Mada maalum ya ndege toka FB

Hii sio Taswira nzuri kwenu Air Tanzania
 
Kinachorudi nyuma ni ndege au mzunguko wa injini?
 
Your browser is not able to display this video.
 
Nimekuwa nikisoma zaidi habari za Ndege hii iliyotengenezwa Tanzania. Nimekubali imetengenezwa Tanzania. Bado sijapata jibu kama imetengenezwa na Watanzania, na endapo utaalamu na teknolojia iliyotumika ipo mikononi mwa Watanzania. Naomba kujua.
Nawasilisha!
 
Kampuni kubwa ya kutengeneza Ndege ya Embraer, imetangaza mpango wake mpya wa kutengeneza ndege ya kwanza ya Abiria inayotumia akili bandia (AI) kujiendesha ambayo haitokuwa ikiendeshwa na Rubani katika safari zake zote.

Mpango huo umezinduliwa katika hafla ya Jumuiya ya Kitaifa ya Usafiri wa Anga na Biashara huko Orlando, Florida Nchini Marekani ambapo Ndege hiyo haitokuwa na chumba cha Marubani kama ilivyozoeleka kwenye Ndege tulizonazo sasa na badala yake itakuwa na chumba kama sebule ndogo ambacho Abiria wanaweza kukaa na ku-njoy maisha wakiwa angani ( kama inavyoonekana kwenye picha ).

Madirisha ya Ndege hiyo iliyopewa jina la ‘Ndege ya siku zijazo’ yatakuwa madirisha ya kipekee kwani yatakuwa na ‘touch screen’ ili kumuwezesha Abiria kupata urahisi wa kufanikisha hitaji lake lolote kwa wakati wowote.

Haya ni maono tu ambayo ndio kwanza yametangazwa na Kampuni hii ambayo inashika namba tatu kwa utengenezaji wa Ndege Duniani baada ya Boeing na Airbus, ni maono ambayo yamekuja wakati huu ambao tayari Dunia inashuhudia Magari yanayojiendesha yenyewe yakiwa barabarani huko Marekani na kufanya shughuli za kila siku zikiwemo TAXI za kubebea abiria huko San Francisco, tazama picha zaidi hapa instagram.com/p/DA1T9pUiTjh/…
 
Shirika la Ndege la Air France limesitisha safari nyingine za ndege katika Bahari Nyekundu, baada ya Rubani kuona "Kitu Kinang'aa" katika Urefu wa Juu mapema leo wakati wa Safari ya Kawaida. Kitu hicho kinaaminika kuwa kilikuwa ni Kombora la Ballisti lililorushwa na Houthis nchini Yemen, huku Ndege kadhaa zikielekezwa Kwengwa au Kuelekezwa Kwingine kufuatia Tukio hilo.

 
Ripoti ya uchunguzi imehitimisha kuwa nahodha wa ndege aina ya ATR 72-600 ya shirika la ndege la Binter Canarias alifunga breki ya kuegesha ndege wakati ikiwa angani kwa sababu ilikuwa inazuia mwonekano wa picha aliyokuwa akijaribu kupiga.

Marubani hao walisahau kuachia breki kabla ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Las Palmas, Uhispania, na kusababisha uharibifu wa matairi na ringi mnamo tarehe 9 Agosti 2023.

Ndege ya Binter Canarias NT501, ATR 72-600, ilitua kwenye njia ya 03L kwenye Uwanja wa Ndege wa Las Palmas de Gran Canaria (LPA) ikiwa kwenye breki ya maegesho na kupasua tairi na ringi.

Ripoti inasema, wakiwa usawa wa futi 8000, marubani wa ndege walianza kupiga picha kwenye chumba cha marubani na katika kinasa sauti cha chumba cha marubani, nahodha alisikika akisema, "Sitaki hiyo ionekane kwenye picha"

Baada ya kufunga breki hiyo, walisahau kufungua na kusalia hadi wakati wa kutua, na kwa bahati nzuti hakukuwa na ripoti ya majeruhi katika tukio hilo.

Chanzo;
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…