pia vipi kuhusu upatikanaji wa used engine ya 1KZ.....?!

mkuu kwani hiyo Gari ulikuwa na engine ya 2lt na gearbox ya aina gani manual or automatic?

kama ni automatic hauna haja ya kubadili gearbox ww nunua engine tuu ya 1kz gearbox tumia ileile.
kuhusu suala la spea za 1kz mkuu usiulize zipo nyingi sana mpaka utakimbia we.maana tz ndio dampo la toyota
 
sio kweli mkuu hiyo kitu haitakiwi kutolewa kabisa mkuu hutakiwi kuitoa.hilo suala la sijui kupasua rejeta ukiona Gari inafanya hivyo ujue inamatatizo mengine .

na wengi thermostert zikiwa zinakaribia kufa au zikianza kufa au kufa kabisa huwa hawaelewi.lakini wakikutana na mwenye ujuzi kidogo akimwambia aitoe na akiitoa Gari ikiwa fresh basi kila Gari ikija kwake au ushauri atakao utoa ni kuitoa tuu.

yaani ni sawa sawa na kuwa engine za D4 mbovu.watu wanaongea ukimuuliza ubovu wake hajui atakwambia ooo hazitengenezeki

Kwa uzoefu wangu kwa nchi zenye joto,thermostat hufa kwa kuchelewa kufungua njia,ikitokea hii ukiwa uko kwenye safari ndefu msukumo wa water pump husababisha rejeta kupasuka kwani maji hayaruhusiwi kuendelea na mzunguko.

Kama unataka thermostat iendelee kuwepo inakulazimu uwe unaibadilisha mara kwa mara
 
Tuache kykariri, magari yote duniani hutengenezwa kwa ajili ya maeneo husika,kwa kuwa kipato chetu wengi ni cha kuunga unga na hatuna uwezo wa kununua magari mapya kwa mazingira husika ndiyo maana tunanunua magari used. Kwa sababu hiyo inatubidi tupambane na changamoto husika, hata ukienda kwenye seminar za wazalishaji magari watakuambia.

Mfano mzuri angalia wanaonunua mabasi au malori used kutoka kwa nchi za baridi magari yao yanavyochemsha ,solution yake ni kubadilisha rejeta na kuweka rejeta kuwa kwa nchi za joto. Vivyo hivyo kwa gari ndogo lazima ufanye adjustment kulingana na mzingira husika.

Ila kama unanunua gari mpya kwa mazingira husika challenge hii hutoipata kabisa
 
Wakuu naomba kujua ni kwanini tunapowapa mafundi waunge sehemu za vyuma kwenye magari yetu (welding) wanataka gari iwe kwenye silencer "on) au terminal ziwe disconnected?
Najua ni issues za short lakini gari ikiwa silencer inazuia vipi short? mshana jr, Transistor et el!
 
Last edited by a moderator:

Ngoja wenye ujuzi na hili waje
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom