Mkuu Lege naomba msaada wako.
Gar yangu inashida ambayo nimeshindwa kugundua ni kitu gani, kuna muda na muda tena mara chache.
Nikizima kuja kuwasha inazingua mpaka ni boost. Nikahisi terminal haziko nimebadili lakini bado.
Na dalili za kutokea hivyo huwa inaonyesha. Kuna saa kama natembea nimewasha taa mwanga unakuwa una vibrate hata kwenye dashboard inaonyesha mwanga wake hautulii na sterling inakuwa ngumu. Ila nikitembea tembea inapotea.
Na hili tatizo limeanza siku ambayo nili park pale tazara na gari kugoma kuwaka mpaka nikamuita fundi wangu anitolee sterling lock ili tulitoe maeneo hayo kwasababu walituambia watu pale kuwa key less car zinasumbua kuwaka maeneo ya Tazara mpaka zitoke hapo.
Na kweli tulitoka pale hadi tmk na tulipo washa gari ikawaka na fundi kurudishia ile lock. Lakini tatizo likaanza siku hyo hyo mara sterling kuwa ngumu saa nyingine mara zikizma kusumbua kuwaka.
Sasa inanipa tabu kiongozi. Msaada wako naamini utakuwa ushakutana na shida kama hizi.
Natanguliza shukrani mkuu Lege.