Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

KWA UCHACHE KUHUSU NDEGE YA MAKAMO WA RAIS WA MAREKANI "AIR FORCE TWO"

Makamu wa rais nchini Marekani walianza kusafiri kwa ndege kupitia "Air Force Two" mwaka 1959.

Ndege yeyote inayombeba rais aliye madarakani nchini Marekani huitwa "Air Force One" haijalishi ni ndege aina gani.
Jina la "Air Force Two" linarejea kwa ndege yoyote inayombeba makamu wa rais.

Kwa miaka mingi, ndege kadhaa tofauti zimebeba cheo cha "Air Force Two", zikiwasafirisha makamu wa rais na mara kadhaa wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Marekani na 'Congress' duniani kote.

Ndege inayotumika sana hivi sasa ni C-32, toleo la kijeshi lililogeuzwa kutoka ndege ya abiria #Boeing757-200.
Makamu wa Rais #Kamala #Harris pia hutumia C-32.

Ndege ya C-32/B757 ni ya kipekee kwa kuwa inaweza kuruka umbali mrefu na kutumia njia fupi za kurukia ambazo si rahisi kwa ndege nyingine kubwa. Boeing iliacha kutengeneza B757 mnamo 2005.

C-32, ina kituo cha mawasiliano, chumba cha mkutano, na viti 32 vya waandishi wa habari/maafisa.

Eneo la mbele lina kituo cha mawasiliano, gali, maliwato na viti 10 vya daraja la biashara.

Sehemu ya pili ni chumba cha kulala maalum kwa matumizi ya makamu wa rais, eneo la kubadilisha, maliwato binafsi, mifumo tofauti ya burudani, viti viwili vya daraja la kwanza vinavyozunguka.

Sehemu ya tatu ina kituo cha mkutano na wafanyakazi na viti vinane vya daraja la biashara.

Sehemu ya nyuma ina viti 32, gali, vyoo viwili na kabati.

Ndani kuna Saa ioneshayo saa tofauti kati ya Washington DC na kule aendapo makamo wa rais.

Rais na makamu wa rais hawasafiri pamoja kwa sababu za usalama.

Ndege inayombeba rais wa Marekani kwasasa "Air Force One" hutumia VC-25, ambayo ni Boeing747 maalumu iliyobadilishwa kijeshi.

Pia ipo Boeing747 maarufu E-4B inayojulikana zaidi kama "ndege ya Siku ya Mwisho"/"Doomsday" au "Nightwatch"

E-4B awali iliundwa kubeba Katibu wa Ulinzi na Wakuu, Pamoja wa Wafanyakazi wakati wa shambulio la nyuklia
kwa sababu inaweza kutuma amri ya kurusha silaha za nyuklia ikiwa angani, kutoka maghala ya makombora na nyambizi.

Ndege zote VC-25, C-32 na E4B zinawezwa kujazwa mafuta zikiwa angani.

Chanzo:
#insider
#AirForceMagazine
FB_IMG_1683969777732.jpg
FB_IMG_1683969771360.jpg
 
SALA ANGANI

Nyuma ya ndege ya #Saudia, viti 9 vimeondolewa na badala yake wameweka sehemu ya ibada (swala) ambayo inaweza kutumiw na watu wasiozidi 10 kwa wakati mmoja.

Ingawa katika ulimwengu wa Kiarabu inaruhusiwa kusali wakiwa umeketi kwenye kiti cha ndege, Saudia imeamua kuweka wakfu eneo la kipekee lenye skrini ambayo inawasaidia waumini kujielekeza kuelekea Mecca.

#DatoCurioso
[emoji991]Saudia Airlines
FB_IMG_1683969880978.jpg
FB_IMG_1683969874428.jpg
FB_IMG_1683969868400.jpg
FB_IMG_1683969861230.jpg
 
Timu ya wanasayansi wa Marekani huko New Mexico inawageuza ndege waliokufa kuwa ndege zisizo na rubani maarufu 'Drones' ili kujifunza mbinu za kuruka ambazo zinaweza kusaidia sekta ya usafiri wa anga na utafiti wa ndege hai.

Kwasasa sampuli ya ndege hiyo isiyo na rubani inaweza kuruka kwa muda usiozidi dakika 20, wanasayansi waliambia Reuters.

Mostafa Hassanalian, profesa wa uhandisi wa mitambo anayeongoza mradi huo katika Taasisi ya Madini na Teknolojia ya New Mexico huko Socorro, alisema timu hiyo ilianza kuwachunguza ndege waliokufa baada ya ndege zisizo na rubani kutotoa matokeo mazuri.

Wanasayansi watafanya kazi kutengeneza ndege isiyo na rubani ambayo inaweza kutumia muda mwingi angani na kufanya majaribio kati ya ndege hai

Bofya link hii kwa video:


Kwa Taarifa zaidi:
www.businessinsider.com/american-scientists-turning-dead-birds-into-drones-study-flight-techniques-2023-4%3famp
@reuters
FB_IMG_1683969982174.jpg
 
Picha hii maarufu ya #Concorde ilipigwa mnamo Aprili 1985.
Ndiyo picha pekee ya Concorde kwa karibu ikiwa kwenye kasi inayozidi 2000km/saa (Supersonic speed).

Picha hii ilichukuliwa na #Adrian #Meredith ambaye alikuwa rubani kwenye ndegevita ya Uingereza Tonardo GR4 "Royal Air Force" #RAF wakati akiifukuzia Concorde juu ya Bahari ya #Ireland zaidi ya futi 50,000.

Ilibidi Concorde ipunguze mwendo kutoka mara mbili ya kasi ya sauti Mach 2 hadi Mach 1.5-1.6 ili rubani wa Tornado GR4 wapate urahisi wa kunasa picha.

Hata hivyo Tornado GR4 iliweza kukimbizana na Concord kwa kasi ya 2000km/saa kwa mda wa dakika Nne tu kabla ya kupata ishara ya mshale wa mafuta kuisha huku Concord ikiendelea kubaki kwa kasi hiyo hadi New York.
FB_IMG_1683970092013.jpg
 
KISANDUKU CHEUSI (BLACK BOX)

(Tafsiri nyepesi)

Kisanduku au visanduku vyeusi maarufu kama "Black Boxes au Flight_Recorders") ni vifaa vya umeme katika muundo wa boksi ndogo za chuma ambapo kimoja hunasa sauti ndani ya chumba cha marubani (Cockpit) na kingine huifadhi data za mwenendo wa ndege pindi inapofanya kazi.

Mara nyingi visanduku hivi huwa viwili.

Kisanduku cha kwanza kinanaitwa '#Cockpit_Voice_Recorder {#CVR} ambacho kazi yake kunasa sauti ndani ya chumba cha marubani {#Cockpit)

Cha pili kinaitwa #Flight_Data_Recorder {#FDR} ambacho kinarekodi maelfu ya data za mwenendo wa ndege kama vile, mwendo, uelekeo, kimo, kona, taarifa za '#sensor', ngamizi, mifumo ya ndege na vitu vingine vya kiufundi kinachofanywa katika ndege husika.

Vifaa hivi husaidia kupata taarifa/sababu za uhakika endapo inatokea ajali au tukio la kuhatarisha usalama katika ndege.

Mara nyingi visanduku hivi vinasimikwa ndani ya mkia wa ndege na inatajwa sababu ya kuwekwa katika sehemu hiyo mara nyingi huwa inasalia katika ajali.

Kisanduku cheusi kinatengenezwa na malighafi madhubuti ambayo inaweza kuhimili misukosukokwa asilimia kama vishindo vya kupigiza ardhini (G-force zaidi ya 3000), Hali joto zaidi 1000°C kwa saa Moja au kukaa ndani ya maji kina cha Hadi kilomita 6 kwa siku 30.

Pia ndani vimeundwa na vifaa maalumu vya kuzalisha mawimbi ili kujulisha sehemu vilipo endapo vitakuwa ndani ya kina cha maji cha utefu wa Hadi kilomita 02 "Underwater_Locator_Beacon"

Visanduku hivi huwa vina rangi ya chungwa "#Orange" na sio rangi nyeusi kama vinavyoitwa ili kuweza kuonekana kirahisi pale ajali inapotokea.

Hakuna sababu za uhakika kwanini vifaa hivyo vinaitwa visanduku vyeusi "black box" ila baadhi ya wadau wa usafiri wa anga wanasema jina hilo linatokana na kurekodi matukio ya siri ya chombo na wahusika ambao wengine wanakuwa hawapo hai.

Admin,

#Like & #Share
Aviation Media Tz
Tweeter
Instagram
TikTok
YouTube
FB_IMG_1683970152116.jpg
 
"HAWAVUMI LAKINI WAMO"

"Flight Deck Sailors/Operations" wafyatuaji Manati katika Manoari za kijeshi ambapo watu wengi hawafahamu uwepo wao.

Wadhibiti hawa hujifungia kwenye chumba kidogo cha vioo kilicho chini maarufu "Bubble" ambapo ufyatua manati (Catapult) inayosukuma ndege kwa kasi wakati wa kuruka kutoka kwenye manoari, kwa mfumo wa "Integrated Catapult Control System" kwa kifupi #ICCS kwa kushirikiana na Marshaller nje.
FB_IMG_1683970255281.jpg
 
Pale unaposema "Ndege ni Airbus na Boeing"
Ndege mwenyewe..[emoji23]
FB_IMG_1683973499588.jpg
 
VISAIDIZI VYA NDEGE KUPAA

(Lifting Devices)

UPAAJI NDEGE KWA KIFUPI

Tujikumbushe kuwa, ili ndege iweze kunyanyuka (lift) na kupaa angani inahitaji hewa yenye kasi kutoka mbele kupita kwenye mbawa zake (kasi hiyo hutegemea umbile na uzito wa ndege)

Kasi ya hewa inayopita mbele ya ndege wakati inakimbia kwenye Barbara ya kuruka ndiyo inaweka tofauti ya mkandamizo wa hewa (Pressure) kwenye mbawa.
Kutokana na umbile la mbawa, hewa ipitayo chini
inatengeneza 'pressure' kubwa kuliko ipitayo juu ya mbawa.

Hivyo 'pressure' kubwa chini husukuma mbawa juu kwenye 'pressure' ndogo na ndege kuanza kunyanyuka kwa kusaidiana na 'control' nyengine.

VISAIDIZI VYA KUPAA

Wakati wa kuruka na kutua, ndege inahitaji mwendo mdogo zaidi ili kuwa ndani ya mipaka ya urefu wa barabara (Runway).
Lakini mwendo mdogo hauwezi kunyanyua ndege ikihitaji kupaa wala kushikilia ndege hewani ikitaka kutua kwasababu 'pressure' ya hewa inayohitajika kunyanyua mbawa pia itakuwa ndogo.

Hapo ndipo wataalamu wa maumbohewa (Aerodynamics) wakabuni vifaa vya kusaidia ndege kuruka na kutua katika mwendo mdogo.
Vifaa hivyo ni kama 'Flaps, 'Slats na 'Spoilers' /Speedbrakes n.k

#FLAPS
Ni sehemu inayotembea nyuma ya mbawa(trailing edge) ambayo hupinda kuelekea chini au kuchomoka nyuma na kupinda kuelekea chini.
Wakati wa kupaa 'Flaps' hupinda chini kwa nyuzi kadhaa (degrees°) ili kusaidia kuongeza pressure zaidi ya kusukuma mbawa juu (lift).

Wakati wa kutua 'Flaps' hupinda chini kwa nyuzi nyingi zaidi kuongeza ukubwa wa mbawa na kubadili kuwa umbo ambalo linahifadhi 'pressure' kubwa zaidi na kuburuta (drag) ili kutua kwa mwendo mdogo pasipo kupoteza mnyanyuo (lift).

Hapa inarudi sayansi ya asili ambapo ndege hai pia hutua kwa kubinua mbawa zake nusu wima kwa kiasi kufanya 'angle of attack' Ili kutua taratibu.

#SLATS (Slots)
Ni sehemu inayotembea mbele ya mbawa.
Hizi ni kama bapa nyembamba za chuma zinazokunjuka na kufunga mbele ya mbawa ili kuongeza ukubwa na ufanisi wa hewa kupita.
'Slats' mara nyingi zinatembea pamoja na 'Flaps'
Hii mara nyingi ni Kwa ndege kubwa.

Kuongezeka ukubwa wa mbawa husaidia ndege kuruka na kutua kirahisi katika mwendo mdogo zaidi.
'Flaps na Slats' hutumika mara nyingi kwenye kuruka na kutua.

#SPOILERS/SPEEDBRAKE
'Spoilers' ni paneli zilizowekwa juu ya mbawa.
Mara nyingi ndege inapogusa chini wakati wa kutua huwa zinanyanyuka juu ya mbawa.
Kazi yake ni kukinzana/kuvuruga/kukinga hewa inayopita juu ya mbawa ili kuongeza mburuto kwenye ndege (drag) iweze kupunguza mwendo kwa haraka zaidi.

Pia zinasaidia kuongeza uzito wa ndege kwa kuikandamiza kwenye barabara ili breki za tairi zikamate vizuri inapotua
'Spoilers' au 'SpeedBreak' pia hutumika angani kama kupunguza kasi ya ndege kwa dharura/haraka.

Katika ukataji wa kona angani, baadhi ya 'Spoilers' inaweza kusaidiana automatiki na vielekezi vingine kama #Aileron au #Flaperon.

Kumbuka 'Spoilers' na 'Slats' sio rahisi kukuta kwenye ndege zote hasa ndogo kwakuwa hazina mwendo mkubwa wa kupaa na kutua.

Lakini pia Ndege kubwa (heavy aircraft) zinahitaji kupunguza mwendo haraka wakati wa kutua hivyo mara nyingi zinatumia brake tatu kwa wakati mmoja ili kusimama haraka,
1>'Spoilers'(speedbrake),
2>'Reverse' za injini (Thrust reverser) na
3>'Brake' za tairi.

Endapo ingekosekana teknolojia ya vifaa vya kusaidia kunyanyua, Si ajabu zingejengwa 'runway' zenye urefu wa kilometa nyingi zaidi.

NB:
Makala za #Admin sio Elimu kamili, bali kutoa mwangaza wa awali.
Tumia muda wako kujisomea kiundani.

Elimu ijayo tutaangalia je, ndege ina uwezo wa kurudi nyuma (reverse)

[emoji328]
FB_IMG_1683975069890.jpg
 
KISANDUKU CHEUSI (BLACK BOX)

(Tafsiri nyepesi)

Kisanduku au visanduku vyeusi maarufu kama "Black Boxes au Flight_Recorders") ni vifaa vya umeme katika muundo wa boksi ndogo za chuma ambapo kimoja hunasa sauti ndani ya chumba cha marubani (Cockpit) na kingine huifadhi data za mwenendo wa ndege pindi inapofanya kazi.

Mara nyingi visanduku hivi huwa viwili.

Kisanduku cha kwanza kinanaitwa '#Cockpit_Voice_Recorder {#CVR} ambacho kazi yake kunasa sauti ndani ya chumba cha marubani {#Cockpit)

Cha pili kinaitwa #Flight_Data_Recorder {#FDR} ambacho kinarekodi maelfu ya data za mwenendo wa ndege kama vile, mwendo, uelekeo, kimo, kona, taarifa za '#sensor', ngamizi, mifumo ya ndege na vitu vingine vya kiufundi kinachofanywa katika ndege husika.

Vifaa hivi husaidia kupata taarifa/sababu za uhakika endapo inatokea ajali au tukio la kuhatarisha usalama katika ndege.

Mara nyingi visanduku hivi vinasimikwa ndani ya mkia wa ndege na inatajwa sababu ya kuwekwa katika sehemu hiyo mara nyingi huwa inasalia katika ajali.

Kisanduku cheusi kinatengenezwa na malighafi madhubuti ambayo inaweza kuhimili misukosukokwa asilimia kama vishindo vya kupigiza ardhini (G-force zaidi ya 3000), Hali joto zaidi 1000°C kwa saa Moja au kukaa ndani ya maji kina cha Hadi kilomita 6 kwa siku 30.

Pia ndani vimeundwa na vifaa maalumu vya kuzalisha mawimbi ili kujulisha sehemu vilipo endapo vitakuwa ndani ya kina cha maji cha utefu wa Hadi kilomita 02 "Underwater_Locator_Beacon"

Visanduku hivi huwa vina rangi ya chungwa "#Orange" na sio rangi nyeusi kama vinavyoitwa ili kuweza kuonekana kirahisi pale ajali inapotokea.

Hakuna sababu za uhakika kwanini vifaa hivyo vinaitwa visanduku vyeusi "black box" ila baadhi ya wadau wa usafiri wa anga wanasema jina hilo linatokana na kurekodi matukio ya siri ya chombo na wahusika ambao wengine wanakuwa hawapo hai.

Admin,

#Like & #Share
Aviation Media Tz
Tweeter
Instagram
TikTok
YouTubeView attachment 2620138

Niliwahi kusoma makala moja ya jarida la mambo ya ndege na historia ya uvumbuzi wake

na walisema kuwa wakati walivyogundua hiyo teknolojia ya black box siku moja kabla ya kwenda kuonyesha maafisa wa serikali ilibidi kipakwe rangi Nyeusi ili kuendana na jina hilo, ila bahat mbaya wale waliopewa hiyo kazi hawakusikia vizuri na badala yake wakapaka rangi hiyo ya orange.

Nafikiri ni kioja kimoja wapo kilichoingia katika historia ya errors in engineering.

(Sikumbuki details vzr ila concept ni hyohyo)
 
"DINOS J.SAMARAS" BABA WA USAFIRI WA ANGA TANZANIA ASIYEFAHAMIKA NA WENGI

Endapo umewahi kuona au kusikia kampuni ya usafiri wa anga inayotoa huduma za kukodi ndege, kuuza au kufanya matengenezo katika jengo la kwanza la uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere (Terminal 1) iitwayo #TanzanAir basi hutoacha kutaja jina la #Dinos_J_Samaras.

Dinos (Sasa Marehemu) alizaliwa mnamo mwaka 1931 Dar es salaam, Tanzania na ni miongoni mwa watu wa kwanza kupata leseni za urubani nchini.
Awali alikuwa mkulima wa Mkonge, mwanachama wa #TANU na mbunge akiwakilisha #Morogoro enzi za #Tanganyika na baadae #Tanzania.

Mnamo mwaka 1967 alianzisha kampuni ya #Tanzanian_Air_Services_Ltd ambayo inajulikana zaidi kama TanzanAir na ndege yake ilianza kuruka rasmi mnamo 1969.

Baadae serikali ilimshauri kutengeneza karakana yake Jengo namba Moja (Terminal One) ili kuanza kutoa huduma za matengenezo ya ndege hapa nchini badala ya makampuni kwenda kufanya matengenezo #Nairobi nchini #Kenya.

Tangu hapo Dinos aliendeleza kampuni hadi kufikia kifo chake mnamo mwaka 2010 na kuacha kampuni kamili iliyoajiri watu zaidi ya 70.

Mwaka mmoja kabla ya kifo chake alitunukiwa medali na mamlaka ya usafiri wa anga ikimtambua kama "Baba wa usafiri wa anga Tanzania"

Dinos J.Samaras ameacha mke #Lela_Samaras ambaye pia ni mwanzilishi mwenza wa kampuni, pamoja na watoto wawili, #JohnSamaras (Mkurugenzi Mtendaji wa Sasa) na #JoannaSamaras ambao Kwa pamoja wanaendeleza vema kampuni hiyo.

