Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania - OUT), Adam Namamba amezungumza na JamiiForums kuhusu madai ya baadhi ya Watumishi wa Chuo hicho kutolipwa stahiki zao mbalimbali.
Awali, Wanachama wa JamiiForums.com walidai kuna changamoto ya kutopatikana kwa fedha ya kujikimu, posho na malipo mengine mbalimbali hali ambayo inafanya Wafanyakazi wengi hasa wa ngazi ya chini ikiwemo wahadhiri kusota kwa njaa muda mwingi.
Kusoma zaidi hoja hizo bofya hapa ~ Chuo Kikuu Huria Tanzania lipeni Waajiriwa wenu pesa zao za kujikimu, mtawaua njaa na kuwafedhehesha mtaani
UFAFANUZI WA OUT
Chuo kinafanya jitihada mbalimbali kufuatilia suala hilo na hata katika mahafali ya Mwaka 2024, Makamu Mkuu wa Chuo alizungumza hilo tukiwa Kigoma, mbele ya Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, alimkumbusha hilo jambo ili akisaidie chuo malipo hayo yaweze kulipwa.
Kuhusu malipo ya fedha za kujikimu, kwa ujumla chuo kinajitahidi sana kulipa stahiki za kujikimu kwa wakati na iwapo malipo yanachelewa basi kunakuwa na sababu za msingi ambapo mtumishi hupewa taarifa kwa wakati.
Lakini pia kuna wakati Mtumishi anaweza kwenda safari, akalipwa, akichelewa kufanya marejesho hawezi kulipwa hela nyingine haijarejeshwa.
Pia mfumo wa malipo unapoanza kutumiwa, mbele huwa kunatakiwa watu wa kusaini au kupitisha, inaweza kutokea mtu mmoja au wawili wanaotakiwa kupitisha hawapo, hivyo inachangia malipo kuchelewa.
Inaweza kutokea pia Mtumishi mwenyewe kakosea au kachelewa kufanya mchakato na hivyo mfumo unapata changamoto.
Tangu Awamu iliyopita ya Serikali, fedha zote za Taasisi zinaingia BoT (Benki Kuu ya Tanzania), hivyo kunakuwa na mchakato wa kutoka taasisi moja kwenda nyingine.
Kuhusu Program za mafunzo ya ana kwa ana zimekuwa zikiendelea na hata wiki iliyopita zimefanyika kadhaa, kinachotokea kukitokea kukwama kwa mawasiliano kati ya Mwanafunzi na Mkufunzi kunaweza kusababisha ionekane kama mafunzo hayo hayafanyiki.
Pia Soma:
~ Chuo Kikuu Huria - Singida kiboreshe mazingira yake, ni kama vile kimetelekezwa
~ Uongozi wa Chuo Kikuu Huria wasema utaboresha mazingira ya Kampasi ya Singida