Mtoto Wa mdogo wangu alichelewa kuongea, na vile ninavyompenda jamani nikawa nahisi kulia. Siku moja mama yake akanipigia "chu..." Kaongea dah nilifurahi, alianza na neno baba akiwa na umri wa miaka 3.
Ndani ya miezi mi 3 ali develop Maneno mengi zaidi, mama, Dada, bibi etc, ila Maneno mengi alikuwa anayatamka tofauti, eg, ajiwa= majiwa, sasa= Chacha, chikamo= shikamoo, bali= wali, Dage= maharage, danga=Karanga, jaji=Maji, Chule= shule chimu=simu etc
Ndani ya miezi sita alianza kuongea sana mpaka tunashangaa, akawa anaongea kila kitu as if analipiza muda ambao hakuongea.
Mtoto alikuwa mchanganfu kila mtu akawa anatamani ambebe. Ni wa kike lakini anapendwa na jinsia ya kiume mpaka basi, kila mwanaume umsalimia chikamoo baba.😁 nadhani kwakuwa neno la kwanza kutamka lilikuwa baba ndo maana anapendwa na jinsia ya me.
Kuna kipindi alikuja kukaaa na mm, wakaka wa huku wote wakitoka kazini anawapokea getini, wote anawaita baba😀 ananiomba simu awapigie 😁 hawajui majina, ila anajua vyumba vyao, anaita baba wa kule, anawapigia simu, anawambia, " nimewamichii"😀
Wanamletea jawadi😁.
Kwa sasa anaongea utadhani anachoma taarifa ya habari, ana miaka chita, anachoma daracha la kwanja.😀😀😂