Makao makuu ya TanzanAir yapo Jengo la kwanza 'Terminal One' katika uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) na Sasa wanaendesha ndege ndogo mbalimbali zenye injini za 'Pangaboi' ('TurboProps' za injini moja na mbili) ambazo zina uwezo wa kupakia idadi ya abiria tofauti kati ya 06 hadi 20.

Sehemu ya ndege wanazoendesha ni,
#Beechcraft_Kingair350i,
#Beechcraft_B200, #Beechcraft_1900D
#Cessna208_Caravan,
#Cessna406_Caravan_ii n.k

Admin.

Credits:
@Tanzanair
FB_IMG_1683979237758.jpg
 
JE, NDEGE INAWEZAJE KUPAA ANGANI? [emoji928]

{Ufafanuzi Mdogo}

Kumbuka ndege ina viungo vya msingi vinne (PrimaryComponents) [emoji2929]

1>Bodi/Kiwiliwili {Fuselage} kubeba abiria au mizigo.
2>Mbawa {Wings} kupaisha ndege na kubeba mafuta.
3>Mkia {Tail} kushikilia uelekeo wa ndege.
4>Injini: kusukuma ndege {Thrust}

Kila ndege ina mwendo wake ambao ikifika mbawa zinatengeneza "pressure" ya kutosha kuweza kunyanyua {Lift Off}.

Ndege inapokimbia katika njia ya kuruka {Runway} hewa inayokuja kutoka mbele inagawanywa mara mbili katika mbawa ambapo moja hupita juu na nyengine chini.

Kutokana na umbile la mbele ya mbawa {leading_edge} hewa inayopita juu ya mbawa inapita kwa kasi zaidi kuliko hewa inayopita chini.
Hali hiyo inapelekea hewa inayopita chini ya mbawa kuwa na mkandamizo mkubwa {HighPressure} kuliko ipitayo juu ya mbawa kadri ndege inavyoongeza kasi.

Hewa yenye "pressure" kubwa chini husukuma mbawa juu na ndege kuanza kunyanyuka taratibu {Lift}
Lakini ili iweze kunyanyua mbele na kupaa rasmi turudi kwenye vidhibiti vya mkia {TailControlSurface}

Mkia una mbawa ndogo mbili zilizolala {Horizontal stabilizer} zenye vidhibiti viitwavyo "Elevator".

Mkia uliosimama {vertical stabilizer} una kidhibiti kiitwacho "rudder".

Vidhibiti vya mkia uliolala kazi yake kuelekeza pua ya ndege kwenda juu au chini {Pitch} kulingana na maamrisho ya Rubani.

Endapo vidhibiti hivyo (elevators) vikigeuzwa na Rubani kuangalia juu pale ndege ikifikia kasi inayohitajika itaanza kunyanyuka mbele na kupaa kwasababu hewa inayopita mkiani itakinzwa upande wa juu na kukandamiza mkia kwenda chini hivyo kupelekea ndege kunyanyuka mbele.

Hali kadhalika na kinyume chake kama ndege ikiwa angani na rubani anataka kuanza kutua vidhibiti hivyo vitageuka kuangalia chini ambapo hewa inayopita chini ya mkia itakinzwa na kusukuma mkia juu ambapo upande wa mbele utalazimika kupelekea chini.
(Hii inafanya kazi kama mzani)

Na kidhibiti cha mkia uliosimama (Rudder) pia kazi yake kuelekeza pua ya ndege kwenda kulia au kushoto {Yaw}.
Endapo kidhibiti hicho (rudder) kitageuka kulia basi hewa ya upande huo itakinzwa na kusukuma mkia kwenda kushoto hivyo pua ya ndege italazimishwa kwenda kulia na kinyume chake.

Kwahiyo wakati ndege imefikia kasi yake ambayo hewa ina 'pressure' ya kutosha kuweza kunyanyua mbawa Rubani anaamuru vielekezi vya mkia uliolala (Elevator) kugeukia juu ambapo vitakinzana na hewa ipitayo juu kuweka uzito na kulazimisha mkia kwenda chini na pua kuelekea juu na kupaa.

Mbali ya yote, ndege huwa na vifaa vingine vinavyosaidia ndege kupaa na kutua kwa urahisi pasipo kuhitaji kasi kubwa sana.
Vifaa hivyo (lifting devices) vinavyochomoka na kuinama nyuma ya mbawa huitwa "flaps"
Ndege za kisasa zina vifaa vingine vya ziada kama 'Slats' mbele ya mbawa, Trims kwenye vidhibiti vya mkia n.k

Lakini pia Kuna 'Ailerons' kila bawa kwaajili ya ndege kulala kushoto au kulia hasa inapohitaji kukata kona angani kwa kusaidiana na kidhibiti cha mkia "rudder"
Pia husaidia kuweka ndege sawa pale inapoyumba (Aerodynamic Steering)

(Kumbuka ufafanuzi huu haikufanyi kuwa Rubani [emoji61])

#Like & #Share ili tuendelee kujifunza mambo mengine zaidi.

