Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Madagascar imeamua kubadili mtazamo wake juu ya kukabiliana na virusi vya corona na kujumuika na jitihada za kimataifa kupata chanjo ya corona."Kuna hatua kadhaa ambazo inabidi kupitia kabla ya kupata chanjo hiyo lakini kujisajili ndio jambo la msingi na hatua muhimu kabla ya kupata chanjo hiyo, lakini tayari tuko kwenye hatua muhimu katika usajili," Waziri wa Afya Prof Jean Louis Rakotovao alisema kwenye video aliyoiweka kwenye ukurasa wa wizara yake wa Facebook.
Awali Madagascar ilionesha kutokuwa na nia ya kushiriki katika jitihada za kupokea chanjo. Ilidai kuwa ni bora kutumia dawa ya asili inayofahamika kama Covid-Organics.
Dawa hiyo ambayo iko katika mfumo wa chai au vidonge iliitangazwa na Rais wa taifa hilo bwana Andry Rajoelina kuwa ndio dawa ya corona.
Hata hivyo hakuna tiba ya virusi vya corona, Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani.