Mada ya wanyama

Mada ya wanyama

Screenshot_20220203-082248.jpg
 
TANZIA[emoji29]

Panya wa kiume kutoka Tanzania, Magawa ambaye mwaka 2020 alitunukiwa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini nchini Cambodia, amekufa akiwa ni panya Mzee mwenye umri wa miaka minane ambao ni umri mkubwa kwa panya.

Mwezi November mwaka jana Magawa alitimiza umri wa miaka minane na alistaafu pia mwaka jana kutokana na uzee wake kwakuwa alianza kupunguza kasi ya kutegua mabomu.

Magawa alizaliwa Tanzania November 5,2014 akiwa na uzani wa KG 1.2 na urefu wa Sentimita 70 na hadi anakufa amenusa mabomu na silaha nyingine zaidi ya 100.

Magawa amefia nchini Cambodia kwakuwa baada ya kustaafu hakurejeshwa Tanzania na amekufa usiku wa kuamkia Jumapili ya juzi.
#MillardAyoUPDATES
Mungu afanye ukubwa wake kwenye afya ya kijana wako.
Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom