Mkuu usiwe na wasiwasi ataongea tu muda ukifika--huyo hana tatizo lolote la kiufundi--ni tatizo la kimaumbile tu. Watoto wa kiume huchelewa sana kuongea. Mtoto wangu alianza kuongea akiwa na umri wa miaka 3.5. Mpaka sasa anakaribia miaka 4 lakini bado anaongea kwa kusuasua.
Kipindi hajaweza kuongea, akiwa na tatizo humshika mtu mkono na kumpeleka kwenye friji kisha kuonyesha anachotaka--maji, soda, juice, etc. Niliogopa nikadhani mwananangu ana tatizo lakini kila nikiangalia matendo namuona yupo intelligent sana.
Mtoto wako ataongea tu usiwe na wasiwasi. kuna mtu nilikutana naye akasema watoto wake wote huchelewa sana kuongea--huongea wakiwa na umri wa miaka 5. ni suala la kawaida. brain development differs from child to child. your child will speak eventually.