NDEGE MPYA YA KIJESHI URUSI YAANGUKA NA KUUA WATATU
***
Kama ulipitwa kutazama A to Z kuhusu uzamiaji ndege, hatari, vifo pamoja na uchambuzi mdogo kuhusu ndege ya Boeing C17 Globemaster-iii kupitia video, bofya link ifuatayo:
***
Ndege mpya ya kijeshi ya Urusi #Ilyushin Il-112V imeonekana kuwaka moto injini ya kulia wakati wa majaribio kisha kuanguka karibu na #Moscow Jumanne, vyombo vya habari vya Urusi viliripoti, ikinukuu United Aircraft Corporation.
Ndege hiyo ilikuwa na watu watatu ndani wakati wa ajali.
Taarifa iliyowekwa kwenye Twitter na waundaji wa ndege hiyo #UAC ilisema hakuna aliyenusurika.
Watu hao watatu walikuwa mhandisi wa majaribio ya ndege #NikolaiKhludeyev, rubani wa majaribio #DmitryKomarov, na rubani wa majaribio #NikolaiKuimov, shirika la habari la serikali la Urusi TASS liliripoti.
UAC imesema kuwa itachukua hatua muhimu kusaidia familia za marehemu.
UAC iliwaambia waandishi wa habari Jumanne kwamba moja ya injini za ndege hiyo iliwaka moto, TASS iliripoti.
"Kulingana na taarifa za mwanzo na video iliyonasa mubashara tukio hilo inaonesha ajali ya Il-112V ilitanguliwa na moto kwenye injini ya kulia'.
Ndege hiyo ilianguka ilipokuwa ikikaribia kutua karibu na uwanja wa ndege wa #Kubinka.
Kisha ikalipuka baada ya kupiga chini.
Il-112V ni ndege nyepesi ya usafirishaji wa kijeshi inayotengenezwa na Ilyushin Aviation Complex, ambayo ni sehemu ya United Aircraft Corporation.
Ndege inaweza kubeba hadi tani tano za wa wafanyakazi, silaha, au mizigo mingine.
Ndege hiyo mpya imekusudiwa kuchukua nafasi ya ndege za zamani za Antonov An-26.
Urusi imekuwa ikifanyia kazi ndege hiyo tangu 2014 na ilipaa mara yake ya kwanza mnamo Machi 2019 na bado ipo katika muendelezo majaribio.
Imeripoti,
#Insider