Elimu ijayo tutaangalia visaidizi vya ndege kupaa (Lifting Devices)

#Admin

[emoji991] Credit:
Airliners.net
FB_IMG_1683979405130.jpg
 
FAHAMU AINA YA INJINI ZA NDEGE

(ufafanuzi rahisi)

Ndege inaweza kuwa na injini 1 hadi 8 na katika hizo ni injini za aina mbili ndiyo maarufu:

(1)-Injini za #Jet (Zenye mfano wa pipa lililolazwa)

(2)-Injini za #Piston (Nyingi pangaboi)

1> INJINI ZA JET
Hizi zimegawanyika kutokana na 'modification' za ufanisi na matumizi yake:

a)Turbojet/PureJet'
Mfumo wa ndege nyingi za awali miaka ya 70 kushuka chini pia ndege za kivita.

b)Turbofan
Hizi ni injini za mfumo wa ndege nyingi za sasa ambazo zinakuwa na kipenyo kikubwa cha feni

c)Turboshaft
Mfumo wa baadhi ya ndege za sasa hasa Helicopter n.k

d)Turbo Propeller au 'Turbo Prop'
Mfumo wa ndege za kisasa za masafa mafupi zenye mapangaboi yanayoendeshwa na mfumo wa 'gas turbine' badala piston.

Ramjet/Scramjet
Mfumo ulio katika ndege za majaribio za mwendokasi mara nyingi ufanya kazi kuanzia mara tatu hadi tano ya kasi ya sauti 'Hypersonic' mfano mfano makombora na ndege za majaribio.

Injini za mfumo wa jet zinafanya kazi kwa mfano wa sheria ya Tatu ya #Newton (#action & reaction):

1-Kunyonya hewa mbele (Sucking)
2-Kukandamiza (compression)
3-Kulipua hewa iliyokandamizwa kwa kuchanganya na mafuta (Ignition)
4-Kutoka nyuma kwa kasi na kuisukuma ndege mbele (Thrust)
Kwa kifupi wanasema #Suck_Squeeze_Bang_Blow yaani Nyonya-kandamiza-Lipua-Puliza nje (nyuma)

Mfano wa Puto lililopulizwa na kuachiwa hewani pasipo kuzibwa mdomo litasukumwa kwakuwa hewa itatoka mdomoni kwenda kinyume na uelekeo wa puto.

Ndege nyingi kubwa za kisasa zinatumia injini aina ya 'Turbofan' (#gas_driven) ambazo zinasemakana kuwa na nguvu kubwa na ulaji mdogo wa mafuta.
Unaweza kutambua injini hizi kwa haraka kuangalia feni kubwa lililo mbele ya injini (Sio mapangaboi)

i> #Turbojet (Purejet)

Hizi zina vifeni vidogo vya compressor mbele ambavyo hufanya kazi ile ile ya kunyonya hewa kuingiza ndani (#air_inlet)>Hewa kukandamizwa na vifeni (#compressor_blades)>Hewa kulipuliwa katika (#combustion_chamber)>Hewa iliyolipuliwa kutoka kwa kasi nyuma (thrust) kwenye #exaust_nozzle.
Hii ndiyo nguvu pekee inayosukuma ndege kwenda mbele.
Injini hii hutumia mafuta mengi kuliko injini ya 'Turbofan' na nyingi zinatumika zaidi kwenye ndege za kivita na ndege za zamani.
Ni injini nyembamba/kipenyo kidogo zaidi kuliko turbofan.
Injini hizi zinakula mafuta mengi na kuzalisha nguvu ndogo kwa kuwa ni teknolojia ya zamani.

ii> #Turbofan

Hii ni injini itumikayo katika ndege nyingi hasa kubwa za kisasa.
Uboreshaji na ukubwa wake zinaondoa katika uhalisia wa kuitwa injini za jet halisi.
Hizi pia zinavuta na kusukuma hewa kama injini ya 'turbojet' isipokuwa zinavuta hewa mbili.
Hewa ya kwanza ni ile inayoingia kwenye mfumo wa ndani ya injini (#inner_core) kama ifanyavyo injini ya 'Turbojet' na ya pili inavutwa na feni lake kubwa mbele kupita nje ya mfumo wa ndani na kupuliza moja kwa moja nyuma ya injini.
Nguvu ya feni hilo mbele kuzunguka inatokana na kuzunguka visahani nyuma ya injini(turbine) ambavyo vimeungwa na #shaft' hadi katika feni hilo.
Hewa ipitayo nje ya mfumo wa injini (#Bypass_air) na hewa ya ipitayo ndani ya injini zote husukuma ndege kwa wakati mmoja ingawa hewa ipitayo nje ndiyo nyingi yenye nguvu zaidi.

iii- #Turbo_Prop au #TurboPropeller
Hizi zina mfumo wa injini kama turbofan hapo juu lakini mbele inakuwa na mapanga badala ya feni.
Visaani vya Turbine vinapozunguka vinazungusha shaft ambayo huzungusha mapanga mbele ya injini.
Mfano wa ndege hizi ni Bombardier Dash-8, ATR, Cesna208 n.k

iv- #Turbo_Shaft
Injini za Turboshaft' hufanya kazi kama Turbo Prop isipokuwa shaft inaunganishwa na mapanga makubwa marefu.
Hii shaft inaweza kuwa imeunganishwa na mfumo wa Gear au ikawa Free Turbine.
Injini hizi nyingi zinatumika kwenye #Helicopter za kisasa ili kuipa nguvu zaidi ya Helicopter zinazotumia injini za Piston.

#Scramjet/Ramjet.
Hizi ni injini za majaribio kwa roketi au ndege inayoenda kasi Mara tano ya kasi ya sauti (5500km/h).
Zina uwezo wa kuanza kufanya kazi katika mwendo huo kwasababu haina utumbo unaozunguka ndani kufua upepo bali kasi kubwa ya hewa inayoingia mbele haihitaji tena kuvutwa na kukandamizwa bali hulipuliwa moja kwa moja na kusukuma chombo.

2-MFUMO WA INJINI ZA PISTON
Injini hizi zina mfumo wa Piston kama ilivyo kwenye injini za gari isipokuwa crankshaft yake imeungwa na Mapanga mbele (Propeller Blades)
Mapanga yanafanya kazi ya kuchota upepo mbele na kupuliza nyuma ambapo husababisha ndege kwenda mbele.
Ndege nyingi zenye injini za piston ni ndogo na zile za zamani ambazo nyingi hutumia mafuta ya AvGas.

Tukumbuke pia injini za ndege hazina mahusiano wala kiunganishi chochote na tairi za ndege.
Injini za mfumo wa jet hutumia sana mafuta ya #JetA (Mafuta ya taa yaliyoboreshwa) wakati Piston hutumia #AvGas (kama petrol iliyoimarishwa)

Kumbuka pia Tairi za ndege ni 'freewheel' na zimeunganishwa na mifumo ya 'brake' na kona tu.
Hakuna kitu kinachozungusha tairi kutoka kwenye injini bali zinafuata uelekeo wa kule ndege inaposukumwa.

#Admin

Aviation Media Tanzania
FB_IMG_1683979582713.jpg
 
KWANINI "#PARACHUTE" SIO SALAMA KWA NDEGE ZA ABIRIA?

Watu wengi wamekuwa wakiuliza swali
"Kwanini ndege za abiria wasiweke miamvuli {#parachutes} ili kila mtu aweze kuruka inapotokea dharura"

Kiuhalisia kwasasa haiwezekani kwasababu zifuatazo:

1> Urukaji kwa kutumia mwamvuli {parachute} unahitaji mafunzo ya saa 4 hadi 5 darasani ikifuatia vitendo akiwemo mwalimu mmoja au wawili.
Utuaji unahitaji akili na ustadi mkubwa ili kuepuka kuvunja viungo vya mwili.
Ndege zibebazo abiria 100 hadi 500 ni vigumu kutoa mafunzo gharama na muda.

2>Urukaji wa kawaida wa mwamvuli ndege haitakiwi kuzidi kasi ya 200km/saa na umbali usiozidi futi 13,000 kwa warukaji waliobobea na Futi 3,500 warukaji wa kawaida ukiacha urukaji maalumu wa kijasusi au kijeshi.
Ndege kama #Boeing787 {#Dreamliner} kawaida hupaa futi 35,000 hadi 43,000 kwa kasi inayofika hadi 900km/saa.
Kuruka katika kasi hiyo unaweza kuvunjwa na kusambaratishwa na upepo na kupigizwa katika mbawa au mkia wa ndege.

Urukaji wa mwamvuli unaozidi futi 13,000 unahitaji kifaa maalumu cha kukufahamisha kimo ulichopo, #Musk na Mtungi wa '#oxygen' kwasababu umbali huo hakuna oksijeni ya kutosha hivyo unaweza kuzimia kwa kukosa hewa {#hypoxia} kabla ya kufika kimo sahihi cha kufungua mwamvuli wako.

3> Mwamvuli mmoja na vifaa vyake vya kiufundi unaweza kugharimu kati ya milioni 15 hadi 20.

4> Mafunzo yanahitaji kufahamu kuendesha mwamvuli huo pamoja na ishara za mikono kama njia ya mawasiliano.

5>Mwamvuli mmoja una kilogramu zaidi ya 20, mara idadi ya abiria wote ni uzito mkubwa sana ambao utaathiri mafuta na uzito wa ndege.

6>Urukaji wa mwamvuli unahitaji kupeana nafasi hadi futi 500 au nusu dakika kwa watu wa kawaida ili kuepuka kuvaana angani.
Hii si rahisi kwa abiria walio'panic kwenye dharura.

7>Takwimu zinaonesha ndege nyingi asilimia 80% hupata dharura wakati wa kutua au kupaa.
Hivyo hakuna muda na kimo cha kutosha abiria kuweza kuruka.

8> Ndege chache zipatazo dharura katika kimo cha mbali husababishwa na hali mbaya ya hewa kama wingu la mawe na radi {#thunderstorm} hivyo ni vigumu kuruka na mwamvuli katika hali hiyo.

