Madai ya jukwaa la wakristo hayana ukweli

Dragunov Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
2,795
Reaction score
9
Jukwaa la Wakristo Tanzania madai yenu kuhusu suala la ulinzi na usalama nawashauri muipate Katiba Inayopendekezwa na muisome kwa makini Katiba hiyo katika SURA YA 17 mtapata majibu mazuri ya wasiwasi wenu kuhusu usalama wa nchi.


Kuhusu suala la Muundo wa Serikali, wajameni SURA YA 7 ya Katiba Inayopendekezwa imeeleza wazi wazi juu ya Muundo wa Jamhuri ya Muungano katika IBARA YA 73.


Kuhusu masuala ya mauaji ya watu wenye ualbino, nadhani kila siku mnasikia wahusika wanavyokamatwa haswa waganga wa jadi pamoja na wauaji, lakini pia kuna kesi mbalimbali zinaendelea na nyingine zimeshatolewa hukumu kali.


Kuhusu kuwataka waumini wenu wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu mlizozitaja hapo mmechemsha, kwasababu msidhani kuwa waumini wote watafanya hivyo, nina amini wapo waumini wenye busara na wenye uelewa juu ya ukweli wa mambo mazuri yaliyoelezwa ndani ya Katiba Inayopendekezwa ambao hawatapoteza haki yao ya kufanya hivyo mlivyopanga.


Lakini pia hivi hamuoni kuwa mtakuwa mmemkosea Mwenyezi Mungu kwa kuwashinikiza waumini wenu waipinge Katiba hiyo? Kwani hata Biblia yenyewe inasema “ya Kaisari mpeni Kaisari nay a Mungu mpeni Mungu”, sasa udikteta huo mnaowafanyia waumini mmeupata wapi? Dini mnaiingiza na siasa tena jamanai? Tanzania ni nchi isiyokuwa na dini, kuweni makini msije mkaulizwa na Muumba wenu je kwanini mliwanyima haki waumini wenu katika Mamlaka ya Dunia. Kuwenu mfano wa mbele katika kuelimisha waumini badala ya kuwashinikiza waikatae. Huo sio uungwana kabisaaaaa!.
 

waambie hao wanajukwaa la wakristo manaake wamegeuza dini kuwa siasa, biblia ina maneno mengi na mazuri ya kuwaelimisha waumini wao lakini wanatumia mda mwingi kujadili ishu za siasa badala ya kujadili ishu za maandiko matakatifu!! Mtakuja kuulizwa na mwenyezi mungu, kwani mnachokifanya kwa sasa ni kuwanyima haki za msingi waumini wenu, nyie tunawaamini muwe mstari wa mbele kuelimisha waumini juu ya masuala ya nchi likiwemo hili la katiba, lakini mnatoa hoja za ajabu ambazo dah haziendani kabisa na vyeo vyenu vya makanisa. Lakini kumbukeni kuwa hatimae mwisho mwishowe wema utashinda tu, hata kwenye biblia zenu imeandikwa hivyo.
 
Kweli waambie kwani nao ni wanadamu. Kwa hili wamejikwaa lakini hawajaanguka. Nadhani wameshajirudi na nadhani leo makanisani watakuwa wamebadili maubiri na kuwataka waumini wao waipigie kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa.
 
#1
Junior MemberArray


Join Date : 14th March 2015
Posts : 2
Rep Power : 0
Likes Received3
Likes Given2


[h=2]
Madai ya jukwaa la wakristo hayana ukweli[/h]
POLE SANA SNAKE!

 

Yako ndio yana ukweli.
 
Kweli waambie kwani nao ni wanadamu. Kwa hili wamejikwaa lakini hawajaanguka. Nadhani wameshajirudi na nadhani leo makanisani watakuwa wamebadili maubiri na kuwataka waumini wao waipigie kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa.

Huu mwaka mamento fresh mtakuwa wengi sana.
 
Angalia ni jukwaa la wakristo sio jukwaa la ukristo.
 

@#$*****?!
 
Ni kweli mkuu. Hadi wanafungua ID za dharura leo leo ili wasionekane hadharani wao ni nani. Hii ni tabia ya nyoka wenye hila na sumu kali. Kwa hii ndiyo untazidi kukoleza kabisa kwamba KATIBA YA CHENGE HAPANA!

Wana mpngao wa kutugawa waTanzania. Shura ya maimamu nao walishaikataa tena walikuwa wa kwanza kutoa tamko kama taasisi za dini. Waislam nao wote KATIBA YA CHENGE HAPANA!.

Wanaccm wenyewe waliokuwa wanashurutishwa na wasira wako pamoja na makundi haya mawili kwa misingi ya utaifa na kwamba wamekuwa wakitumikishwa kifikra kwa maslahi ya mafisadi. sasa wana ccm KATIBA YA CHENGE HAPANA".

Ukawa tuko pamoja na ninyi "KATIBA YA CHENGE HAPANA!.

Wakapige kura ya ndiyo mafisadi na familia zao lakini tutadhibiti kwanye kuhesabu na hata wakilazimisha kuipitisha kwa hila kama walivofanya BMK, bado haitekelezwi kwa nguvu ya umma na hata hawa mafisadi, wasahau kukaa kwa amani labda wahame nchi. Huwezi kuwa na amani kati kati ya watu wenye mateso na uchungu!.

Naona watawala wameshaanza kujambajamba
 
Ijumaa ijayo Jukwaa la waislam tutatoa waraka wetu. Na kwa vile tupo wengi, bara na visiwani, wakwetu tutahamasisha katiba.

Baada ya hapo, kwa wale wasio na Dini na waganga wa jadi mje na waraka wenu
 
HAPANA KWA KATIBA YA CHENGE, dawa ya ccm ni kuwachoma moto tu msitulazimishe upumbavu wenu!
 
Kila mtu na utashi wake kamwe hakuna mtu au askofu wala padri au mchungaji hata shehe ambaye ataweza kutupangia nini chakufanya.

kila mtu asome katiba na kuamua kivyake siyo kupangiwa na mtu yeyote yule.
 
Wajinga ndio waliwao...hata sitoi povu maana tayar mia mbili IPO...il a nnalowwza kusema msikilizeni mtumishi Wa bwana
 
#1

junior memberarray


join date : 14th march 2015
posts : 2
rep power : 0
likes received3
likes given2


madai ya jukwaa la wakristo hayana ukweli



pole sana snake!


toa hoja acha matusi, hakuna snake hapa
 
jamani acheni kupotosha; wananchi wameambiwa washiriki lakini wapige kula ya hapana sasa udikteta hupo wapi? madikteta ndo wale walio yakataa maoni Ya wananchi ccm kwisha.
 

hujitambui ndo mana unapayuka payuka bila hoja zenye mantiki pole sana hii itapita
 
Mmebaki wachache sana, na mtajikuta jangwani peke yenu. Watanzania tumeshaamua 'KATIBA YA CHENGE HAPANA!. Matusi ya mwendawazimu huwa hayaumi kwa sababu ni sehemu ya wehu wake na hayabadilishi ukweli.


hujitambui ndo mana unapayuka payuka bila hoja zenye mantiki pole sana hii itapita
 
Tena wakaenda mbele zaidi kwamba "mwana ccm atakayeipigia katiba kura ya hapana, arudishe kadi". Anataka udikteta utoke hapa uende wapi?

jamani acheni kupotosha; wananchi wameambiwa washiriki lakini wapige kula ya hapana sasa udikteta hupo wapi? madikteta ndo wale walio yakataa maoni Ya wananchi ccm kwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…