Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Kikosi maalum cha Kijeshi nchini Madagascar cha 'CAPSAT' kimetangaza kuchukua madaraka, kikimwondoa madarakani Rais Andry Rajoelina, baada ya Wabunge katika Bunge la kitaifa kupiga kura ya kumwondoa, licha ya Rais Rajoelina kutangaza kulivunja kabla ya kura kupigwa.
Kwa mujibu wa #BBCNews, Uamuzi wa Jeshi hilo umefikiwa leo Oktoba 14, 2025, wakati ambapo bado inaelezwa kwamba haifahamiki ni wapi alipo kiongozi huyo baada ya kudaiwa kuonekana akiondoka kwa Ndege ya Jeshi la Ufaransa.
Jenerali mwandamizi wa Jeshi ametoa kauli kuwa, vikosi vya usalama vinafanya kazi pamoja ili kudumisha utulivu katika taifa hilo ambalo limekumbwa na wiki kadhaa za maandamano dhidi ya utawala wa Rais Rajoelina.
Soma Pia: Rais wa Madagascar aondolewa madarakani na wabunge saa chache baada ya kuvunja bunge
Mwaka 2009, kikosi hicho cha CAPSAT kilimuunga mkono Rajoelina alipoipindua Serikali ya Rais wa wakati huo, Marc Ravalomanana na sasa kimegeuka dhidi yake kufuatia maandamano makubwa ya watu wasioridhishwa na utawala wake.