9> Dharura nyingi zinahitaji ufunge mkanda kuepuka kurushwa au kuelea ndani ya ndege.
Kwahiyo ni vigumu kuvaa mwamvuli na kutembea kufikia mlango.
Pia ndege itahitaji mlango kuundwa na milango maalumu nyuma ya kutokea.

10> Ndege zipaazo kimo cha mbali huwa zinatengeneza mkandamizo wa hewa ndani {cabin_pressure} ili abiria apate mazingira yanayofanana na ardhini kuepusha damu kujaa gesi, kuchemka povu {#blood_boiling_bubbles} na kukusababishia kifo kwasababu ya 'pressure' ndogo.

Kutulia ndani ya Ndege ni salama zaidi:

Soma:
FB_IMG_1684080596873.jpg
 
ALIMANUSRA KUGONGWA NA NDEGE SABABU YA SIMU

Video imeibuka kutoka Brazili ya 'alimanusra' kati ya ndege inayotua na mtu aliyekuwa 'busy' kwenye simu yake.
Kisa hicho kilitokea katika maonyesho ya #Agrishow huko #Ribeirao_Preto.

Picha zinaonyesha mwanamume huyo akitembea kwenye njia fupi ya kurukia ndege huku #Beechcraft #Baron58 ikiwa inatua.
"Laiti kama asingeinama chini alikuwa anagongwa kichwani" wamesema mashuhuda.

Baadaye, video inayosemekana kuwa kutoka kwa mtazamo wa rubani ilitolewa ikionyesha jinsi alivyokuwa karibu kumgonga mpita njia.
Katika chapisho kwenye Instagram lililoripotiwa kutoka kwa rubani, alisema alimwona mtu huyo sekunde ya mwisho.

Bofya Link ifuatayo kwa Video ya tukio husika[emoji116]



Chanzo:
FB_IMG_1684080690563.jpg
 
JE, NDEGE INARUDI NYUMA?

Ndege nyingi za sasa zina mfumo wa kurudi nyuma #reverse' ambao mara nyingi hutumika kupunguza kasi wakati ikitua (#Braking).

Kwa baadhi ya ndege za 'Mapangaboi' #Propeller hutumia panga zake kubadili umbile (#angle) hivyo badala ya kuvuta hewa kwenda nyuma inasukuma kuelekea mbele na kusababisha ndege kupunguza kasi yake pale inapotua.

Hali kadhalika na kwenye injini zenye mfumo wa #Jet huwa zinafungua injini katikati na kubadili uelekeo wa hewa inayosukumwa nyuma kuvuja na kulazimishwa kuelekea mbele.

Baadhi ya Injini za mfumo wa 'jet nyingine zinafungua vimilango vyake vidogo katikati au nyuma ya injini.

Ndege nyingi kubwa zina mifumo mitatu ya kupunguza mwendo #braking ikiwemo

1>#Reverse' ya Injini au #Reverse_Thrust

2>'Brake' za matairi na

3> #Ground_Spoilers au #Speedbrake' ambazo ni bapa zinazo nyanyuka juu ya mbawa.

Hivi vyote mara nyingi hufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza kasi ya ndege inapotua ili kusimama haraka kwakuwa hutua na kasi kubwa sana.
Kasi ya kutua ndege kama #MD11 ikiwa imejaa mzigo hata Gari yako yenye speed 260km/h haifukuzi.

Brake zote za kukinzana na upepo {spoilers na reverse thrust} husaidia kutozipa mzigo mkubwa 'brake' za matairi ambazo huweza kupasua tairi, kuharibika, kuwaka moto au mda mwingine kuteleza kama barabara #Runway ikiwa imetuama maji endapo kama zitatumika pekee bila msaada wa #brake' nyengine.

Licha ya kukinzana na upepo juu ya mbawa, 'spoilers/speedbrake' pia husaidia kukandamiza ndege chini hivyo tairi kushika barabara vizuri wakati zinakamata 'brake kupunguza mwendo.

Sasa kwanini ndege haitumii 'Reverse' kujitoa kwenye Maegesho?
badala yake inasukumwa kurudi nyuma (#Pushback) na vigari maalumu #Tow_Truck/#Tug

1>Kuepuka kelele kali za 'reverse'

2>Kuepuka ulaji mafuta

3>Kuepuka hatari ya ndege kugongana na vitu vingine nyuma.

4>Kuepuka uharibifu wa injini kwa kunyonya taka na vumbi kwasababu upepo wa 'reverse' hutokea pembeni ya injini kwa kasi kubwa kuelekea mbele ya injini.

5> Reverse ni mfumo wa dharura ambao kiufundi haishauriwi kutumika hovyo kwasababu hewa yake inapitia sehemu za injini ambazo ni rahisi kupata uharibifu.

#Admin
Credit
#boldmethodView attachment 2620053
Sijaona ndege ikirudi nyuma, nimeona ikisukumwa na kagari hivi kuirudisha nyuma.
 
Back
Top Bottom