MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Mpeni majibu yenye matumaini jamani na sio kumkejeli yani hakuna kitu kinauma kama mzazi akiona mwanae hakui katika uwiano sawa na wenzake. Kuna rfk angu mmoja alikua na mtoto na yy akiwa hivyo ila nadhani wa kwake hakua anaongea maneno mapk 3 yrs wakaenda muhimbili kuja kugundua badae ni kuwa mtoto alibanwa mishipa ya fahamu iliyo karibu na masikio so hasikii vzr ndo kilichompelekea kutokuongea kwa wakati.

So nashauri wazazi tuwe tunawachunguza watt na tupende ku google ateleast satages za ukuaji. Mfano mtt wa miezi fulani anatakiwa aweje au afanye matendo gani. Hii hupelekea kutambua tatz mapema kwa sababu wanasema ni rahisi mtoto kutibika tatizo lake akiwahi kabla hajafikia miaka 3.

Ila usikate tamaa huyo kama anatoa sauti na anatamka baba mama inawezekana ni uzito tuu wa ulimi endeleeni kumfanyia uchunguzi na urudi hospital usikubali ushauri wa mitaani. Msumbueni daktari mpk aone kuna ulazima wa kutake more mesurement.
 
Kingine kama mtoto hana mtu wa kumwongelesha maneno madogo madogo hasa watoto wenzie lazima atachelewa kuongea, mtoto hawezi jifunza kuongea vizuri kwa watu wazima bali kwa watoto wenzake, nyie huwa mna Masentesi marefu marefu.

Mfaano umesema akiongea ukihesabu maneno hayafiki 30, kwa kweli mtoto wa miaka 30 kutengeneza maneno 30 kwa wakati mmoja ni hawezi hata wa darasa kwanza hawezi, labda wa darasa la tatu ndo anaweza kujieleza kwa maneno 30, kumbuka maneno 30 ni aya (paragraph) nzima.

Kama mwanao kwa umri huo anataja mama, bibi, dada, kaka atajifunza tu mengine akianza kucheza na wenzake mpe mda kikubwa uspanic
 
Asante sana mkuu kwa ushauri.Mungu akubariki sana.
 
Nashkuru sana mkuu...inaumiza sana nafsi unapomuona mwanao anajaribu kukueleza kitu akiwa na furaha kisha wewe huelewi naye anategemea umjibu basi unabaki kujichekesha nayeye anabaki kukutizama usoni...ah ila ndiyo maisha tutafanyaje!
Kabisa mi zaman nilikua nalia ila sasa nimezoea namuachia mungu sababu jitihada zote nimeshafanya
 
Jaribu kuirepost na kule kwenye jukwaa la jf doctor huenda ukapata ushauri mzuri zaidi
 
Utakuwa mnamlea sanaa kizungu Huyo ,au atakuwa geti kali. Chukua watoto waomzidi kidogo aishi nao halo kwako au mwache ajichanganye na watoto wa rika lake uswahilini mda si mrefu utaona anaongea vizuri tu.
 

mkuu thanks for this
na mie ninatatizo kama lako japo mie mtt wangu ana miaka saba na bado hajachanganya kbs
naomba kama mwenye namba ya huyo mtaalam atushirikishe na ss ili tuangalie cha kufanya mapema
natanguliza shukran
 
Utakuwa mnamlea sanaa kizungu Huyo ,au atakuwa geti kali. Chukua watoto waomzidi kidogo aishi nao halo kwako au mwache ajichanganye na watoto wa rika lake uswahilini mda si mrefu utaona anaongea vizuri tu.
Tayari nimeshamwanzisha shule mkuu,so tayari anakaa na watoto wenzie.
 
mkuu thanks for this
na mie ninatatizo kama lako japo mie mtt wangu ana miaka saba na bado hajachanganya kbs
naomba kama mwenye namba ya huyo mtaalam atushirikishe na ss ili tuangalie cha kufanya mapema
natanguliza shukran
Tuombe uzima mkuu nitaku-PM number yake kesho.
 
Kabemendwa huyo
 

Hata darasani atakuwa anachelewa kuelewa kusoma

Mpeleke kwenye maombi
 
Aisee mkuu ktk hilo kundi nitoe kabisa maana kama ingekuwa kuiona pepo ni kuheshimu ndoa tu basi mimi pepo ingekuwa ya kwangu bila shaka yoyote.ila nashkuru umenifamisha.
nakujuan vizuri sana. unataka nifunguke
 
Dah pole saana mkuu, kuna uzi niliuketaga humu (in 2016) ukiulizia hili jambo. Na mm lilinsibu ila nimempatia speech therapist ndo naona anaanza improve.
Pole saana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…