Mada ya wanyama

Mada ya wanyama

WAJUE WANYAMA KWA SIFA ZAO ZA KIPEKEE.

1. Nyangumi.
Huyu ndio mnyama mkubwa kuliko wanyama wote, ukimuweka katika kiwanja cha mpira wa miguu, hubakiza mita chache ili kufikia nusu ya kiwanja hicho, mbali na ukubwa huo lakini ni mnyama mwenye macho madogo sana, ila sehemu za siri noma sana dume huwa na uume wenye futi 12.

2. Twiga.
Huyu ndiye mnyama mrefu kwenda juu kuliko wanyama wote unaowafahamu, anapenda amani, ni mpole lakini hapendi mizaha, miguu yake ndio silaha pindi anapovamiwa na hilo teke usiombe.

3. Kozi
Huyu ndiye kiumbe mwenye uwezo wa kukimbia kuliko mnyama yoyote, ni ndege mwenye ufanano sana na tai, ukimshitua akakimbia kama upo Dar es salaam usiendelee kumtafuta dar, wapigie ndugu zako moro kuuliza kama ametua huko au lah.

4. Nyegere.
Ndio anavunja rekodi kwa wivu alishawashangaza watalii hapo Serengeti baada ya jike wake kujikwaa, alichimba shimo refu kidogo kuhakiki kama ile ilikuwa ni ajali kweli, au kuna faulo alitaka kuchezewa kwa bae wake.

5. Kobe
Ndiye mnyama anayeishi miaka mingi duniani, pengine kuliko wanyama wengine wote hufikia miaka hadi 350, kwa Tanzania tunao wenye miaka 200+, kama nakuona raha za dunia zinavyokufanya utamani kuwa Kobe.

6. Kicheche.
Ndiye mnyama anayependa ngono kuliko kiumbe yoyote, wanapokutana jinsia tofauti kabla ya salamu huanza kusasambua kwanza, yaani hawa katika jamii zao hata msibani hukutana kwa mapenzi pia, inakadiriwa kwa siku ili walale usingizini mwororo auheni wapitiane mara 60 na zaidi ! Na ndio sababu hata mtu akiwa kiwembe huitwa kicheche.

7. Konokono.
Ndio kiumbe anayesafiri taratibu sana na hii ni kwa sababu hujitengenezea njia ya kupita kwanza ndipo apite.

8. Tai
Ndio kiumbe mkorofi kupita kiasi ni kawaida kunyang'anya watalii chakula, ni kawaida kusumbua ndege wenzie wanapoatamia, kupigana nk ili mradi fujo.

9. Nyati
Mnyama mwenye hasira na kisasi kuliko wanyama wengine wote, simba wanamwelewa vyema sana huyu kiumbe, wakithubutu kuua mtoto wake na wao huenda kukanyaga watoto wake vile vile au vipi bwana jicho kwa jicho, jino kwa jino tuone sasa.

10. Kipepeo.
Ndiye kiumbe mpenda amani pasina mfano, ukipita msituni umenuna usitegemee watakusogelea, ila mkipita na mwenza wako, mnacheka mna furaha, ahaa utashangaa wanawapamba !

11. Simba.
Pengine sababu ya kuitwa Mfalme ni ubabe, Dume la simba ndio mnyama pekee anayejijua kwamba anaogopwa na hata majike wake wanapopata dhahama, akipata taarifa hujitokeza mara moja na ukiona madume yameongozana mawili basi jua huo mziki mwamuzi ni Mungu.

12. Mbu
Ndio kiumbe aliyeweza kuua binadamu wengi sana kuliko mnyama yoyote yule unayemfahamu wewe, utapokaona tafadhari Katie kitasa.

13. Komba
Ndiye mnyama mlevi kuliko wanyama wote na akilewa hulia pasina sababu ya msingi, hata ukibahatika kumuona sura yake imekaa kilevi levi, hupendelea pombe za kienyeji kuliko bia, we watege kwa mnazi au ulanzi sio misosi hapo utawapata.

14. Popo
Pamoja kwamba mchoro wake hupendeza sana katika michoro, ila ni miongoni mwa viumbe wenye sura mbaya sana kuliko wengine wote.

15. Tembo
Ndiye mnyama mwenye uwezo wa kuhifadhi sana kumbukumbu katika kichwa chake, kama ulipojenga walihawi kupita tegemea kuna siku watakuwa wageni wako, wakati tunakazana kusema tembo wamevamia sehemu fulani tukae tukijua maeneo hayo wana historia nayo, sasa siku mpige jiwe mkutane baada ya miaka kumi ndio utajua ule mkonga ni bakora au pua.

16. Pomboo
Ndiye mnyama mwenye huruma sana kiasi kwamba akikuona una tatizo, huacha mambo yake na kutaka kukusaidia
Itaendelea...
 
Sijui kwanini nyoka wanakulana

Eneweiss hata wachawi nao wanakula watu, wamelaaniwa kama nyoka
Hahahahaa na kujikula wakizidiwa na njaa ..wachawi hawajikuli
 

Attachments

  • kronos-kingsnake.jpg
    kronos-kingsnake.jpg
    341.4 KB · Views: 105
WANYAMA NA TABIA ZA BINADAMU


1. PUNDA: anaposema "Siendi" haendi hata umpige na gogo la mbuyu. kuna watu ambao waking'ang'ania wazo moja hata aambiwe ukweli aje, habadilishi wazo lake.
PUNDA

2: SIMBA: Huyu ni mgomvi" watu wenye tabia za simba wapo tayari kupigana kwa vyovyote vile na yeyote yule anayeingilia mipango ama matakwa yao.
SIMBA
3: SUNGURA: yeye ni kutimua Mbio tu. Watu wenye tabia ya Sungura siku zote hawatatui tatizo, wakiona ugomvi ama vuguvugu la ugomvi linataka kutokea haraka sana wanabadilisha maada. Hawa ni waoga
SUNGURA
Leo nimejalibu kuweka hao wachache, ila wapo wengi jalibu kutembelea kila siku Blog hii utapata kuona jinsi tabia zetu zinavyofanana na wanyama. Leo unaweza usione tabia unayofanana nayo ila nakuhaidi posti ijayo utaikuta.


4: NYANI: Anapumbaza na Mcheshi, Mara nyingi watu wenye tabia za nyani huwa wanapenda kuwa wachekeshaji sana na wanapumbaza wenzao pale wanapokua wanafanya mambo muhimu.

NYANI
5: NYOKA: Huyu huwa anapenda kujificha kwenye nyasi na huruka ghafla na kung'ata. Wapo watu wenye tabia kama za nyoka, Mara nyingi huwa wanakaa kimya kwa muda mrefu wakati jamii fulani ikiwa inashiriki kufanya jambo, lakini endapo wakisema jambo moja tu huaribu kila kitu kinachoendelea.

NYOKA

6: KOBE: Huyu upenda kujiingiza ndani ya nyumba yake endapo mazingira hayapo shwari, na hujitoa anapohisi hali imekua shwari nje. Wapo watu watabia kama za kobe, hupenda kujitoa kwenye jamii ama kundi endapo kuna matatizo, hawatoi mchango wowote ule, kama wa mawazo, pengine wangependa jamii isifahamu kama wapo ndani ya hiyo jamii ili wasisumbuliwe kabisa.

KOBE
7: TEMBO: Anatabia ya kuangusha miti barabarani, na kuzui njia ili chochote kisipite hadi atakapo amua yeye. Wapo Ndugu zetu wenye hizi tabia, wanakua wasumbumbufu, wababe huzuia kundi kuendelea na shuguli zake kufikia malengo yaliyopangwa.


TEMBO
8: MBUNI: Huona kila kitu kipo sawa wakati wote, hawafikiri kama kuna tatizo kamwe. Wapo watu wenye tabia kama za Mbuni, mara nyingi huinamisha kichwa chake kwenye mchanga, hukataa kabisa kukubali kama kuna matatizo.
 
Huyu ni mmoja ya wanyama wenye akili sana duniani. Kwenye top four kuna sokwe mtu, mbwa, pomboo(dolphin) na huyu jamaa. Pia ni bosi mmoja msafi sana. Kama umewahi mfuga utakuta anajisaidia mbali na anapokula.
Umemsahau Tembo
 
Mnyama mpenda ngono zaidi...ndio mwenye janaba kali kuliko wote

Kicheche ni mnyama mdogo mwenye vituko vingi ambavyo huwashangaza watu wengi na moja ya kituko chake ni uwezo wake mkubwa wa kujamiana mara nyingi zaidi kwa siku na wana milio maalum kila wakitaka kujamiana.

Wataalamu wa wanyama wanasema kuwa kicheche anauwezo wa kujamiana mara 26 kwa siku sawa na mtu kukimbia umbali wa 360km kwa siku.

Na anauwezo wa kuishi kwa miaka 13 tu.

Kicheche ni mnyama anayepatikana katika sehemu ya jangwa la sahara Barani Afrika ukanda wa savana ni adimu sana kupatikana katika misitu mikubwa kama ya Congo na maeneo ya pwani.

Kicheche anafanana sana na Nguchiro ana urefu wa sentimeta 60, urefu huo ukijumlisha mwili na mkia wake ambapo mkia pekee una urefu wa sentimeta 20.

Chakula kikubwa cha kicheche ni ndege, nyoka, mijusi, chura, wadudu na wanyama wengine wadogo kama panya nk.

Unaambiwa wakati wa kukabiliana na maadui mnyama huyo hutoa harufu kali kwa kujamba na kuwafanya maadui kugaili kumkamata na wazungu humuita “Father of stinks kutokana na harufu kali anayo toa wakati akijihami na maadui.

Pia kicheche ana tabia ya kuinua mkia wake kwa kubinua mgongo ili aonekane mkubwa baada ya kumuona adui yake kwa lengo la kumtisha na mara nyingi hupenda kula kila wakati
 
He[emoji44]
We jamaa namashaka na uwezo wa ubongo wako kuelewa mambo mbali mbali. Yaani researches na studies zote hizo zilizofanyika zinazopatikana katika vyanzo mbalimbali unauliza mtu amejuaje Jambo?
Mshana Jr njoo umueleweshe mtu wako huku
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Huyu ndo mnyama anaesadikiwa kuwa mvivu kuliko wote duniani.Mnyama huyu hulala kwa muda wa masaa 18 kwa siku kwa kuning’inia kwenye matawi ya miti na akiwa anatembea ardhini anatumia muda wa dakika 1 kutembea umbali wa kati ya Sentimeta 15-30 ambao ni sawa na urefu wa rula moja.kitaalamu anaitwa lazy sloth.
Sloths.jpg
 
Huyu ndo mnyama anaesadikiwa kuwa mvivu kuliko wote duniani.Mnyama huyu hulala kwa muda wa masaa 18 kwa siku kwa kuning’inia kwenye matawi ya miti na akiwa anatembea ardhini anatumia muda wa dakika 1 kutembea umbali wa kati ya Sentimeta 15-30 ambao ni sawa na urefu wa rula moja.kitaalamu anaitwa lazy sloth.View attachment 1710371
Unalala sangap mzee??
 
Siyo kila mara nyoka akikung'ata atakuachia sumu. Huweza kukung'ata na asikuachie sumu kwakua anajua wewe siyo chakula chake hivyo hawezi kupoteza sumu yake wakati ataihitaji katika kuwinda.

Kitendo cha kung'ata bila kutoa sumu huitwa 'Dry bite' takwimu zinasema kwamba kuna uwezekano mkubwa wa mwanamke kudanganya kafika kileleni kuliko nyoka kukung'ata na kukuachia sumu.
 
Nyoka wengi humuepuka binadamu, ndiyo maana hata habari za anaconda hazijulikani sana kwakua akihisi uwepo wa binadamu hutoweka eneo hilo mara moja. Exception ipo kwa wanafamilia wawili, kobra na koboko.

Kumekua na taarifa zinazochanganya, mfano mwanzo iliaminiwa kwamba nyoka hawa hutafuta ugomvi, yaani wanaweza kukuona ukiwa mbali na wakakufuata. Hivi karibuni taarifa mpya iliyotoka ilikanusha madai hayo na kusema na wao hukimbia binadamu na hushambulia wakiwa threatened tu.

Nyoka hawa hukua mpaka kufikia urefu wa futi 11, kwa ufananisho Hashim Thabit ana urefu wa futi 7. Koboko akiwa anashambulia hupendelea kunyooka kiasi kwamba anakupita urefu kisha ugomvi uanze vizuri.
 
Back
Top Bottom