Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Sawa bosi kazana sasa ndoto itimiesi umeshaniambia nisikate tamaa ipo siku ntabeba abiria
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa bosi kazana sasa ndoto itimiesi umeshaniambia nisikate tamaa ipo siku ntabeba abiria
sawa mkuuSawa bosi kazana sasa ndoto itimie
KISANDUKU CHEUSI (BLACK BOX)
(Tafsiri nyepesi)
Kisanduku au visanduku vyeusi maarufu kama "Black Boxes au Flight_Recorders") ni vifaa vya umeme katika muundo wa boksi ndogo za chuma ambapo kimoja hunasa sauti ndani ya chumba cha marubani (Cockpit) na kingine huifadhi data za mwenendo wa ndege pindi inapofanya kazi.
Mara nyingi visanduku hivi huwa viwili.
Kisanduku cha kwanza kinanaitwa '#Cockpit_Voice_Recorder {#CVR} ambacho kazi yake kunasa sauti ndani ya chumba cha marubani {#Cockpit)
Cha pili kinaitwa #Flight_Data_Recorder {#FDR} ambacho kinarekodi maelfu ya data za mwenendo wa ndege kama vile, mwendo, uelekeo, kimo, kona, taarifa za '#sensor', ngamizi, mifumo ya ndege na vitu vingine vya kiufundi kinachofanywa katika ndege husika.
Vifaa hivi husaidia kupata taarifa/sababu za uhakika endapo inatokea ajali au tukio la kuhatarisha usalama katika ndege.
Mara nyingi visanduku hivi vinasimikwa ndani ya mkia wa ndege na inatajwa sababu ya kuwekwa katika sehemu hiyo mara nyingi huwa inasalia katika ajali.
Kisanduku cheusi kinatengenezwa na malighafi madhubuti ambayo inaweza kuhimili misukosukokwa asilimia kama vishindo vya kupigiza ardhini (G-force zaidi ya 3000), Hali joto zaidi 1000°C kwa saa Moja au kukaa ndani ya maji kina cha Hadi kilomita 6 kwa siku 30.
Pia ndani vimeundwa na vifaa maalumu vya kuzalisha mawimbi ili kujulisha sehemu vilipo endapo vitakuwa ndani ya kina cha maji cha utefu wa Hadi kilomita 02 "Underwater_Locator_Beacon"
Visanduku hivi huwa vina rangi ya chungwa "#Orange" na sio rangi nyeusi kama vinavyoitwa ili kuweza kuonekana kirahisi pale ajali inapotokea.
Hakuna sababu za uhakika kwanini vifaa hivyo vinaitwa visanduku vyeusi "black box" ila baadhi ya wadau wa usafiri wa anga wanasema jina hilo linatokana na kurekodi matukio ya siri ya chombo na wahusika ambao wengine wanakuwa hawapo hai.
Admin,
#Like & #Share
Aviation Media Tz
Tweeter
TikTok
YouTubeView attachment 2620138
Sijaona ndege ikirudi nyuma, nimeona ikisukumwa na kagari hivi kuirudisha nyuma.JE, NDEGE INARUDI NYUMA?
Ndege nyingi za sasa zina mfumo wa kurudi nyuma #reverse' ambao mara nyingi hutumika kupunguza kasi wakati ikitua (#Braking).
Kwa baadhi ya ndege za 'Mapangaboi' #Propeller hutumia panga zake kubadili umbile (#angle) hivyo badala ya kuvuta hewa kwenda nyuma inasukuma kuelekea mbele na kusababisha ndege kupunguza kasi yake pale inapotua.
Hali kadhalika na kwenye injini zenye mfumo wa #Jet huwa zinafungua injini katikati na kubadili uelekeo wa hewa inayosukumwa nyuma kuvuja na kulazimishwa kuelekea mbele.
Baadhi ya Injini za mfumo wa 'jet nyingine zinafungua vimilango vyake vidogo katikati au nyuma ya injini.
Ndege nyingi kubwa zina mifumo mitatu ya kupunguza mwendo #braking ikiwemo
1>#Reverse' ya Injini au #Reverse_Thrust
2>'Brake' za matairi na
3> #Ground_Spoilers au #Speedbrake' ambazo ni bapa zinazo nyanyuka juu ya mbawa.
Hivi vyote mara nyingi hufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza kasi ya ndege inapotua ili kusimama haraka kwakuwa hutua na kasi kubwa sana.
Kasi ya kutua ndege kama #MD11 ikiwa imejaa mzigo hata Gari yako yenye speed 260km/h haifukuzi.
Brake zote za kukinzana na upepo {spoilers na reverse thrust} husaidia kutozipa mzigo mkubwa 'brake' za matairi ambazo huweza kupasua tairi, kuharibika, kuwaka moto au mda mwingine kuteleza kama barabara #Runway ikiwa imetuama maji endapo kama zitatumika pekee bila msaada wa #brake' nyengine.
Licha ya kukinzana na upepo juu ya mbawa, 'spoilers/speedbrake' pia husaidia kukandamiza ndege chini hivyo tairi kushika barabara vizuri wakati zinakamata 'brake kupunguza mwendo.
Sasa kwanini ndege haitumii 'Reverse' kujitoa kwenye Maegesho?
badala yake inasukumwa kurudi nyuma (#Pushback) na vigari maalumu #Tow_Truck/#Tug
1>Kuepuka kelele kali za 'reverse'
2>Kuepuka ulaji mafuta
3>Kuepuka hatari ya ndege kugongana na vitu vingine nyuma.
4>Kuepuka uharibifu wa injini kwa kunyonya taka na vumbi kwasababu upepo wa 'reverse' hutokea pembeni ya injini kwa kasi kubwa kuelekea mbele ya injini.
5> Reverse ni mfumo wa dharura ambao kiufundi haishauriwi kutumika hovyo kwasababu hewa yake inapitia sehemu za injini ambazo ni rahisi kupata uharibifu.
#Admin
Credit
#boldmethodView attachment 2620053