Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

BAADA ya kuosha engine ya GARI yangu (NISSAN),DASHBOARD HAIWAKI TAA (P,R,N,D &L),PIA GARI INAJIRESI NA HAINA NGUVU ,TAFADHALI WATAALAM KWA MSAADA!
 
BAADA ya kuosha engine ya GARI yangu (NISSAN),DASHBOARD HAIWAKI TAA (P,R,N,D &L),PIA GARI INAJIRESI NA HAINA NGUVU ,TAFADHALI WATAALAM KWA MSAADA!
Magari ya Automatic hayapatani sana na maji kwakuwa mfumo wake mzima ni umeme, hivyo kuna sehemu maji yameingia ambapo kuna connection za
distrbutor/ignition module au plugs na coil au ECU. Nibora kukabidhi gari mapema kwa fundi akuondolee hizo hitilafu.
 
Habari za mchana wakuu. Gari aina ya Noah breki IPO chini kabisaa, fundi akaniambia nibadilishe breki. Nikaweka zote mpya ila ndo kwanza breki imepotea. Baada ya kuangaliwa zaidi fudi kaniambia booster ya breki ina shida kwani inaruhusu upepo itoke ndani ya gari. Akanishauri ninunue booster na master yake, yaani complete. Akadai ataagiza dar, Tsh laki na 80

OK, je ikiwekwa hiyo booster na master yake nitakuwa nimetatua tatizo???
 
Aerial ya gari ili isiibiwe kirahisi (iko nyuma juu ya gari) nifanyeje? Aina ya gari TOYOTO SALOON WISH.
 
Msaada wenu wakuu, nina gari IST (1NZ-FE engine) ilianzisha tatizo la engine kupiga kelele na taa ya oil kuwaka wakati gari ikiwa inaendeshwa. Nikaenda kwa fundi akasema labda oil filter itakuwa mbovu, hivyo akabadilisha oil na oil filter, lakin baada ya siku mbili tatizo likarudi tena. Fundi akasema itakuwa ni oil pump haisukumi oil ya kutosha ndio maana gari inapiga kelele. Tumebadilisha na kuweka oil pump mpya lakin tatizo liko palepale na kelele nahisi ndio kama zimezidi. Shida inaweza kuwa nini? au kama kuna fundi anaweza tatua tatizo nitashukuru, niko Mwanza.
 
ushauri wangu ununue injine nyingine maana utapata usumbufu usio wa lazima. kumbuka injini ni kama laki 7 tu lakini ukianza kukatengeneza utajikuta imezidi laki 7 hakajapona
 
Wanajukwaa....nahitaji show ya mbele ya honda fit nyeusi....mwongozo tafadhali....niko dsm.
 
Back
Top Bottom