Mada maalum ya ndege toka FB

Hii naikumbuka Midway airport, Chicago.
 
Ndege ya mizigo #Cargolux Boeing 747 imevunjika sehemu ya mfumo wa tairi za nyuma wakati wa kutua kwa dharura katika uwanja wa Ndege wa Luxemburg siku ya jumapili.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Taarifa zaidi:
 
ogopa sana hii habari uipate ukiwa ndani ya ndege ndo unatua!!
 
"PILATUS PC-12" UCHAWI KUTOKA USWIZI

Pilatus PC-12 ni ndege yenye mkandanizo wa hewa (pressurized cabin) ya injini moja 'turboprop' PT6A-67 inayotengenezwa na Pilatus Stans, Uswizi, tangu 1991.

Pilatus inatumiwa sana na, Mashirika madogo ya ndege ya kikanda, waendeshaji wa ndege za kubeba wagonjwa na mashirika mengi ya serikali ikwemo jeshi na polisi.

Inaweza kutembea umbali wa kilomita 2,804 katika mwendokasi wa 500km/h na kimo cha futi 30,000 ikiwa na abiria tisa ndani.
Ni moja ya ndege yenye mafanikio sana katika ufanisi na mauzo.
Pilatus PC-12 ina umbo hewa linalosababisha kuteleza angani mithili ya mshale kuliko ndege za 'mapangaboi' za jamii yake zenye injini moja na mbili.

Je, unafahamu kampuni zinazomiliki ndege hapa nchini?
Tuonane kwenye 'comments'

Chanzo:
Globalair.com

[emoji991]
@Pilotkel80
 
JINSI HELIKOPTA INAVYOPAA

(Ufafanuzi mwepesi)

#Helicopter ni ndege inayotumia mbawa zinayozunguka juu (panga) kutengeneza '#lift' ili iweze kunyanyuka kupaa.
Kumbuka ndege ya kawaida inategemea kusukumwa na injini kwenda mbele ili mbawa zake zipitiwe na hewa ya kutosha kuweza kutengeneza mkandamizo wa hewa chini ya mbawa utakaosababisha kunyanyuka 'lift' na kupaa.

Kwa Helikopta hali ni tofauti kidogo, kwani panga ndiyo zinakimbia/kuzunguka (rotation) ili kuzalisha 'lift' kwa kusukuma hewa chini.

Lakini pia ina panga ndogo nyuma {mkiani} ili kuzuia bodi {#fuselage} kuzunguka pamoja na panga kubwa inapozunguka (torque effect)

'Helicopter' kiasili ni ndege isiyotaka kupaa kwasababu vidhibiti vyake (contros) lazima vifanye kazi kwa kupingana ili iweze kwenda sawa.
Hiyo ndiyo sababu 'Helicopter' inahitaji hesabu kubwa zaidi kupaisha.

Hii ndiyo sababu hata baadhi ya Helikopta zinazotoka na mfumo wa kujiendesha yenyewe {autopilot} ni gharama kiasi.
Rubani wa Helikopta muda wote hufanya kazi ya kuipa milinganyo tofauti {balance} kati ya panga kubwa na ndogo itakayomwezesha kupaa alivyokusudia.

UPAAJI
{Endapo kila kitu shwari}
Rubani huwasha mzunguko wa injini #rpm hadi ifike kiwango kinachohitajika kwa kutumia '#throttle' {inafanana na mkono wa #acceleretor ya pikipiki}

Baada ya hapo huvuta juu taratibu '#collective' {inafanana na #handbrake ya mkono ya gari za zamani}
Kazi ya 'collective' ni kubadili 'angle' ya mapanga ya juu {rotor blades angle} ili iwe na umbile linaloweza kukandamiza hewa chini na kupaa {mfano wa panga za feni zilivyokunjwa ili kuweza kusukuma upepo}.

Wakati wa kunyanyuka ina tabia ya kiwiliwili kutaka kuzunga na panga kubwa {#torque effect} hivyo rubani huzuia hali hiyo kwa kukanyaga pedeli ya kulia au kushoto kuiweka sawa, kutegemea bodi inazunguka upande gani.
Pedeli hizi zina'control panga ndogo mkiani kama ilivyo kwenye ndege ya kawaida pedeli zinavyo'control' kielekezi (#rudder) mkiani ili kukata kona.

Ikifika kimo anachohitaji kwenda juu hutumia "#cyclic" ambayo ni 'control stick' iliyopo katikati ya miguu ya rubani na kazi yake kuinamisha panga kubwa iwe kulia, kushoto, mbele au nyuma ili helikopta ielekee upande ambao panga litainamia.

Kama ni kwenda mbele atasukuma mbele taratibu "cyclic" ambayo itasababisha mzunguko wa panga la juu {#main_rotor_disk} kuinama kidogo mbele na kusababisha helikopta kufuata kuelekea huo.
Hii ni kwasababu panga kubwa litaanza kukandamiza hewa kwenda chini na nyuma na kusababisha helikopta kunyanyuka juu na kwenda mbele (lift & Thrust)

Rubani pia anaweza kuongeza nguvu ya injini kidogo kwenye 'throttle' yake au kuvuta "collective" ili kuongeza kasi ya panga kuzalisha nguvu hizo mbili kutegemea na haraka au uzito wa Helkopta wakati huo akikanyaga kiumakini pedeli kusahihisha uelekeo.

Zipo 'Helikopta ambazo hazina panga ndogo nyuma, ila panga mbili kubwa zilizo katika nguzo moja (rotor must) ambazo zinazunguka kinyume ili kuondoa tatizo la kiwiliwili kuzunguka na panga wanaita 'Coaxial rotor' au 'Counter rotating Blades' mfano Kamov #Ka52.
Pia kuna Helkopta nyengine yenye panga zote kubwa mbele na nyuma zinazozunguka kinyume mfano #Chinook CH-47 ili kuondoa hali ya 'torque'effect.

Helkopta ni mashine ya kufanya kazi nyingi ambazo ndege ya kawaida haiwezi kufanya.
Na hii kutokana na uwezo wa wa kuganda sehemu moja hewani (hovering), kugeuka papo kwa papo, kwenda ubavu au kurudi kinyume na kutua sehemu ambazo ndege ya kawaida haiwezi.

Kutokana na ugumu wa kupaisha Helikopta wanaanga wanatumia usemi ufuatao;
"kupaisha ndege ya kawaida ni kama kuendesha baiskeli ya tairi mbili, lakini kupaisha Helkopta ni kama kuendesha baiskeli ya tairi moja.

#Like & #share!
#Admins
 
KAMBA NDANI YA CHUMBA CHA RUBANI..

Baadhi ya ndege zina kamba za kutoroka nje rubani pale inapotokea dharura kubwa kama ajali ya moto, mlango kujifung (jam) n.k

Mfano, Airbus320 ina kamba yenye fundo la mita 5.5 (futi 17.04) iliyohifadhiwa juu ya madirisha ya chumba cha marubani.

Kuna kamba 2 kwenye chumba cha marubani (moja kila upande).
Kamba hizi mara nyingi zina uwezo wa kubeba uzito kuanzia kg 150 na kuendelea.
 
Katika ndege ya American Airlines DC-10 kulikuwa na mfumo wa IFE ambapo kamera iliyo kwenye chumba cha maruba ilionesha matukio kwenye Luninga za abiria juu ya kile kilichokuwa kinaendelea.
Hivyo basi Flight 191 ilipoanguka, huenda abiria walishuhudia ajali hiyo kutoka hapa.
Baada ya ajali, IFE hii iliondolewa kutoka kwa DC-10 nyingine.

Chanzo:
Vintage Air Liners/Facebook
 
Mei 15
F-15D ya jeshi la ulinzi wa Kitaifa la Anga (Hispania) iliteleza nje ya njia ya kutua ndege baada ya kutua kwa dharura kwenye barabara ya 14 ya Uwanja wa Ndege wa Kingsley, Klamath Falls, Oregon.

@On the wings of aviation
 
JE, NI VIPI VIGEZO VYA KUSOMEA URUBANI?

'Ajuavyo Admin Wetu'

Unataka kuwa rubani?
Je, umekosa ndoto nyengine ambayo haitafirisi mzazi, mlezi au mdhamini?
Usijali, huu ni utani wenye ukweli ndani yake.

Kabla ya kupata dokezo la huko tuendapo, Kwanza tuanze na matumizi matatu ya msingi ya Usafiri wa Anga:

1>Mashirika Ya Ndege
2>Matumizi Binafsi, na
3> Matumizi ya Kijeshi.

MASHIRIKA YA NDEGE:
Mashirika/Makampuni hizi ni ndege zilizosajiliwa kufanya biashara ya kutoa huduma za usafiri wa anga kama kubeba abiria au mizigo kutoka sehemu moja kwenda nyengine.

BINAFSI
Hizi ni ndege binafsi za kiraia.
Usafiri huu unaweza kutumika kwa matembezi binafsi kama kula bata, biashara, tafiti, ufundishaji n.k
Umiliki wa sehemu hii sio rafiki sana kwa raia wa kusadikika.
Kumiliki ghali, kusajili ghali, uendeshaji ghali, kuegesha ghali, vipuri ghali, ufundi ghali na pia mafuta ghali.

KIJESHI:
Huu ni usafiri wa anga wa kijeshi.
Majeshi, hasa ya anga yanaweza kutumia usafiri huu kwa kusafirisha Askari, Mizigo, Ujasusi, Uokoaji, Kumpiga adui, Kujilinda n.k
Kwa Dunia ya sasa jeshi la anga ndiyo kama uti wa mgongo.

Wanasema Adui akikuwahi angani basi kashinda nusu ya vita, kwahiyo sio bunduki wala kifaru vitakusaidia sana na ndiyo maana nchi nyingi zinajitutumua kuimalisha ulinzi wa anga.
Hapa nisiongelee sana.

VIGEZO VYA KUJIFUNZA URUBANI

1>VIPIMO/MATIBABU
Cha kwanza lazima ukapime afya katika hospitali walizotibitisha Mamlaka ili uwe na Cheti cha Afya Daraja la 1 na utaendelea kupima kupata Vyeti vya madaraja mengine kadri unavyosoma leseni kubwa zaidi.
Utapimwa vitu kama Macho, Usikivu, Shinikizo la Moyo, ulemavu wa viungo vya msingi na Akili.
Hakuna mtu anayetaka kupaishwa na Rubani saa mbovu' futi 30,000.

2> ELIMU
Vigezo vinatofautiana kati ya shule na shule.
Wengine wanachukua kidato cha Nne, wengine cha sita, na hata wengine wanaangalia kichwa chako kinauwezo kiasi gani cha kujifunza na kuwasiliana kwa lugha inayotakiwa.

Kitu kimoja ningependa ufahamu hapa.
Nchi nyingi unaweza kujifunza urubani hata kama uliishia darasa la saba, ilihali uwe na vigezo vya Mdhibiti.

Mfano, umri wa kisheria kutoka Mamlaka za nchi tofauti zinataja mtu anaweza kujifunza urubani kuanzia umri wa miaka 16, 17 na 18 na kuendelea na ukomo wa miaka 60 au zaidi.
Hii ni kwasababu sio kila anayejifunza urubani anahitaji kurusha ndege ya biashara, bali wengine hujifunza kwaajili ya kurusha ndege binafsi.
Kumbuka muigizaji maarufu wa filamu Morgan Freeman alipata leseni ya urubani akiwa na miaka 65.

Mafunzo ya Urubani yanakuwa rahisi zaidi kwa mtu aliyepitia masomo ya Kiingereza, Hesabu na Jiografia na hata Fizikia kiasi.
Lakini hii haimaanishi mtu mwenye masomo tofauti hana vigezo vya kusomea urubani.
Hata mwanafunzi wa HKL anaweza kuwa Rubani sababu tayari ana msingi wa masomo tajwa kutoka 'Ordinary Level'
Changamoto ya kwanza endapo ukiwa na elimu chini ya ile iliyopendekezwa katika kujifunza Urubani, jiandae kukutana na ugumu wa kiasi chake.

Usingependa urudi nyumbani unaongea mwenyewe "Bora ningefunguliwa duka kariakoo"

Changamoto ya pili pia kama ukifanikiwa kupata Leseni ya urubani na elimu ndogo, fahamu kwamba mashirika mengi makubwa ya Ndege sasa yanapenda kuajiri kwa kuangalia Leseni pamoja na elimu yako (Leseni +Diploma au Degree)

Kama ilivyo kwa leseni ya gari, unaweza kuwa na Class C na elimu ya darasa la saba, ila kazi inahitaji mtu mwenye class C na elimu ya kidato cha 4 au 6.

Kwa kupitia shule ya mafunzo, Leseni unayohitaji inategemea unataka kuwa rubani wa aina gani.
Ikiwa unataka kuwa rubani wa ndege binafsi basi itabidi upate
'Private Pilot License' (PPL) ambayo ni masaa 40 hadi 50 ya ujuzi wa kupaa kabla ya kufanya mtihani wa kupata leseni.

Kama urubani wa abiria/biashara, basi upate
'Commercial Pilot License (CPL) masaa kuanzia 200 au 250 na kuendelea.

Pia ngazi nyengine ni 'Airline Transport Pilot License' (ATPL) ambayo ni mchanganyiko wa masaa ya kutosha, ujuzi na taaluma

3> ADA
Hapa jiandae kisaikolojia maana huyu ndiyo mchawi wa ndoto za urubani kwa kila mtu, hii hata Ulaya na Marekani.
Kama ulikuwa hujui anza kufahamu sasa masuala ya Usafiri wa anga hakuna kitu rahisi rahisi kama sekta nyengine.

Kupaa na ndege saa moja ya mafunzo ni kati ya dola za kimarekani $200-$300.
Unahitaji saa 40-45 ili kuweza kufanya mtihani kupata leseni binafsi tu (PPL), kisha zinahitajika saa 200 za kufanya mtihani wa Leseni za biashara (CPL) hapo sijaongelea gharama za darasani (ground school) na matakwa mengine.

Ingawa baadhi watu huomba kudandia ndege za walimu baada ya kupata Leseni ya PPL ili kutafuta ujuzi kujenga masaa na kupunguza gharama kuelekea CPL.

Bahati mbaya zaidi kupata udhamini wa kusomeshwa Urubani kutoka kwa mtu baki, Taasisi au kampuni si jambo rahisi hata kidogo.
Tuelewane hapa, mzazi, mlezi, mdhamini, mtoaji mikopo anahitaji kujidhatiti na kujitoa kwelikweli ili kufanikisha malengo ya mlengwa anayehitaji kuwa rubani.

Tuliona kijana #NarcentMeena aliamua kuuza karanga za jumla na rejareja ili apate ada ya kujisomesha urubani ili kutimiza ndoto yake.

Mbali na yote, kuwa rubani inawezekana hata kwa mtu wa chini wa kawaida.
Muda mwingine 'mchawi sio kibunda' mchawi matumizi na akiba.
Kama mwanao ana miaka mi 5,10,15 mfungulie fixed akaunti ili kila ukiokota miambili unaweka, au wale wa Bia unagawanya nusu kaunta nusu akaunti.
Usingoje Kafika miaka18 ndiyo utafute pesa kwa mkupuo za mkupuo, ni ngumu sana.
Wanasema cha kesho jenga leo.
La sivyo utasikia lawama tu "mbona marubani wengi ni wale wenye ngozi ile"

Kama hatujakosea sana, hapa nchini kuna vyuo kama Vinne vinavyotoa Mafunzo ya Urubani
Fly Zanzibar
NIT-Mabibo
Tanzania Pilot Training Centre na
ZRP-Zanzibar.

NB
Kumbuka, kurasa za Aviation Media Tanzania hazina mahusiano na Mamlaka za usafiri wa anga, viwanja vya ndege, Mashirika ya Ndege, wala Taasisi za Mafunzo ya anga tofauti na Habari tu.

Ajuavyo Admin.
 
The 2332 cc is ready for our upcoming street legal race season (once the wildfires subside).
Street friendly 11.5:1 CR for 94 octane (98 RON) at 3,500 ft (1070m) elevation.
Mixture of parts:
*Vintage Italian 48 IDAs.
*JPM venturies/manifolds/heads/exhaust/pushrods/tubes.
*CB2300 street-strip camshaft/wedgemated crank/flywheel/cylinders (honed).
*Wiseco pistons (notched).
*Scat 1.4 rocker arm kit and valve covers.
*Berg deep sump.
*Geers oil filter.
*MSD full setup.
Many thanks to those who provided build tips![emoji178]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…