Nyegere ama Honey Badger
Huyu jamaa ni mkorofi sana na haogopi chochote. Anapambana mpaka na simba na anajulikana na wanyama wengine kama mnyama mkorofi mpaka wengi huwa wanaamua kuachana nae tu, ingawa ana kamwili kadogo.
Anapenda asali na huifuata hata sebuleni kwa nyuki, na wakimdunga asilii chochote maana ana ngozi ngumu sana. Chakula chake kingine pendwa ni nyoka na nge. Sumu zao hazina madhara kwake, yeye akikutana nao ni kushambulia tu na kula.
View attachment 2044067
Kitu cha ajabu nilichojifunza ni kuwa duma wamevolve kuzaa watoto wanaofana na nyegere. Evolution iliwafundisha kuwa nyegere huwa hasumbuliwi na boya yeyote hivyo wakaevole ku mimic/camouflage kama nyegere.Duma ni dhaifu kulingana na wengine kama chui, simba, nk hivyo hawezi kutegemea ubabe wake, ikabidi atafute namna kwa evolution. Mama duma huwa analazimika kuwaacha watoto wake akienda kuwinda hivyo watoto wanakuwa hatarini zaidi mama akiwa mbali. Hivyo basi kwa kuwa watoto wa duma wana nywele nyeupe mgongoni, kwa mbali wanaoneka kama nyegere kwa maadui, nao maadui wakiwaona wanajisemea tu 'daah, nyegere wale, tuachane nao tu', hivyo vitoto vya duma vinapona.
View attachment 2044068